Kila siku Serikali kupitia vitengo vyake mbalimbali wanabuni njia za kuongeza mapato.
Tozo mpya ya shilingi milioni moja kwa magari yanayokodishwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo ya kubeba miili ya marehemu inatazamiwa kupitishwa na kuanza kutumika, kumbuka tozo hiyo inayosimamiwa na (LATRA)

- Tunachokijua
- Mamlaka ya usafiri ardhini LATRA ilikanusha kuanzisha tozo kwa magari madogo ya kubeba maiti kupitia taarifa iliyorushwa na kituo cha Habari cha ITV.
Kanusho hilo lilibainisha kuwa mabasi madogo yenye uwezo wa kubeba abiria 14 hadi 30 ndio walengwa wa tozo na si magari ya kubeba maiti.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa usafirishaji Johansen Kahatano amesema Serikali haijawahi kufikiria kuanzisha tozo ya namna hiyo. Taarifa ya kuanzisha tozo kwenye magari ya kubeba maiti ni za kuzushwa tu.