Magari ya Japan (Japanese used cars) za kununua 2026!

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
35,566
Reaction score
104,386
Wakuu.
Tujaribu kulist magari yaliyotumika Japan ambayo ni rafiki kununua kwa mwaka 2026 (maybe na kuendelea). Nimeanza mimi kwa kuyaweka hapa, maelezo kidogo, ila unaweza kudiscuss zaidi.

Vigezo nilivyotumia:
-Gharama (kuna category ya chini ya Mil 20 na nyingine Mil 20+)!
-Fuel efficiency (ndio maana mengi hybrid au engine ndogo)
-YOM (zilizotengenezwa kuanzia 2010-2020)
-Bei za online reference nitatumia Beforward.
-Gharama za kurun, maintenance na kupatikana kwa spare Tanzania.
Note: Vingine naweza kukosea utarekebisha, au utaongezea.

Category I: Chini ya Milion 20!

1. Toyota Aqua (2012–2014)


Hii inaitwa Prius C, ni hybrid nzuri sana. Engine ndogo 1.5L yenye kukupatia 25 km/L bila shida.
Kuipata mtandaoni unaipata kuanzia $3,000 na ushuru kuanzia Mil 7.5!

2. Suzuki Swift Hybrid (2015+)


Hii 3rd gen ya Suzuki Swift ina option ya hybrid, non hybrid na turbo. Engine ndogo, performance kubwa na muonekano mzuri kuliko generation ya nyuma.

Hybrid ina engine options nyingi sana. Ina 1.2L, 1.25L, 1.3L, 1.4L ushindwe wewe tu.
Beforward utaipata kuanzia $3,500 iliyo kwenye hali nzuri na TRA watataka kuanzia kama Mil 7.5 hivi kutegemea na mwaka na engine size.

Mazda Demio (SkyActiv 2012–2014)


Kuanzia mwaka 2014 Demio ilijiunga na SkyActiv engine, na koddo design. Ukiachana na Demio za nyuma zilizokua na muonekano “wa kawaida”, hii sasa ukiiona unaweza dhania ni Axela. Kazuri sana.

Ukipata 2.0L Sio hybrid, ila SkyActiv inajulikana kwa best fuel efficient. Ukipata 1.5L ni hybrid. Note: Isiwe Diesel.

Beforward unaipata kuanzia CIF ya $3,300 hivi au less, na ushuru utaanzia Mil 7.8 hivi.

Honda Fit Hybrid (GP1/GP5 2010–2017)

Hapa utachagua Hybrid ya 2nd generation (GP1) ya 2013 kurudi nyuma.

Au Hybrid ya 3rd gen GP5 ya kuanzia 2014+

Zote nzuri ila GP5 more efficient, inakupa 25 km/L bila stress wakati GP1 inaenda kwenye 14-16 km/L. Sababu kuu ni hybrid system wanazotumia, GP1 ni Hybrid Assist wakati GP5 ni parallel hybrid.

TRA watataka kama Mil 7.5 hivi wakati kuipata kwa $3,500 au less ni easy.

Toyota Prius (ZVW30 2010–2012)


Huyu ndio best selling hybrid worldwide. Hana haja kutangazwa, kama una pesa mnunue.

Category II: Premium & SUV (Juu ya Milion 20)
Honda Vezel Hybrid (2013–2015)

Toyota Sienta Hybrid (2015+)

Toyota C-HR (2016+)

Toyota Corolla Cross Hybrid (2020+)

Nissan Note e-Power (2016+)

Honda CR-V Hybrid

Nissan X-Trail e-Power / Hybrid (T32)

Subaru XV Hybrid (2013–2015)

Mitsubishi Outlander PHEV (2013–2015)

Suzuki Escudo Hybrid (2015+)


Unaonaje list?
Nimeachana na magari premium ya Ulaya tumeona tufocus kwa Japanese tu.
 
Hiyo demio mbona bei kitonga, vipi heka heka za off-road anaweza, ground clearance yake ipoje, ndoto zangu za kuvuta Harrier zishafifia na mwaka huu nataka niendeshe gari hilo nimeapa
Demio bei rafiki kinoma. Mchawi wetu TRA ndio anasababisha iende mbali ila ilitakiwa tusinunue zaidi ya Mil 15.

Off-road na ground clearance inaweza kua changamoto. Kako chini sana.
 
Chuma kali inavutia sana mkuu. Chini ya Mil 25 unaagiza mwenyewe JP.

Ila kama una option nyingine ifikire, CX5 labda iwe ya Petrol. Hizi za Diesel tukiacha ushabiki bado tunazokosea sisi watumihaji na mafundi.
Pamoja na tra au ni 25 pekee bila ushuru .
Afu wanasemaga tatizo lake kuu sijui PDC (utanisahihisha) lakin katita chuma nakubali hii mama design ya nje tu sio poa...
 
Kiongozi nataka kujilipua VOLKASWAGEN TOUREG ya mwaka 2007 - 8 CIF $6,200 ya kuagiza mwenyewe bila Agent, bajeti yangu ni ML 26 pamoja na ushuru. Je bajeti yangu inatosha kulingana na uzoefu wako.

TRA inasoma 10,900,000 TZs
Mkuu, kama CIF inapatikana kwa hiyo bei $6,200 ambayo ni kama Mil 16 na Ushuru Mil 11 inamaana kama Mil 27 hivi.

Gharama za Agent, Port, Shipping Line etc hazitavuka Mil 1.5 hivi.

Kwahiyo safe side ni Mil 28.5 hadi 30 hivi.

Ila unalikubali sana Touareg au?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…