Magereza: Hakuna upendeleo katika huduma ya chakula kwa wafungwa na mahabusu

Magereza: Hakuna upendeleo katika huduma ya chakula kwa wafungwa na mahabusu

Kumjibu aliyekua analilia chakula mahakamani unapokua Gerezani unaruhusiwa kula ulichotoka nacho Jela tuu na hauruhusiwi kurudi nacho Jela
Nani amelilia chakula? alisema hajala, ni haki yake... na mtu akigoma kula chakula utamuitaje? au hukuwahi kusikia magerezani watu wanagoma kula? Heche aligoma kula naye utasemaje?
 
Jeshi la Magereza Tanzania linapenda kuujulisha umma kuwa, katika kutekeleza majukumu yake ya kuwapokea, kuwahifadhi na kuwarekebisha wafungwa na mahabusu, limeendelea kuzingatia usalama wao katika kipindi chote wanapokuwa chini ya ulinzi wa jeshi hilo.

Kwa msingi huo, Jeshi la Magereza limeweka utaratibu madhubuti wa kusimamia utoaji wa huduma mbalimbali, ikiwemo chakula kwa wafungwa na mahabusu kwa mujibu wa kanuni za kiusalama. Udhibiti, usimamizi na uangalizi wa huduma ya chakula ni utaratibu wa kisheria unaolenga kulinda afya na usalama wa wafungwa na mahabusu, pamoja na kuzuia mazingira yoyote hatarishi.

Kila mfungwa au mahabusu anahudumiwa kulingana na matakwa ya sheria bila upendeleo wowote.

Jeshi la Magereza litaendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi, kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika kusimamia haki na wajibu wa wafungwa na mahabusu.

Pia Soma: Mama wa CHADEMA azimia mahakamani baada ya Lissu kudai kunyimwa chakula
Kwahiyo hapa nawaza kusema pengine ilikuwa katika kuzingatia usalama wake,je vihatarishi ni nini na vya kiwango gani?
 
Nipo sana tu CDM lkn lugha zinazoendelea chamani zinafanya wengine kuona aibu kujulikana kuwa ni CHADEMA
 
Nipo sana tu CDM lkn lugha zinazoendelea chamani zinafanya wengine kuona aibu kujulikana kuwa ni CHADEMA
Kama unapinga mauaji, utekaji na ufisadi bas hapo una qualifications za kuwa chadema
 
Yaani huo ndio ufafanuzi? Sasa kafafanua nini juu ya madai ya mahabusu kunyima chakula? Ila baadhi ya watu serikali ni wapuuzi
 
Hakuna asiyepinga Mauaji. Ht huko CCM wanapinga mauaji
Taja mmoja aliyekuja public akapinga? Kwa nini wapinge wanachama na sio chama? Hicho chama kilikuwa wapi kuunga mkono kauli za Gwajima kupinga mauaji?
 
Hizi ndo lugha za CHADEMA
Unadhani kila negative comment inatoka kwa mfuasi wa chadema, huwazi kwamba kuna mtu anaangalia mambo kwa namna tofauti kidogo?

Kiazi kingine hiki.
 
Unadhani kila negative comment inatoka kwa mfuasi wa chadema, huwazi kwamba kuna mtu anaangalia mambo kwa namna tofauti kidogo?

Kiazi kingine hiki.
Ni ngumu sana kuitenganisha CHADEMA ya sasa na lugha za kashfa/matusi.
Zamani hatukuwa hivyo. Naona kabisa chama kimevamiwq
 
Ni ngumu sana kuitenganisha CHADEMA ya sasa na lugha za kashfa/matusi.
Zamani hatukuwa hivyo. Naona kabisa chama kimevamiwq
CCM ya sasa sio tu ina lugha mbaya, imeamua KUUA watanzania. Now tell me nani ana afadhali.
 
Ujinga tu...
Haya majitu hovyo sana...

Sasa hio taarifa wametoa ili iweje? na ina lengo gani?


Ilipaswa waanze kuomba radhi kwa umma na wafungwa/mahabusu wote ambao huwa wanawanyima chakula... na ni tabia iliyokubuhu kumnyima Lissu chakula..

Wametoa taarifa kama wanapinga madai ya kumnyima Lissu chakula si kweli.. hali ya kuwa jamaa alisema pale hajala na ana njaa...
lengo ni kumjilisha yule mtuhumiwa wa uhaini aliekua analili chipsi mayayi wakati ugali maharage upo kwa mujibu wa sheria ya magereza kwa mahabusu.

mtu anapenda kula halafu analeta ukorofi wa kukiuka sheria, ataisoma sasa :NoGodNo:
 
Back
Top Bottom