Ilikuwa ivi asee,,,mtu mzma mwenye hekima zake zote kafika kwenye ofisi yangu ya huduma za kifedha akitaka kutoa pesa...ila kabla alikuja na story kadhaa ooh ndugu ofisi yako nzur ila ingependez uweke hiki na hiki ili iwe bora zaidi nikamsikiliza vizuri sna na nikamjib ushauri wako mzuri ntaufanyia kazi...sasa akasema nahitaj kutoa pesa kiasi cha laki 3 sijui makato saivi yakoje..nikamjib wanakata kiasi fulani akasikitika san ,,basi nikaona anapiga simu anaongea na mtu nitumie basi hiyo hela nitumie hiyo hela makato ni kiasi fulani ,,kakaa kam dk 1 akaniuliza ivi una namba ya voda anitumie kwa namba yako..nikamjib ndio basi niandikie na jina lako nimtumie,nikasema sio kesi acha atume tu si ntaitoa mwenyewe hapa hap ofisi bana..hakuna shida...dah basi mzee kamtumia namb yangu na jina,,,ghafla hela ikaingia nusu km laki 2 na elf8,,nikamwambia mbona katuma kidgo akapiga sim kuongea naye anamwambia ebana tuma hela yote mi nadaiwa rafiki ang,,kweli jamaa akatuma yote iliyobaki lak1 na elf2...nikamwambia mzee tayari katuma yote ipo hapa laki3 na elf10. ...basi mi nikaanza process za kuichomoa hela ,,wakt huo hela yake laki3 ipo mkononi nimeishika sijampa ...sasa wakti nafanyia process ya kuitoa nikaona aahh huyu mzee ngoja nimpe hela yake tu niitoe tu hapa taratibu..basi mzee kaondoka km dk 1 naingiza kiasi naona sms kiasi cha laki 1 kimerudishwa...dah nkastuka nikatoa haraka haraka palepale nkaingiza laki 2 iliyobaki kweny akaunti...coz natumia smartphone ilidisplay sms juu...ndio maana nikafanikiwa kuona hiyo sms ya kurudishwa kwa muamala huo...kweli nikafanikiwa kuokoa laki 2,,laki moja jamaa akafanikiwa kuirudisha...dah kwnza nikala pozi kwa dakika kadhaa nikimtafakari yule mzee ni mtu mzma sana akosi 55 naah yule...nikaanza kuuliza majirani zangu wakasema wanamuonaga sehem fulani anapenda kukaa tu...basi nikawaambia kanitapeli hapa uyo mzee km laki 1 wakasikitika tu basi, sasa kuhus wanamuonaga sehem fulani nikaenda kuuliza wakasema anakujaga hapa basi hatujui anapokaa...nikaenda voda kufatilia namba ile iyotuma pesa kwangu...nikagundua huyu mtu hakua mbali na hay maeneo, kozi aliweka pesa kwa wakal mwngine ndio akaja kwangu kuitoa kupitia namba yangu binafsi....
KOSA Kwangu:
Kukubali aondoke kabla hela sijaitoa yote..pili kuruhusu mm km wakal kutumia namb yang binafsi kutumiwa pesa ,tatu kumpatia pesa kabla sijamaliza kutoa pesa.
USHAURI:
Ww kama wakal sehem yoyote ulipo USIMUAMINI mtu yoyote yule akija ofisini kwako...mbinu matapeli wanatumia ni nyingi sana...na wengine wanatumia mbinu za zamani baada ya kukusoma uelekeo wako katik biashara hii...mwngne anaweza kuja kwako kupata huduma akiwa ana nia ya kutapeli lakin akagundua udhaifu ulipo akatumia kama fursa ya kuja tena siku ingne kukutapeli..
Pia mwisho namalizia kusema makosa binadam tunafanya mengi san ila ndio mwanzo wa kujifunza..
Ni hayo tu kwa herini.