Magazeti yapewa siku saba kujieleza - Mkuchika

Magazeti yapewa siku saba kujieleza - Mkuchika

My understanding:
1. Taifa Tanzania- Karamagi
2. Taifa Letu - Mengi
3. Sema usikike - Mengi

Do you have idea hayo magazeti ni ya udaku au ya habari?kama ukiweza kunipa wahariri wake utanisaidia sana.

Mengi ana matatizo gani,analalamika wanamchafua wakati na yeye anachafua?
 
Do you have idea hayo magazeti ni ya udaku au ya habari?kama ukiweza kunipa wahariri wake utanisaidia sana.

Mengi ana matatizo gani,analalamika wanamchafua wakati na yeye anachafua?

Naona kama magazeti haya yako kati ya Udaku na ya kawaida, nikiwa namaana ya kuwa haina picha zile kubwa za rangi mbele (tabloid style ya UK au magazeti ya Shigongo), lakini habari zake zimeandikwa kiudaku.
Mengi nadhani ame-react hajaanza yeye kutoa magazeti kama haya na ni baada ya kuchafuliwa sana katika magazeti ya Karamagi.
 
Originally Posted by Susuviri
Mzee Mwanakijiji: I don't want to sound cynical but that is what I am about to write will sound like: Newspapers like other commodities is demnad and supply. Kama watanzania tunapenda kusoma malumbano ya wakubwa au kuangalia picha za ngono na ufuska, wacha tuendelee kuangalia, why? Because unapokataza ndo inazidi kuwa object of desire. Mi nadhani censorship imepitwa na wakati, kama watu wasingenunua magazeti haya wasingeyachapisha.

MIMI NAULIZA SWALI TU KWA KUWA BANGI, KOKEINI (MADAWA YA KULEVYA)ZINA WATEJA TUSIPIGE MARUFUKU?
 
Duh..mkuu, unakimbia majukumu . Jamii yoyote ni lazima iwe inalinda haki za raia wake wote bila kuangalia maslahi ya kibiashara.
 
MIMI NAULIZA SWALI TU KWA KUWA BANGI, KOKEINI (MADAWA YA KULEVYA)ZINA WATEJA TUSIPIGE MARUFUKU?

Kakuju: comparison nzuri sana! Sasa je unafahamu kuwa katika baadhi ya mataifa bangi ni halali? Na je unafahamu kuwa katika nchi ya Holland, hata ecstasy n.k. pia vimehalalishwa na vinauzwa kihalali. Cocaine haiuzwi kutokana na kuwa ina madhara makubwa sana ya afya. lakini udaku na picha za ngono hazina athari za kiafya ni ya kufurahisha macho!
Pia ukiangalia demand and supply ya madawa ya kulevya mara nyingi imethibitika kwamba inapokuwa na adhabu kubwa sana na idhini nyingi, bei yake hupanda sana na hivyo kuwavutia watu wengi zaidi kujiingiza katika biashara hiyo. Same applies for udaku and ngono tukisema tutazipiga marufuku.
 
Duh..mkuu, unakimbia majukumu . Jamii yoyote ni lazima iwe inalinda haki za raia wake wote bila kuangalia maslahi ya kibiashara.

Lakini naomba niulize hivi leo hii nini motisha kubwa ya wananchi? Uzalendo? Mapenzi na nchi yao? No! It's money, money makes the world go around! Sasa huu ni ukweli , and I know that I may not agree with this view but I have to face it as reality.
Ukisema jamii ilinde haki za raia wake, nauliza:
a) nani ataweka sheria ya kulinda haki hizi? Je huyu mlinzi ana upeo gani na uwezo gani wa kufanya maamuzi kuwa haki za wnaanchi milioni 35 ni nini?
b) who protects the minority? Kama kila raia basi tuangalie pia minority ambao wanaweza kuwa na interest tofauti na majority (nadhani wenzangu mnaopinga magazeti ya udaku na ngono you are a minority), na ni wakati gani inakubalika kuwa the minority's rights are more important than the majority?

Kwa hiyo ujue sijachukulia ishu hii kirahisi nilipomwandikia jibu Mzee Mwanakijiji.
 
BINAFSI mimi sioni shida ya hayo magazeti. Whatever they write waandike atakaye taka kununua anunue asiyetaka aache. Mfano mimi sijawahi kusoma magazeti ya udaku though yako kila kona. So it is a free market economy waache wenyekuzipenda habari hizo wazipate. By the way hata zisipoandikwa magazetini unaweza kuzipata elsewhere kama kwenye internet etc etc. I think through that way tutakuwa tunawajua the real people that we want them to lead us, i mean we would be able to make an informed decision on the people tunaotaka watuongoze. Kama mimi binafsi nikijua jamaa ni mchafuzi wa wake za watu then sitamconsider kumpigia kura pengine somebody else atampigia. I think that is what we call Democrasia. Waache waseme na waandike TUWAJUE. No fussy no mussy.
 
Mengi Vs Karamagi? Mengi Vs Masha? Mengi Vs Manji? Mengi Vs Masilingi? and the list goes on and on. Hapa naona wengi mmeanza kupata picha. Huyu jamaa ana matatizo gani? Kwanini yeye ndio mtu wa kulumbana na wenzake tu kila siku? Kwani yeye ndio mfanyabiashara pekee mwenye mafanikio hapa nchini? Mbona wako wengine wengi tu (hata kama hawamfikii Mengi) wenye mafanikio? Mbona hatusikii wakilumbana na wanasiasa? Au kwasababu hawamiliki vyombo vya habari? Na hii vita huwa anashinda nani? Mengi au wapinzani wake? Vita kati ya Mengi Vs Masilingi, nani alishinda?

Tafakari, jiulize.............
 
Mbona ameyazungumzia hayo tu? Yale ya Global publishers ni almost yote yana habari za maisha binafsi ya watu
 
Kakuju: comparison nzuri sana! Sasa je unafahamu kuwa katika baadhi ya mataifa bangi ni halali? Na je unafahamu kuwa katika nchi ya Holland, hata ecstasy n.k. pia vimehalalishwa na vinauzwa kihalali. Cocaine haiuzwi kutokana na kuwa ina madhara makubwa sana ya afya. lakini udaku na picha za ngono hazina athari za kiafya ni ya kufurahisha macho!
Pia ukiangalia demand and supply ya madawa ya kulevya mara nyingi imethibitika kwamba inapokuwa na adhabu kubwa sana na idhini nyingi, bei yake hupanda sana na hivyo kuwavutia watu wengi zaidi kujiingiza katika biashara hiyo. Same applies for udaku and ngono tukisema tutazipiga marufuku.

Sijawahi kuona mtu anayefikiria kwa nguvu halafu akafikiria vitu vya ajabu kama wewe!!
 
Last edited:
Sijawahi kuona mtu anayefikiria kwa nguvu halafu akafikiria vitu vya ajabu kama wewe!!

Heheheheee...mwache bana huyo rafiki yangu...huwaga anapata "tingly feeling up his leg" kila amsikiapo Obama akiongea....Lol
 
Duh..mkuu, unakimbia majukumu . Jamii yoyote ni lazima iwe inalinda haki za raia wake wote bila kuangalia maslahi ya kibiashara.

Na, haki za raia zilindwe na sheria siku zote. Siyo hasira mbele ya mic. ili tuamini wewe ni mkali. NO! NO! NO!

Hiyo privacy inayotakiwa kulindwa ni ipi?
Kwa mwananchi wa kawaida kama mimi napenda sana kusikia na kumfahamu waziri mpenda mashoga ambaye kwa siku zote sikufahamu kama ana tabia hiyo. Ukisha kuwa public figure, mind your steps. Usitake kufanya ufuska eti uachwe kwa kisingizio cha privancy.

Mbona huyo mkuchika hajawahi kusema lolote juu ya wale ambao kila siku tunawaona kwenye magazeti ya ‘udaku’? Tena wakitajwa kwa majina au kwa kuwa siyo wanasiasa?

Ubaya ni KUSINGIZIA mtu kitendo kibaya kama hicho gazetini. Lakini ukifanya mambo yasiyokuwa ya ki-maadili unategemea wakuandike kwa maadili!

Awe Mengi aandikwe, awe Spika aandikwe, awe mkulima aandikwe pia. Lakini wote hao wasisingiziwe. Na wakidhani wamesingiziwa waende kwenye vyombo vya sheria. FINITO!
 
Hivi kashfa ya Monica Lewinky na Clinton si maisha ya mtu binafsi? kwanini uliendeshwa mchakato wa kutaka kumtoa Clinton kwenye ofisi ya urais? Wakina nani waliitoa hii habari?
 
SPIKA wa Bunge Samuel Sitta jana aliomba radhi kwa kuachia nakala za magazeti yanayoonekana kuwa ya habari za udaku kusambazwa ndani ya kikao cha Bunge la Jamhuri, akisema kuwa "alipitiwa".

Juzi, kabla ya kufungwa kwa Mkutano wa 14 wa Bunge, waziri mmoja 'kijana' anasemekana kununua nakala zote za gazeti hilo linaloandikwa kwa lugha ya Kiswahili na ambalo linatoka kwa wikina kuwapa wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge kugawa kwa kila mbunge.

Habari zilizoandikwa kwenye gazeti hilo zinaonekana kuwa ni za kushabikia tuhuma kuwa mfanyabiashara mmoja amefunga ndoa na uandishi wa habari hizo hauonekani kuheshimu maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.

"Nilipitiwa na kushtukia magazeti yamegawiwa kwa wabunge ndani ya ukumbi," alisema Spika Sitta akizungumza kitendo cha magazeti hayo kusambazwa na wafanyakazi wa Bunge wakati kikao kikiendelea.

Gazeti hilo jipya linaitwa "Sauti ya Umma" na tarehe zilizochapishwa juu ya kurasa zake zinaonyesha kuwa lilitakiwa kuwa sokoni kuanzia Februari 12, lakini lilitua Dodoma juzi jioni. Kuna habari zinasema kuwa nakala za gazeti hilo zilisafirishwa kwa ndege kuwahi Bunge.

"Baada ya kusoma habari hizo, niligundua kuwa habari zilizoandikwa zilikuwa ni mbaya," alisema Sitta. "Nilichukia sana baada ya kuyasoma na kugundua kuwa yalikuwa na habari hizo. Ni kitu kibaya sana.

"Nilipitiwa... hiyo ni hali ya kawaida ya kibinadamu. Mambo kama hayo hutokea... naomba hilo liishie hapo."

Katika siku za karibuni kumezuka magazeti mpya na mengine yakiwa yamefufuliwa ambayo yamekuwa yakiandikwa habari za mwandani wa watu maarufu, hasa wafanyabiashara na wanasiasa.

Habari nyingi kati ya hizo zimekuwa ni kuhusu maisha yao ya ndoa, ufuska na uchafu wa shughuli zao za kisiasa na kibiashara.

Sitta pia alisema kuwa kumekuwa na baadhi ya wabunge wanaolalamika kuwa analipeleka puta bunge na kusema kuwa maneno yao yanatokana kutojua anachotaka kifanyike na kwamba yeye ni mtu wa kanuni na anaamini kuwa ataendelea kuwa hivyo siku zote.

Spika huyo, ambaye aliwahi kusema kuwa ataongoza kwa kasi na viwango, bado alikuwa anazungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za Bunge, siku moja baada ya chombo hicho cha kutunga sheria kuahirisha mkutano wake 14 juzi.

Alitolea mfano kuwa nyumba za serikali zilizouzwa kwa bei ya kutupwa ambazo ziliwekea azimio na bunge ili zirejeshwe mara moja na kwamba nyumba hizo zimeanza kurejeshwa na serikali ilitoa ufafanuzi wa kina bungeni tofauti na siku za nyuma.

Kurejeshwa kwa nyumba hizo kulitokana na hoja binafsi iliyowasilishwa bungeni na mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro alisema kuwa nyumba za serikali ziliuzwa bila ya kufuata utaratibu maalumu huku maeneo mengine yakiwa ni nyeti kabisa ambayo hayakufaa kupewa watu wengine zaidi ya serikali.

"Zamani ilikuwa ni vigumu kwa serikali kujieleza mbele ya bunge kama ilivyo sasa... sehemu kubwa ilikuwa ni ubabaishaji, lakini kwa sasa ni kujieleza kwa upana na ikitokea hakuna uhakika katika jambo fulani ni lazima tuseme kuwa bunge halijaridhika," alisema Sitta.

Alisema kuwa majibu ya serikali yanahitaji urasimu kidogo tofauti na ilivyo kwa bunge kwani serikali ikitaka kwenda kwa spidi sana inakutana na vikwazo vya kisheria.
Kuhusu yeye kuonekana kuwabana wabunge katika ukumbi wa bunge, Sitta alisema kuwa yeye hambani mtu yeyote kutokana na kufuata kanuni.
 
Hivi kashfa ya Monica Lewinky na Clinton si maisha ya mtu binafsi? kwanini uliendeshwa mchakato wa kutaka kumtoa Clinton kwenye ofisi ya urais? Wakina nani waliitoa hii habari?

Kwa sababu Clinton alidanganya kwenye kiapo (sijui kama ilikuwa ni mahakamani au wapi) wakati wa kutoa ushahidi (deposition)....

Ni yale yale yaliyomkuta Kwame Kilpatrick.....tena kama unakumbuka kwenye deposition ya yule dada mahakamani, alikuwa na attitude mbaya, akawa anazungusha macho na kukataa kata kata kuwa yeye na meya Kilpatrick walikuwa na affair....na baadaye text messages zao zikaja kuonyesha kinyume....Kwa hiyo ingawa mambo yao yalikuwa ni ya kifaragha, mbele ya mahakama walitakiwa kusema ukweli kwa mujibu wa sheria zao. Sijui sheria za bongo zinasemaje kuhusu Perjury lakini sidhani kama ziko tofauti sana
 
Hivi kashfa ya Monica Lewinky na Clinton si maisha ya mtu binafsi? kwanini uliendeshwa mchakato wa kutaka kumtoa Clinton kwenye ofisi ya urais? Wakina nani waliitoa hii habari?
Republicans. Walidhani wamemmaliza Clinton.
 
Republicans. Walidhani wamemmaliza Clinton.

Walifuata sheria tu na hawakuwa na makosa yoyote. Yeye Bubba alidanganya under oath. Unabisha hilo? Na kudanganya under oath ni Perjury ambayo ni felony? Unabisha?
 
Ndugu watanzania nafikiri imefika sasa kuelezana dhambi ya ukweli!!!
kuna hoja tumeziona nyingi watu wakilalamika kuchafuana ,mkuchika anafanaya kazi gani,na mengineyo!!!
samahani wana JF labda ntatofautiana kidogo na baadhi ya wenzangu,kilichofanyika na kinachofanyika hakuna tofauti na kinachofanyika humu ndani Jamii forums,ndugu wana jamii mbinguni ni nzuri sana kama tutakuwa wa wazi na wa kweli...

HOJA:
Mkuchika alichofanya ni kuendekeza mbea bila kutafuta ukweli uko wapi,wengi walikuja hapa kumlalamikia "AFANDE MASHA""Aalipotoa siku saba,sasa basi kila mtu anajua kilichomkuta masha ,swali langu ni moja tu tunaposema mkuchika kwa nini amechelewa kutoa seven days nahisi atutawatendea haki hasa waandishi wa habari,

MASWALI:

Taifa letu na SEMA KWELI walikuja na hoja za

1))MASHA ALIWASILIANA NA WAKUU WA SAGEM KULE GINIVA

2))KARAMAGI AENDEKEZA WAKE ZA WATU

Ok!!naomba kuuliza hiyo story ya karamagi humu ndani imesemwa lini??na ninani aliepiga kelele JF tufungiwe??humu ndani hakukuwa na kificho walimtaja mpaka mkuu wa wilaya !!!!alieibiwa mkewe!!!

SWALI:
JE si kweli karamagi anamtafuna mke wa MONGELLA.. je si kweli wametengana??je sikweli yule mwanamke walipelekwa kwenye masomo fasta akaja kupolekewa pale airport dar??je si kweli mongela alikuwepo hapo???
Ndugu Wadau,hakuna uongo hata mmoja ulifanyika kuhusu hoja za lile gazeti::
kweli huo upuuzi ulifanyika na watu wakaleta daata hapa na si hiyo hilo tu wanajua hapa dar kila uchau anaofanya karamagi.je kosa analosema mh mkuchika kusema siri za viongozi, Je kama kiongozi anashindwa kujiheshimu kwanini asianikwe hadharani!!ama leo hii anapitisha hoja ruksa kula wake za watu??je huyu ni binadamu na kionghozi anaetufaa kweli??je si yeye anaeitaji siku saba kutueleza wapi sherria ya nchi inaruhusu kula wake za watu

2)1))MASHA ALIWASILIANA NA WAKUU WA SAGEM KULE GINIVA

JE si kweli masha aliwasiliana na hawa wahuni ,,na si kweli masha alienda huko giniva,,nafikiri hapa kinachotakiwa kufanywa na mtu kama huyu ni kuchunguza je kweli hizi anazosema udaku ni za kweli!!!

USHAURI:
NI VYEMA TUSIWAKATISHE TAMAA HAWA WA MAGAZETI KAMA KUNA UKWELI TUWAPONGEZE NA KAMA KUNA UONGO TUSIACHE KUWASEMA

HAPPY VALENTINE
 
Mengi Vs Karamagi? Mengi Vs Masha? Mengi Vs Manji? Mengi Vs Masilingi? and the list goes on and on. Hapa naona wengi mmeanza kupata picha. Huyu jamaa ana matatizo gani? Kwanini yeye ndio mtu wa kulumbana na wenzake tu kila siku? Kwani yeye ndio mfanyabiashara pekee mwenye mafanikio hapa nchini? Mbona wako wengine wengi tu (hata kama hawamfikii Mengi) wenye mafanikio? Mbona hatusikii wakilumbana na wanasiasa? Au kwasababu hawamiliki vyombo vya habari? Na hii vita huwa anashinda nani? Mengi au wapinzani wake? Vita kati ya Mengi Vs Masilingi, nani alishinda?

Tafakari, jiulize.............

Zero nadhani bado uko zero katika hii topic. Ni vyema ukaanzia huku

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-ya-karamagi-co-dhidi-ya-jakaya-kikwete.html

Na ujue JF ilijua Old 17th November 2008, 01:58 AM kipindi ambacho hata hao kina Karamagu walikuwa hawajaanzisha hayo magazeti. Unapomtaja Karamagi, Masha, Manji umesahau kumtaja Lowassa, Chenge, Mahalu na wenzake ambao kwa kiasi kikubwa umma unawajua wako kundi gani. Kwa bahati mbaya sana baada ya kuanguka kwa Lowassa, waliamini moja kwa moja kwamba kuanguka huko kulitokana na magazeti na kwa kiwango kikubwa yanayochapishwa na kampuni za Mengi na yale ambayo Mengi anayaunga mkono pamoja na yale yasiyo na upande yakiwamo ya UHURU na Daily NEws. Wakaona dawa na wao kwa kuwa wana fedha wawekeze katika media. Rostam na EL wakatangulia kununua Habari Corp (RAI, Mtanzania na The African) na wao wakawekeza mamilioni. Kama ilivyofahamika na JF mapema, wakaanza kuwashughulikia watu wanaoamini kuwa wabaya wao, kina Samuel Sitta, MWakyembe, Anne Kilango, Ole Sendeka, na baadaye wakaanza kumsakama Mengi. Hii vita haikuanzia kwenye hizo picha za juzi zilizogeuzwa kuwa za harusi (ambayo si wizi), ilianza hata kabla. Baada ya Mengi kulalamika kwa njia isiyo rasmi, akalalamika hadharani mara nyingi, humu ndani JF na kwingineko watu wakambeza kwa kulia lia na Mkuchuka, MCT,Spika Sitta wakakaa kimya. Sasa Mengi akaona kumbe ni HALALI (kama ilivokuwa kwa umma kuua majambazi) akaanzisha Sema Usikike na kufufua Taifa Letu, kwa nguvu. makombora yake yakawagusa pabaya wahusika na Mengi akaangaza kwamba wao walianza kwa kutunga uongo na waandishi makini wakianza kuandika UKWELI wa uchafu wao wasilalamika. Hata kabla hawajlalamika, Mkuchika (Serikali) ikaingilia kati na sasa imetaja magazeti matatu, mawili ya mengi na moja la Karamagi, akiacha mengine kibao ya kundi la kina Karamagi likiwamo (Umma) lililosambazwa Bungeni na lile la Sati Huru, ambalo liliandika mambo ya matusi kabisa ya nguoni kumtukana Mengi. Mkuchika hakuyaona hayo, hakuliona Tazama, hakuliona Nyundo ambayo atataka yaendelee kufanya kazi ya kuwashambulia kina MWakyemba na kuwasafisha kina Kamaragi na Lowassa. JF AMKENI MUWAAMSHE WATANZANIA WETU.

MUNGU YUKO NA WAPENDA HAKI MILELE
 
Halisi, loud and clear, tatizo la nchi yetu mtu mmoja au watu wawili au kikundi tu kinaweza kuyumbisha nchi. Mahali walipofikia sasa hawa KALOKIRO ni balaa kwa taifa.
 
Back
Top Bottom