DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Jeshi la Magereza Tanzania linapenda kuujulisha umma kuwa, katika kutekeleza majukumu yake ya kuwapokea, kuwahifadhi na kuwarekebisha wafungwa na mahabusu, limeendelea kuzingatia usalama wao katika kipindi chote wanapokuwa chini ya ulinzi wa jeshi hilo.
Kwa msingi huo, Jeshi la Magereza limeweka utaratibu madhubuti wa kusimamia utoaji wa huduma mbalimbali, ikiwemo chakula kwa wafungwa na mahabusu kwa mujibu wa kanuni za kiusalama. Udhibiti, usimamizi na uangalizi wa huduma ya chakula ni utaratibu wa kisheria unaolenga kulinda afya na usalama wa wafungwa na mahabusu, pamoja na kuzuia mazingira yoyote hatarishi.
Kila mfungwa au mahabusu anahudumiwa kulingana na matakwa ya sheria bila upendeleo wowote.
Jeshi la Magereza litaendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi, kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika kusimamia haki na wajibu wa wafungwa na mahabusu.
Pia Soma: Mama wa CHADEMA azimia mahakamani baada ya Lissu kudai kunyimwa chakula