Magenge ya utapeli Tanzania: Tupe stori kama umekumbana na kadhia zao

๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚Kuna watu humu ndani wapo London wanakufanyia mpango wa invitation letter ukijaa tu unao
 
Nilivomaliza chuo 2016 wakat narudi kuchukua cheti nikakutana na mwamba mmoja tulimaliza nae chuo kimoja ila course tofauti. Nilikua namfahamu kwa jina na vile alikua CCM maarufu sana pale chuoni


Akanipa mchongo kua pale makao makuu ya uvccm dodoma yuko kiongozi wao anaitwa mkuu wa majeshi. Huyu mkuu wa majeshi hua anapewa nafasi 15 za kuteua vijana wakajiunge na jeshi. Sasa mara hii alivopewa akamwambia jamaa amsaidie kutafuta vijana ili awapeleke

Jamaa akasema kwa kua tumeonana bac ni vzur aniunganishe na mimi nitafute wenzangu ili tuchangamkie fursa

Bac nilivoelewa somo nkaanza kutafuta wenzangu ambao watakua tyr. Masharti yalikua tupeleke vyeti vya kuzaliwa na sh. 200,000 kila mtu. Tukatoa izo pesa. Kuna jambo nilifanya wakati natafuta wenzangu, kila nliyempigia kumpa huo mchongo nilimueleza kabisa kua huyo jamaa cmjui vzuri, so huenda mchongo ukawa ni wakweli au utapeli. Kwa iyo mtu alitoa pesa nikiwa nshamtahadharisha na akatoa kwa ridhaa yake

Bac ikawa ndo hivo pesa zikaenda na mshkaji akazima simu na kupotea
 
Baada ya kurudi Zenji nikapata kaz ya kufundisha shule binafsi ndogo ndogo tu.

Kufika December nikapewa mchongo kua JKT wanakuja kufanya usaili zenj na kuchukua vijana waende kozi na ikiwezekana wakajiunge na jeshi siku za usoni

Nimaambiwa kuna jamaa ni mwanajeshi anapiga iyo michongo na kashapeleka vijana wengi tu na wote ni wanajeshi sasa ivi

Mara hii niliaminishwa kabisa na mtu ninaemuamini sana tu kua huyu jamaa ni uhakika kabisa

Bac mara hii nikadaiwa laki tatu ya kuanzia mchongo nikatuma kwa ezypesa. Baada ya siku kadhaa jamaa akanambia njoo na vyeti vyako sasa hivi maeneo ya mjini, nikamwambia siwahi saiv niko kazini na ata nikitoka nifike nyumbani kuchukua vyeti kuja huko kwa muda huu unaotaka siwezi kuwahi

Akasema hamna mbaya bac tuma elf 50 niweke mambo sawa, nikatuma. Baada ya siku mbili akanambia lete vile vyeti vyako. Nikamfuata town akanipakia kwenye gari yake mpaka wizarani, akaingia ndani na vile vyeti, baada ya muda akatoka akanambia kazi imeisha tusubir majibu


Baada ya wiki akanipigia simu asubuhi niende kambi ya JKU ndipo usaili unapofanyika, nibebe na 150,000 hiyo ni yake baada ya kufanikisha mchongo. Nikatoka fasta kufika nikakuta watu kibao wamepangwa makundi tofauti tofauti kutokana na wilaya walizotokea. Nikaangalia jina langu lipo kwenye kundi gani nikaelekezwa pakukaa

Kidume nshatupa laki 5 tyr apo. Bac usaili ukawa unafanyika pale watu wanakaguliwa vyeti wenye feki wanarudishwa makwao. Ila baada ya muda zinakuja gari za garama na watu wakubwa pamoja na wale waliondoshwa kwa vyeti feki, wanaongea na wale masoja pale then vijana wanapitishwa kuendelea na vipimo


Foleni ilikua kubwa na zoez lilichukua kama wiki iv kukamilika. Ndani ya hiyo wiki tulikua tunatakiwa tufike sa 12 asubuhi na kuondoka saa nne bila usaili kila cku.

Nilipitia mambo ya ajabu kwa kweli kama kurushwa vichura mara kadhaa, kudekishwa choo na kuruta wa kike wa JKU, kuimbishwa na use**e mwingine mwingi tu

The most painful part for me sio kutupa hela hapana, ni kile kilichonikuta katika vipimo

Baada ya kuhakikiwa vyeti nikaungana na wenzangu kusubir kuingia kwa dktari kwa ajili ya vipimo

Kuingia tu nikaambie nivue shati. Nikaanza kupimwa macho, kipimo ambacho nilifeli vbaya mno. Kila herufi nliokua naonyeshwa nlikua nataja nyingine dah. Nikaambiwa nivue na za chini kwa ajili ya kile kipimo kikubwa chao. Kinachomiuma mpaka leo ni kua, kama afande alijua siwezi kwenda kwa sababu macho yangu ni mabovu, kwa nini asingeniambia tu nivae niende kuliko kunambia nivue afu anipime vle vpjmo vingine??


Mwisho wa siku sikupata nafasi kisa sioni vzur nikaambiwa ntapiga risasi wenzangu mazoezini dah!!

Watu wakanambia na ww hujiongezi tu? Ushawahi kuona mwanajeshi mwarabu? Nikawajibu ndio. Wakaniuliza wapi. Nikawambia Taliban

Ila mpaka leo naamini jamaa hakunitapeli, alitimiza wajibu wake. Ni mimi ndo nilifeli kwenye vpimo
 
Huyo maza ukishika ni 0732 tuu
 
universty abroad mr tony ni mzurumati sana anawadanganya wazazi wanapokwenda kwake kupeleka watoto kusoma nje ya nchi hakuna mshenzi kama huyu jamaa ni tapeli lililobobea

Mwana wa wapi huyu?
 
Muulizeni Kamanda IGP Siro ile suti aliyovaa siku baada ya kuapishwa alipewa zawadi na nani?
 
mtu anataka mwenyewe kutapeliwa bwana....maana ata hao matapeli huwa wanaangalia na mtu mwenyewe wa kumtaperi...kuna wengine mnajirahisi sana kwa matapeli hadi mnawapa nafasi...pole sana rafiki yangu
Mara nyingi sana,wengi wanaotapeliwa tamaa zao ndiyo zinawaponza, maana Tapeli lazima wakutaminishe kitu flani hivi ili uingie tamaa,na ukisha ingia tamaa tu unakua Kama kipofu na unapigwa faster!!
 
Usisahau mtandao wa matapeli wa madini feki
 
Shukran mkuu yani Kama Mungu nasoma uzi huu Kuna boya kanipigia kadai mhudumu wa voda .nmemlipoti now namba yake+255672703002
Wapuuzi sana eti mhudumu wa voda anatumia tigo
 
Haaaaa. Usiombe utapeliwe maumivu yake sio
 
Polisi nilienda tatizo ukitoa hela ndio watafatilia sasa laki1 utashangaa umetumia laki3 na bado usipate hela yako..
Ni kweli wakati mwingine bora umtafute kimya kimya huyo tapeli wako au umuachie Mungu tu, ukienda polisi utaenda kupigwa zaidi na hiyo hela usiipate.
 
Mimi nilipigwa na mwanangu (mtoto wa kaka yangu) mmoja hivi wakati nasoma chuo mwaka 2015, kijana wangu (ananizidi 10 yrs).

basi kijana alikuwa na maisha magumu sana kipindi hicho, anafanya biashara haziendi, familia inakula mlo mmoja.

basi nikaamua kumpa ๐ฆ๐ค๐จ๐ฉ๐จ ๐ค๐ฎ๐ญ๐จ๐ค๐š ๐ค๐ฐ๐ž๐ง๐ฒ๐ž ๐ฉ๐ž๐ฌ๐š ๐ฒ๐š๐ง๐ ๐ฎ ๐ฒ๐š ๐›๐จ๐จ๐ฆ, kiasi cha Tshs laki 2 kwa ahadi ya kurudishiwa baada ya miezi mitatu.

kijana akaenda morogoro huko kununua mchele anakuja kuuza Dar (mbande) kibandani kwake!

kijana akaendelea na biashara na ikaanza kukua kwa kasi sana, miezi ikasonga na pesa haikurudishwa, kila nikimkumbusha ananipiga chenga. Kijana kakaa na pesa miaka 6, kaongeza wanawake watatu, kumbuka hapo kijana si yule wa kulala njaa tena๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…

basi ilifikia hatua tumegombana mpaka kukatiana mawasiliano.

Imekuja kutokea msiba wa baba yangu mdogo mwezi wa pili 2021, ndio nikaonana nae uso kwa uso, tukasalimiana kiaina tu as if nothing happened. Mipango ya kusafirisha mwili ikafanyika kutoka Dar kwenda serengeti kuzika, na yeye kasafiri. Na mimi nikajiunga tukampumzishe mzee wetu

huko sasa ndio nikaamua liwalo na liwe, nikaenda kwa mama yake nikamueleza naona hana msaada, nikamfuata kaka yake mkubwa ambaye ana mauwezo makubwa tu nikamueleza A to Z, yeye ndo akasema nimuache mdogo wake, akalipa pesa chaaap kwa Mpesa.

Hio hela haikukaa hata dakika moja kwenye simu, nilienda kuitoa fasta sana maana binadamu wa sasa si wale tena tuliowajua.

Baada ya malipo hatukuwasiliana tena na hawa watu, kaka mtu ana uwezo mkubwa, ni mwajiriwa wa serikali mwenye mshahara mzito, ana kampuni yake kubwa tu inayo deal na masuala niliyosomea kabisa lakini aligoma kunipa nafasi na mimi sina haja hata ya kuomba wala kukumbusha.

nafasi kampa mdogo wake, kamtafuta na binti.mwingine wa ukoo wetu.kampa job.

mi nimepoa tu Sina neno na mtu napambana mtaani since 2015 sina mchongo wa kueleweka.

Maisha ndivyo yananipeleka race sana, nasaidia watu hata kidogo nilichonacho lakini kwangu milango haifunguki. Kuna wakati mpaka watu waniambia nimerogwa, nachukulia easy tu napambana.

usiamini mtu linapokuja suala la pesa, give what you can afford to lose.

Regards,

Simba.
 
Mara nyingi sana,wengi wanaotapeliwa tamaa zao ndiyo zinawaponza, maana Tapeli lazima wakutaminishe kitu flani hivi ili uingie tamaa,na ukisha ingia tamaa tu unakua Kama kipofu na unapigwa faster!!
Long story short.
 
Da pambana Mr
 
mtu anataka mwenyewe kutapeliwa bwana....maana ata hao matapeli huwa wanaangalia na mtu mwenyewe wa kumtaperi...kuna wengine mnajirahisi sana kwa matapeli hadi mnawapa nafasi...pole sana rafiki yangu
Subiri yule tapeli akupige laki 6 eti anakutafutia kazi Dubai.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ