Mantiki ya kumfunga mtu gerezani ni kumwondolea ule uhuru wake wa kuwa uraiani, na hiyo ndo adhabu anayopewa kutumikia. Sasa unakuwa na wajibu wa kumhudumia kwa kila kitu kama binadamu mwingine anayeishi uraiani, malazi, mavazi, chakula, matibabu kwa ubora unaostahili. Kinyume na hapo unakuwa umemwongezea adhabu nyingine zaidi ya kumpa mateso na manyanyaso ya kimwili na kisaikolojia na hivyo kumvunjia haki zake kama binadamu.