My understanding:
1. Taifa Tanzania- Karamagi
2. Taifa Letu - Mengi
3. Sema usikike - Mengi
Do you have idea hayo magazeti ni ya udaku au ya habari?kama ukiweza kunipa wahariri wake utanisaidia sana.
Mengi ana matatizo gani,analalamika wanamchafua wakati na yeye anachafua?
Mzee Mwanakijiji: I don't want to sound cynical but that is what I am about to write will sound like: Newspapers like other commodities is demnad and supply. Kama watanzania tunapenda kusoma malumbano ya wakubwa au kuangalia picha za ngono na ufuska, wacha tuendelee kuangalia, why? Because unapokataza ndo inazidi kuwa object of desire. Mi nadhani censorship imepitwa na wakati, kama watu wasingenunua magazeti haya wasingeyachapisha.
MIMI NAULIZA SWALI TU KWA KUWA BANGI, KOKEINI (MADAWA YA KULEVYA)ZINA WATEJA TUSIPIGE MARUFUKU?
Duh..mkuu, unakimbia majukumu . Jamii yoyote ni lazima iwe inalinda haki za raia wake wote bila kuangalia maslahi ya kibiashara.
Kakuju: comparison nzuri sana! Sasa je unafahamu kuwa katika baadhi ya mataifa bangi ni halali? Na je unafahamu kuwa katika nchi ya Holland, hata ecstasy n.k. pia vimehalalishwa na vinauzwa kihalali. Cocaine haiuzwi kutokana na kuwa ina madhara makubwa sana ya afya. lakini udaku na picha za ngono hazina athari za kiafya ni ya kufurahisha macho!
Pia ukiangalia demand and supply ya madawa ya kulevya mara nyingi imethibitika kwamba inapokuwa na adhabu kubwa sana na idhini nyingi, bei yake hupanda sana na hivyo kuwavutia watu wengi zaidi kujiingiza katika biashara hiyo. Same applies for udaku and ngono tukisema tutazipiga marufuku.
Sijawahi kuona mtu anayefikiria kwa nguvu halafu akafikiria vitu vya ajabu kama wewe!!
Duh..mkuu, unakimbia majukumu . Jamii yoyote ni lazima iwe inalinda haki za raia wake wote bila kuangalia maslahi ya kibiashara.
Hivi kashfa ya Monica Lewinky na Clinton si maisha ya mtu binafsi? kwanini uliendeshwa mchakato wa kutaka kumtoa Clinton kwenye ofisi ya urais? Wakina nani waliitoa hii habari?
Republicans. Walidhani wamemmaliza Clinton.Hivi kashfa ya Monica Lewinky na Clinton si maisha ya mtu binafsi? kwanini uliendeshwa mchakato wa kutaka kumtoa Clinton kwenye ofisi ya urais? Wakina nani waliitoa hii habari?
Republicans. Walidhani wamemmaliza Clinton.
Mengi Vs Karamagi? Mengi Vs Masha? Mengi Vs Manji? Mengi Vs Masilingi? and the list goes on and on. Hapa naona wengi mmeanza kupata picha. Huyu jamaa ana matatizo gani? Kwanini yeye ndio mtu wa kulumbana na wenzake tu kila siku? Kwani yeye ndio mfanyabiashara pekee mwenye mafanikio hapa nchini? Mbona wako wengine wengi tu (hata kama hawamfikii Mengi) wenye mafanikio? Mbona hatusikii wakilumbana na wanasiasa? Au kwasababu hawamiliki vyombo vya habari? Na hii vita huwa anashinda nani? Mengi au wapinzani wake? Vita kati ya Mengi Vs Masilingi, nani alishinda?
Tafakari, jiulize.............
Zero nadhani bado uko zero katika hii topic. Ni vyema ukaanzia huku
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-ya-karamagi-co-dhidi-ya-jakaya-kikwete.html
Na ujue JF ilijua Old 17th November 2008, 01:58 AM kipindi ambacho hata hao kina Karamagu walikuwa hawajaanzisha hayo magazeti. Unapomtaja Karamagi, Masha, Manji umesahau kumtaja Lowassa, Chenge, Mahalu na wenzake ambao kwa kiasi kikubwa umma unawajua wako kundi gani. Kwa bahati mbaya sana baada ya kuanguka kwa Lowassa, waliamini moja kwa moja kwamba kuanguka huko kulitokana na magazeti na kwa kiwango kikubwa yanayochapishwa na kampuni za Mengi na yale ambayo Mengi anayaunga mkono pamoja na yale yasiyo na upande yakiwamo ya UHURU na Daily NEws. Wakaona dawa na wao kwa kuwa wana fedha wawekeze katika media. Rostam na EL wakatangulia kununua Habari Corp (RAI, Mtanzania na The African) na wao wakawekeza mamilioni. Kama ilivyofahamika na JF mapema, wakaanza kuwashughulikia watu wanaoamini kuwa wabaya wao, kina Samuel Sitta, MWakyembe, Anne Kilango, Ole Sendeka, na baadaye wakaanza kumsakama Mengi. Hii vita haikuanzia kwenye hizo picha za juzi zilizogeuzwa kuwa za harusi (ambayo si wizi), ilianza hata kabla. Baada ya Mengi kulalamika kwa njia isiyo rasmi, akalalamika hadharani mara nyingi, humu ndani JF na kwingineko watu wakambeza kwa kulia lia na Mkuchuka, MCT,Spika Sitta wakakaa kimya. Sasa Mengi akaona kumbe ni HALALI (kama ilivokuwa kwa umma kuua majambazi) akaanzisha Sema Usikike na kufufua Taifa Letu, kwa nguvu. makombora yake yakawagusa pabaya wahusika na Mengi akaangaza kwamba wao walianza kwa kutunga uongo na waandishi makini wakianza kuandika UKWELI wa uchafu wao wasilalamika. Hata kabla hawajlalamika, Mkuchika (Serikali) ikaingilia kati na sasa imetaja magazeti matatu, mawili ya mengi na moja la Karamagi, akiacha mengine kibao ya kundi la kina Karamagi likiwamo (Umma) lililosambazwa Bungeni na lile la Sati Huru, ambalo liliandika mambo ya matusi kabisa ya nguoni kumtukana Mengi. Mkuchika hakuyaona hayo, hakuliona Tazama, hakuliona Nyundo ambayo atataka yaendelee kufanya kazi ya kuwashambulia kina MWakyemba na kuwasafisha kina Kamaragi na Lowassa. JF AMKENI MUWAAMSHE WATANZANIA WETU.
MUNGU YUKO NA WAPENDA HAKI MILELE