SoC02 Mageuzi ya Sayansi na Teknolojia ni fursa kwa vijana

SoC02 Mageuzi ya Sayansi na Teknolojia ni fursa kwa vijana

Stories of Change - 2022 Competition

Dr NGWAKWA

New Member
Joined
Jul 27, 2022
Posts
2
Reaction score
3
MAGEUZI YA SAYANSI NA TENKNOLOJIA NI FURSA KWA VIJANA

Kijana anawezaje kunufaika na maendeleo ya Sayansi na Teknolojia?

Mwandishi wa maarufu wa vitabu huko Marekani, Alvin Toffler katika kitabu chake Cha POWER SHIFT, Aliandika Alieleza Aina tatu za Nguvu, Nguvu za Mwili (physical power), Nguvu ya pesa (wealth power) na Nguvu ya Taarifa (Information power).

Katika kitabu chake Alieleza namna Nguvu hizi zimekuwa zikiendesha ulimwengu katika zama zote, huku kwa Sasa zikiongozwa na Nguvu ya Taarifa. Katika karne za mwanzo Mtu aliyokuwa na uwezo wa kutawala dunia ni yule ambaye alikuwa Nguvu za Mwili, mbabe, Mwenye uwezo wa kupambana kwa kutumia Misuli, Kadri Muda ulivyozidi kwenda taratibu Dunia ikaanza kuhamia katika Nguvu ya utajiri, kwani pesa Ina uwezo wa kununua Hata hiyo Nguvu ya mwili.

Mwenye pesa anaweza kulipa watu wenye Nguvu kwa kutumia pesa zake na kufanikisha Jambo lake. Katika karne ya Ishirini na moja (21) Mwenye Taarifa ndiye Mwenye Nguvu. Mtu Fulani anaweza kuwa na Taarifa Fulani Ambayo Hata mkuu wa nchi Ni lazima amnyenyekee Kutokana na umuhimu wake. Kwa zama hizi Nguvu ya Taarifa ndiyo inayowaendesha wote, Mwenye pesa na Mwenye mamlaka.

Taarifa ninayoongelea hapa Ni maarifa juu ya Sayansi na Teknolojia. Mafanyabiashara na mtawala Mwenye maarifa Zaidi juu ya matumizi ya Sayansi na Teknolojia ndiye ambaye anafanikiwa Zaidi katika zama hizi.

Vijana Kama Taifa la leo hawatakiwi kukosa maarifa juu ya matumizi ya Nguvu hii inayoendesha ulimwengu wa Sasa. Vijana hawatakiwi ubaki nyuma katika matumizi ya Sayansi na Teknolojia ili waweze kujikwamua kiuchumi, kisiasa, na kijamii.

Sababu kwanini vijana wanatakiwa kuwekeza Zaidi katika Sayansi na Teknolojia:-

SAYANSI NA TEKNOLOJIA INARAHISISHA BIASHA.
Vijana wanatakiwa kuchangamkia mageuzi ya Sayansi na Teknolojia kwani hurahisisha ufanyaji biashara kwa namna ifuatayo:-

Uwezo wa kufikia watu wengi kwa wakati mmoja.
Kwa kutumia Sayansi na Teknolojia kijana anaweza kuwafikia watu wengi kwa wakati mmoja kutoka sehemu mbalimbali, Jambo ambalo Lina manufaa makubwa katika nyanja ya kisiasa, kijamii na kichumi.

Kwa mfano kama ni mfanya biashara Unaweza kutumia nafasi hiyo kutangaza biashara yake na ikafikia watu wengi kwa wakati mmoja.

Uwezo wa kupima Aina ya wateja na kupima idadi ya wateja unayotaka kuijulisha kuhusu biashara yako.
Kupitia mtandoa wa internet Kuna teknologia zinazomwezesha mfanyabiashara kulenga soko lake kwa gharama ndogo, na kupima idadi ya watu unaotaka kuwafikia. Kwa mfano mfanyabiashara naweza kutumia matangazo ya kulipia kwa mtandao wa Facebook au Instagram na akalenga wanawake wenye umri wa miaka Kati ya 20-44 na tangazo lake likaoneshwa kwa wateja hao aliowalenga pasipo kuwafikia watu wengine ambao sio wateja wako.

Urahisi katika kuagiza bidhaa na kumfikia mteja.
Kutokana na ukuaji wa sayansi na teknolojia kijana anaweza kuagiza bidhaa, kutoka China, Dubai au Marekani bila Hata kusafiri na ikamfikia kwa wakati pasipo shida yoyote. Hii Ni fursa Ambayo kijana anaweza kuitumia ili kuinuka kiuchumi.

Mifumo mizuri ya Utunzaji Kumbukumbu.
Teknolojia imebuni mifumo mizuri ya Utunzaji Kumbukumbu za biashara, Ambayo inamuwezesha mfanyabiashara kupima ukuaji wa biashara yake kirahisi bila kuwa na madaftari mengi ya Kumbukumbu Ambayo yangemchukulia Muda mwingi katika kuweka pamoja Kumbukumbu ili kupima Mwenendo wa biashara yake.

Niseme tu kwamba Kama kijana unafanya biashara na bado haujaanza kutumia mifumo ya kisasa jiandae kufilisika miaka michache ijayo. Umewahi kujiuliza biashara zilizokuwepo mtaani kwako miaka mitano iliyopita, ni ngapi bado zipo mpaka Sasa?


2. Ni chanzo Cha ajira.
Mageuzi ya Sayansi na Teknolojia yameleta fursa Nyingi Sana za ajira kwa vijana. Taarifa sahihi juu ya mtumizi ya mtandao wa internet imekuwa Ni njia Ambayo imeajiri vijana wengi. Kupitia mtandao wa internet Unaweza kujiajiri Kama mwandishi mtandaoni, Shule za mitandaoni, Channel za you tube ambazo Ni fursa zinazolipa Sana Kama kijana ataamua kujidhatiti katika kutafuta ujuzi just ya fursa hizi.

Ni Chanzo Cha biashara za mtandao.
Vijana wengi bado Wana mawazo hasi juu ya biashara za mtandao (Network marketing) pasipo kujua kwamba hiki Ni Chanzo kikubwa Cha ajira. Vijana wengi wa kitanzania hawapo tayari kujifunza kuhusu biashara za mtandao Kama vile ubadilishe I was fedha za kigoni (Forex), na uuzaji na ununuzi wa sarafu za mtandaoni Kama vile BITCON, na kadharika.

Zipo kampuni yingi Sasa duniani zinazotoa fursa za ajira kwa vijana, kampuni zinazouza nguo na vifaa vya kielektroniki Kama Alibaba zinatoa fursa kwa vijana kujiajiri, Kampuni za utafiti na usambazaji wa Tiba lishe Kama vile BF SUMA, FOREVER LIVING na kadahrika zimewezesha vijana wengi kujikwamua kiuchumi kwa kuwa mawakala wa bidhaa zao mtandaoni.

3. Ni sehemu ya kukutana watu
Kuwa na mtandao mkubwa wa watu wa Aina tofauti tofauti kukuzunguka Ni chanzo Cha utajiri. Hii inamuwezesha kijana amtafute nani, wakati gani anapokuwa na shida gani. Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Uhusianao wa kibiashara kusini mwa Afrika, Gugu Mjadu, Alisema " In The world The most powerful tool is Networking" kwa Tafasiri isiyo rasmi anamaanisha "Kifaaa chenye Nguvu Zaidi duniani Ni kuwa na mtandao". Kadri unavyozidi kuwa na mtandao mkubwa ndivyo unavyoongeza uwezekano wa kufanikiwa.

Ni sehemu ya kujipatia maarifa.
Sayansi na Teknolojia inamwezesha kijana kujipatia maarifa anayoyahitaji kwa Haraka. Kijana inaweza kutumia fursa hii kujiongezea maarifa yatakayomwezesha kujikwamua kiuchumi. Kupitia kozi mbalimbali inazotolewa na Taasisi mbalimbali kwa njia ya mtandao kijana naweza kuitumia kujiongezea kiwango Cha Elimu itakayomwezesha kujikwamua kiuchumi. Kuna Aina ya Elimu Ambayo haitolewi shuleni, Lakini kwa kutumia mitandao mbayo Ni matunda ya Sayansi na Teknolojia Unaweza kuipata.

Ni njia Mojawapo ya kurahisisha kazi.

Kwa kutumia vifaa na vitendea kazi vilivyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia kazi inaweza kurahisisha.

Uvumbuzi wa Sayansi na Teknolojia umeweza kurahisisha usafirishaji wa vifaa Tiba kwa kutumia ndege zisizokuwa na rubani ili kurahisiha kazi na kuokoa Muda.

Huu ni wakati Kama vijana wa kutanzania kufanya utafiti na kutumia teknolojia, zinazogunduliwa Kila siku ili kuweza kunuaika.

Sayansi na teknolojia Ni mwarobaini kwa Matatizo ya Kiuchumi, na Ajira. Ikiwa tutabaki nyuma katika matumizi ya Sayansi na Teknolojia tutabaki kulalamika tu, Mara maisha magumu, mara serikali haijali nakadhalika.

Katika maisha natakiwa kwenda sawa na dunia inavyoenda au Unatakiwa kufika kule dunia inakoenda kabla haijafika ili ufanikiwe.

Wito wangu kwa vijana tuamke, tuzisake noti kwa kutumia sayansi na teknolojia. Najua mtu aliyepo usingizini huwa hapendi kabisa kuamshwa, Ila Mimi nimejitoa mhanga kukuamsha Hata Kama utanichukia.
 
Upvote 5
Hizi ndiyo mada ambazo huwa wengi hawazielewi, juzi kuna mada jamaa wameamua kutumia matatizo kuwa fulsa now wapo mbali sana, kijana anasoma anakuja kuandika sijaelewa, yaani unataka uwekewe open code everything mh!.

Tuendako tech inakuwa na nguvu kuliko manguvu ya mwilini, haishangazi now siwezi kwenda china kukusanya mzigo coz tayari godown kadhaa zipo mitandaoni so wanakusanya na kumpa super collector ambaye anasafirisha.

So hata sasa bado kuna tech ambayo haijagundukiwa so ni fulsa kwa vijana wa tech kufungua code, maisha yanasonga!.
 
Back
Top Bottom