Zero nadhani bado uko zero katika hii topic. Ni vyema ukaanzia huku
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-ya-karamagi-co-dhidi-ya-jakaya-kikwete.html
Na ujue JF ilijua Old 17th November 2008, 01:58 AM kipindi ambacho hata hao kina Karamagu walikuwa hawajaanzisha hayo magazeti. Unapomtaja Karamagi, Masha, Manji umesahau kumtaja Lowassa, Chenge, Mahalu na wenzake ambao kwa kiasi kikubwa umma unawajua wako kundi gani. Kwa bahati mbaya sana baada ya kuanguka kwa Lowassa, waliamini moja kwa moja kwamba kuanguka huko kulitokana na magazeti na kwa kiwango kikubwa yanayochapishwa na kampuni za Mengi na yale ambayo Mengi anayaunga mkono pamoja na yale yasiyo na upande yakiwamo ya UHURU na Daily NEws. Wakaona dawa na wao kwa kuwa wana fedha wawekeze katika media. Rostam na EL wakatangulia kununua Habari Corp (RAI, Mtanzania na The African) na wao wakawekeza mamilioni. Kama ilivyofahamika na JF mapema, wakaanza kuwashughulikia watu wanaoamini kuwa wabaya wao, kina Samuel Sitta, MWakyembe, Anne Kilango, Ole Sendeka, na baadaye wakaanza kumsakama Mengi. Hii vita haikuanzia kwenye hizo picha za juzi zilizogeuzwa kuwa za harusi (ambayo si wizi), ilianza hata kabla. Baada ya Mengi kulalamika kwa njia isiyo rasmi, akalalamika hadharani mara nyingi, humu ndani JF na kwingineko watu wakambeza kwa kulia lia na Mkuchuka, MCT,Spika Sitta wakakaa kimya. Sasa Mengi akaona kumbe ni HALALI (kama ilivokuwa kwa umma kuua majambazi) akaanzisha Sema Usikike na kufufua Taifa Letu, kwa nguvu. makombora yake yakawagusa pabaya wahusika na Mengi akaangaza kwamba wao walianza kwa kutunga uongo na waandishi makini wakianza kuandika UKWELI wa uchafu wao wasilalamika. Hata kabla hawajlalamika, Mkuchika (Serikali) ikaingilia kati na sasa imetaja magazeti matatu, mawili ya mengi na moja la Karamagi, akiacha mengine kibao ya kundi la kina Karamagi likiwamo (Umma) lililosambazwa Bungeni na lile la Sati Huru, ambalo liliandika mambo ya matusi kabisa ya nguoni kumtukana Mengi. Mkuchika hakuyaona hayo, hakuliona Tazama, hakuliona Nyundo ambayo atataka yaendelee kufanya kazi ya kuwashambulia kina MWakyemba na kuwasafisha kina Kamaragi na Lowassa. JF AMKENI MUWAAMSHE WATANZANIA WETU.
MUNGU YUKO NA WAPENDA HAKI MILELE