BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Wakuu, salaam, kuna mambo nimewaza hapa kuhusu Idara zetu za Magereza. Binafsi sikutarajia kuona au kusikia Wanaotoka Gerezani wakihusika na matukio ya uhalifu mitaani kwa sababu naamini moja ya kazi ya Magereza ni kurekebisha tabia za wahalifu na kuwafanya kuwa watu wema baada ya kutoka kifungoni.
Sasa kama Idara ya Magereza inatekeleza suala la urekebishaji Tabia, kwa nini bado wanaotoka kwa msamaha au kumaliza vifungo wanaendelea na uhalifu mitaani hata baada ya kukaa muda mrefu kifungoni?. Tafsiri ya haraka ni kuwa Magereza yetu yamejikita kwenye kuadhibu zaidi kuliko kubadili wafungwa kuwa watu wema.
Na hili linadhihirika wazi hawafanyi jambo hilo kupitia kauli ya Rais Samia aliyoitoa kwa Jeshi la Magereza August 29, 2022 Rais Samia: Magereza mrekebishe tabia za wahalifu
Nadhani Idara ya Magereza na Serikali ziweke msisitizo katika kuwarekebisha Wafungwa zaidi kuliko kuwapa adhabu pekee kwa sababu adhabu hazibadili tabia zaidi ya kuumiza na ndio sababu wengi wakitoka wanarudia uhalifu.