Magazeti yapewa siku saba kujieleza - Mkuchika

Magazeti yapewa siku saba kujieleza - Mkuchika

Ndugu watanzania nafikiri imefika sasa kuelezana dhambi ya ukweli!!!
kuna hoja tumeziona nyingi watu wakilalamika kuchafuana ,mkuchika anafanaya kazi gani,na mengineyo!!!
samahani wana JF labda ntatofautiana kidogo na baadhi ya wenzangu,kilichofanyika na kinachofanyika hakuna tofauti na kinachofanyika humu ndani Jamii forums,ndugu wana jamii mbinguni ni nzuri sana kama tutakuwa wa wazi na wa kweli...

HOJA:
Mkuchika alichofanya ni kuendekeza mbea bila kutafuta ukweli uko wapi,wengi walikuja hapa kumlalamikia "AFANDE MASHA""Aalipotoa siku saba,sasa basi kila mtu anajua kilichomkuta masha ,swali langu ni moja tu tunaposema mkuchika kwa nini amechelewa kutoa seven days nahisi atutawatendea haki hasa waandishi wa habari,

MASWALI:

Taifa letu na SEMA KWELI walikuja na hoja za

1))MASHA ALIWASILIANA NA WAKUU WA SAGEM KULE GINIVA

2))KARAMAGI AENDEKEZA WAKE ZA WATU

Ok!!naomba kuuliza hiyo story ya karamagi humu ndani imesemwa lini??na ninani aliepiga kelele JF tufungiwe??humu ndani hakukuwa na kificho walimtaja mpaka mkuu wa wilaya !!!!alieibiwa mkewe!!!

SWALI:
JE si kweli karamagi anamtafuna mke wa MONGELLA.. je si kweli wametengana??je sikweli yule mwanamke walipelekwa kwenye masomo fasta akaja kupolekewa pale airport dar??je si kweli mongela alikuwepo hapo???
Ndugu Wadau,hakuna uongo hata mmoja ulifanyika kuhusu hoja za lile gazeti::
kweli huo upuuzi ulifanyika na watu wakaleta daata hapa na si hiyo hilo tu wanajua hapa dar kila uchau anaofanya karamagi.je kosa analosema mh mkuchika kusema siri za viongozi, Je kama kiongozi anashindwa kujiheshimu kwanini asianikwe hadharani!!ama leo hii anapitisha hoja ruksa kula wake za watu??je huyu ni binadamu na kionghozi anaetufaa kweli??je si yeye anaeitaji siku saba kutueleza wapi sherria ya nchi inaruhusu kula wake za watu

2)1))MASHA ALIWASILIANA NA WAKUU WA SAGEM KULE GINIVA

JE si kweli masha aliwasiliana na hawa wahuni ,,na si kweli masha alienda huko giniva,,nafikiri hapa kinachotakiwa kufanywa na mtu kama huyu ni kuchunguza je kweli hizi anazosema udaku ni za kweli!!!


USHAURI:
NI VYEMA TUSIWAKATISHE TAMAA HAWA WA MAGAZETI KAMA KUNA UKWELI TUWAPONGEZE NA KAMA KUNA UONGO TUSIACHE KUWASEMA

HAPPY VALENTINE
 
Sijawahi kuona mtu anayefikiria kwa nguvu halafu akafikiria vitu vya ajabu kama wewe!!

Sasa cha ajabu nini, mkuu? Au nimekukwaza? Nyani achana naye na ndo ameshapata kisingizio cha pombe ... kwikwikwiii
 
Walifuata sheria tu na hawakuwa na makosa yoyote. Yeye Bubba alidanganya under oath. Unabisha hilo? Na kudanganya under oath ni Perjury ambayo ni felony? Unabisha?

Cha Clinton ni cha mtoto ukilinganisha na Karl Rove, Dick Cheney na Dubya, bahati yao kwamba walikuwa wababe na Nancy alikuwa wishy wash, Senate majority ingeongozwa na Rahm mbona wangekoma?!
 
Habari kama hizi inafaa zitangazwe. Kama Mengi ameoa,wananchi wana haki ya kufahamu,kwa sababu Mengi ndiye Baba wa Televisheni Tanzania,ni mtu muhimu kwa Watanzania.
Kama Karamagi anadandia wake za watu,kama Waziri Mkuu mstaafu amefanya hayo mambo yaliyotajwa watu wana haki ya kujua.
Ukisema 'Mheshimiwa Mkapa,Kikwete,etc,'',among other things una maana kwamba yeye ni mtu ambaye anafanya mambo ya heshima.
Halafu tukumbuke katika Awamu ya Pili,Mzee Mwinyi aliwakabili watu katika Serkali yake waliofanya vitendo vya ngono za jinsia moja.
Kwa hiyo Mkuchika anasema nini?
 
Its Media comeback bonanza for Mkuchika.
I bet
 
If someone or anyone thinks a certain medium has salandered them its their prerogative to sue for libel
 
Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika amevijia juu vyombo vya habari visivyotaka kuandika habari zake na kuviamuru kutohudhuria mikutano anayoitisha. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkuchika alisema kuna baadhi ya vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikifanya vituko na sasa hataki vifike kwenye mikutano yake.

“Nilipolifungia gazeti la Mwanahalisi, baadhi ya vyombo vya habari vilisema havitashughulika na mambo yangu kwa siku 90. Kwa muda wote ambao nilikuwa kimya, yamefanyika ambayo si ya kitaaluma na vituko vingi.

“ Siku nilipokwenda kukabidhi bendera Taifa Stars nilikuwa na Naibu wangu (Joel Bendera) na Waziri wa Muungano (Muhamed Seif Khatib), lakini baadhi ya vyombo viliandika kuwa Bendera ndiye aliyekabidhi bendera, na kuna vingine viliandika kuwa ni Khatib jambo ambalo lilikuwa ni uongo.

Mkuchika alisema, “ Siku 90 zimepita na Mwanahalisi liko katika circulation (usambazaji) lakini kuna wengine wanaandika Waziri XXX, mimi si waziri XXX, bali naitwa Kapteni mstaafu George Huruma Mkuchika. Sasa kama hamtaki kuandika habari zangu kwa nini mnakuja kwenye mikutano yangu?”

Alisema kitendo cha kutoandika habari zake hakimkomoi yeye, bali vyombo hivyo vimetaka kuwanyima wananchi habari za serikali. “Mimi ni msemaji wa serikali. Mmenichezea kiasi cha kutosha sasa basi. Na Watanzania wanajua mimi na Wizara yangu tunafanya nini.

“Kunifungia hakunifanyi nikose usingizi, ninalala fofofo kwa sababu nina vyombo vya kutosha vinafanya kazi ya kuwahabarisha wananchi,” alisema. Mkuchika aliwashangaa wale wanaoendeleza malumbano ya kutotaka kufanya kazi naye, huku wakijua kuwa wanataka mabadiliko ya sheria ya vyombo vya habari.

“Hawahawa ndiyo wanaotaka ibadilishwe sheria ya vyombo vya habari, na mimi ndiye ninawajibika kuipeleka bungeni, sasa watakaa na nani kujadili jambo hili?,” alihoji Mkuchika. Oktoba mwaka jana, serikali ilitangaza hatua ya kulifungia kwa miezi mitatu gazeti la wiki la Mwanahalisi kwa kuandika habari za uchochezi.

Akitangaza uamuzi huo, Mkuchika alikaririwa akisema Oktoba 8 mwaka jana, Mwanahalisi iliandika habari zilizosema kuna kundi la watu lina mpango wa ‘kumpindua’ Rais Jakaya Kikwete, ili asishinde uchaguzi mwaka 2010. Gazeti lilitaja watu waliodai kuwamo kwenye mpango huo kuwa ni aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa, Rostam Aziz, waliokuwa mawaziri wa zamani Andrew Chenge na Nazir Karamagi.

Pia lilimtaja Waziri wa Mambo ya Ndani Laurance Masha, Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Emmanuel Nchimbi, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima na mtoto wa Rais Ridhwan. Aidha, wakati Mkuchika akitoa kauli hiyo, Mwenyekiti wa Kampuni ya Jukwaa la Wahariri, Sakina Datoo, alituma ujumbe mfupi kwa baadhi ya wahariri akiwataka kuendelea kutoandika habari za waziri mpaka hapo jukwaa la wahariri litakapokutana wiki ijayo, kupitia upya uamuzi huo.

Source: Gazeti la Habari Leo
 
Tusipojua undani wa watu wetu vizuri ndio tunaishia kuchagua VIONGOZI wabovu, wala rushwa, mafisadi, ... Acha magazeti yaandike tuwafahamu kuanzia vitandani, vyumbani, sebuleni, mtaani,....Tumekuwa tukiangalia mazuri yao tuuuu mpaka basi.



Ukweli ni kuwa maisha binafsi ya kiongozi wa umma ni mali ya umma,sisi tunahitaji kujua kiongozi wetu anafanya nyini na mshahara mkubwa tuliompa jee anajirusha sana au vipi? ingawa siungi mkono kuandika yasiyo ya kweli. suala la kusema mambo binafsi ni upuuzi kama mambo hayo binafsi ni kufuja fedha za umma kwa ufuska wakuache tuu?
 
Back
Top Bottom