Ushuhuda wangu kwenye utapeli,nilitapeliwa 4,500 TZS
Nakumbuka after chuo ile kuapply kazi , kuna post niliiona nikavutiwa kuapply, few days later nikaona email nimekua shortlisted for an interview na itafanyikia posta,i was excited ila nilishangaa hiyo interview eti itakua na part ya Refreshment yaani ni coffee sijui so tunatakiwa kutuma just 4,500/= kabla ya siku hiyo mmh nilisita ila home wakasema we tuma mbona ni kiasi kidogo tu basi nikatuma na nikaanza kujiandaa na nondo za interview [emoji2957] siku ikafika mapema nipo Posta nikakuta watu kibao nikiwauliza wanasema ni hiyo interview na wameshatuma hizo 4,500/= kama waliambiwa , basi tukaendelea kusubiri tunaona mda wa interview umefika ila ofisi hata haijafunguliwa wapo walinzi tu mmh, tukawauliza leo kuna interview hapa mbona kama hatuelewi eh walinzi wanashangaa na wanasema hawana taarifa yoyote kama kungekua na interview leo. Basi kuwapigia simu sasa hawapokei. Ndiyo tukajua tumetapeliwa. Nilimind kupotezewa muda na ila huruma wengine walikua wametoka mbali Bukoba, Mwanza huko nauli+accomodation ,dah fresh gradutes tunapitia magumu, na walipata pesa nyingi tu maana ni kiasi kidogo sawa ila kwa watu wengii[emoji51]
Now nimekua over conscious hata mtu aniambie lete buku tu tukusaidie nini nampiga mkwara namreport TCRA ni tapeli [emoji3][emoji2]