Magari ya Japan (Japanese used cars) za kununua 2026!

Magari ya Japan (Japanese used cars) za kununua 2026!

Mkuu, kama CIF inapatikana kwa hiyo bei $6,200 ambayo ni kama Mil 16 na Ushuru Mil 11 inamaana kama Mil 27 hivi.

Gharama za Agent, Port, Shipping Line etc hazitavuka Mil 1.5 hivi.

Kwahiyo safe side ni Mil 28.5 hadi 30 hivi.

Ila unalikubali sana Touareg au?
Kuna baadhi ya member naona wanamiliki haya magari, utakuta ni namba B au A au C na chuma zimenyooka na hawazi kuuza.
 
Mimi sitaki kununua used tena ....nanyooka kwa wachina hapo bongo nichukue pure EV au range extended EV .....
Jamaa wanatoa warrant ndefu sana...
 
Mimi sitaki kununua used tena ....nanyooka kwa wachina hapo bongo nichukue pure EV au range extended EV .....
Jamaa wanatoa warrant ndefu sana...
Nadhani PHEV au REEV ndio mwendo sahihi. Stress za mafuta unaachana nazo kabisa.
 
Tunaomba orodha ya magari yanayositahimili barabara zetu za rough road huku vijijini ambayo hata ukiendea shamba linavumilia shida.

Gari bei yake isizidi 15-25M, service iwe rafiki na mafuta inywe na siyo kubugia.
Sawa mkuu, ngoja niifanyie kazi.
 
Wakuu.
Tujaribu kulist magari yaliyotumika Japan ambayo ni rafiki kununua kwa mwaka 2026 (maybe na kuendelea). Nimeanza mimi kwa kuyaweka hapa, maelezo kidogo, ila unaweza kudiscuss zaidi.

Vigezo nilivyotumia:
-Gharama (kuna category ya chini ya Mil 20 na nyingine Mil 20+)!
-Fuel efficiency (ndio maana mengi hybrid au engine ndogo)
-YOM (zilizotengenezwa kuanzia 2010-2020)
-Bei za online reference nitatumia Beforward.
-Gharama za kurun, maintenance na kupatikana kwa spare Tanzania.
Note: Vingine naweza kukosea utarekebisha, au utaongezea.

Category I: Chini ya Milion 20!

1. Toyota Aqua (2012–2014)

View attachment 3567838
Hii inaitwa Prius C, ni hybrid nzuri sana. Engine ndogo 1.5L yenye kukupatia 25 km/L bila shida. View attachment 3567858
Kuipata mtandaoni unaipata kuanzia $3,000 na ushuru kuanzia Mil 7.5!

2. Suzuki Swift Hybrid (2015+)

View attachment 3567839
Hii 3rd gen ya Suzuki Swift ina option ya hybrid, non hybrid na turbo. Engine ndogo, performance kubwa na muonekano mzuri kuliko generation ya nyuma.
View attachment 3567863
Hybrid ina engine options nyingi sana. Ina 1.2L, 1.25L, 1.3L, 1.4L ushindwe wewe tu.
Beforward utaipata kuanzia $3,500 iliyo kwenye hali nzuri na TRA watataka kuanzia kama Mil 7.5 hivi kutegemea na mwaka na engine size.

Mazda Demio (SkyActiv 2012–2014)

View attachment 3567840
Kuanzia mwaka 2014 Demio ilijiunga na SkyActiv engine, na koddo design. Ukiachana na Demio za nyuma zilizokua na muonekano “wa kawaida”, hii sasa ukiiona unaweza dhania ni Axela. Kazuri sana.
View attachment 3567877
Ukipata 2.0L Sio hybrid, ila SkyActiv inajulikana kwa best fuel efficient. Ukipata 1.5L ni hybrid. Note: Isiwe Diesel.
View attachment 3567879
Beforward unaipata kuanzia CIF ya $3,300 hivi au less, na ushuru utaanzia Mil 7.8 hivi.

Honda Fit Hybrid (GP1/GP5 2010–2017)

Hapa utachagua Hybrid ya 2nd generation (GP1) ya 2013 kurudi nyuma.
View attachment 3567841
Au Hybrid ya 3rd gen GP5 ya kuanzia 2014+
View attachment 3567842
Zote nzuri ila GP5 more efficient, inakupa 25 km/L bila stress wakati GP1 inaenda kwenye 14-16 km/L. Sababu kuu ni hybrid system wanazotumia, GP1 ni Hybrid Assist wakati GP5 ni parallel hybrid.

TRA watataka kama Mil 7.5 hivi wakati kuipata kwa $3,500 au less ni easy.

Toyota Prius (ZVW30 2010–2012)

View attachment 3567843
Huyu ndio best selling hybrid worldwide. Hana haja kutangazwa, kama una pesa mnunue.

Category II: Premium & SUV (Juu ya Milion 20)
Honda Vezel Hybrid (2013–2015)
View attachment 3567844
Toyota Sienta Hybrid (2015+)
View attachment 3567845
Toyota C-HR (2016+)
View attachment 3567846
Toyota Corolla Cross Hybrid (2020+)
View attachment 3567847
Nissan Note e-Power (2016+)
View attachment 3567848
Honda CR-V Hybrid
View attachment 3567854
Nissan X-Trail e-Power / Hybrid (T32)
View attachment 3567853
Subaru XV Hybrid (2013–2015)View attachment 3567851

Mitsubishi Outlander PHEV (2013–2015)View attachment 3567850

Suzuki Escudo Hybrid (2015+)
View attachment 3567849

Unaonaje list?
Nimeachana na magari premium ya Ulaya tumeona tufocus kwa Japanese tu.
Ok
 
Back
Top Bottom