Maggid Mjengwa: Wazee wa Dar es Salaam ni akina nani na wana sifa zipi?

Maggid Mjengwa: Wazee wa Dar es Salaam ni akina nani na wana sifa zipi?

Kwa lugha nyepesi isiyo na kificho, kulingana na muandishi, wazee wa dar lazime wawe ni wawe ni wanaume wa kiislamu, wacheza bao na wasio na elimu ya kutosha
ni kweli lakini hivi kwa yanayoendelea huoni upuuzi unaofanywa na hao unaowamini kuwa ni wasomi?
 
Kama Wazee wa Dar huwa wanapata heshima ya kupiga story na Rais. Nawashauri wanawake waache kuwasema vibaya wanaume wa Dar maana wanapokuja kuzeeka huwa na heshima kubwa kwa viongozi wa nchi.
 
Sasa ulitaka na wale wa chadema wenye kushangilia ushoga nao wawemo?

Hiyo haikubaliki

Hata wakialikwa wao watawaza kumuangusha raisi na hayo ndio mawazo yao.
Hivi ni chama gani chenye katibu wa itikadi na uenezi mwenye tuhuma ya kuolewa mombasa?
 
Raisi wetu mpendwa mama Samia Suluhu Hassan leo anaongea na wazee wa DSM

Niwakumbushe tu wazee wa DSM huu utaratibu ulikuwepo toka mwaka 1957 wakati TANU inazaliwa na kutafuta uhuru.

Wazee hawa kila mara walimuita kijana wao Nyerere kumpa miongozi namna ya kupambana na mkoloni na wengine walikuwa na ukwasi wa hela walikuwa hata wanampa msaada wa kipesa.

Kwenye picha hapo chini hao ni wazee wa DSM mwaka 1957 ninao wakumbuka hapo ni Mshumi Kiyate huyu mzee alikuwa ni mvuvi ndio alikiwa anasaidai familia ya Nyerere wakati alivyoacha kazi vile hakuwa na mshahara.

Siku moja alikutana na Nyerere pale fire akampa shillingi 200 wakati huo Nyerere anaishi Magomeni ili akailishe familia yake. Kumbuka shilling 200 ya wakati ule ulikuwa unaweza kujenga nyumba ya miti ya vyumba vitano.

Mwingine ni Jumbe Tambaza,Dossa Azizi,Suleiman Takadiri,Chaurembo,na wenginewe.

Utaratibu huu umekuwa ukiendelea hadi sasa maraisi wengi wanautumia utaratibu huu swali kwanini wazee wa Dar tu mkoani je.Jibu ni kuwa vuguvugu la kugombea uhuru lilianzia Dar ni vigumu kila mkoa raisi kwenda kuongea na wazee hawa wazee wa dar wanawakilisha wazee wa mikoani.

Ila ninachojiuliza kuwa mzee wa dar kuna kitambulisho au vipi maana sio kila mzee atakwenda huko.

Mama naona amefanya vizuri maana hao wazee hata yeye kwa umri wake ni baba zake

Namtakia hongera na maongezi mema

wazee wa TANU1957.PNG
 
Existence of "Wazee wa mkoa" is it a something progressive? I mean do we have to expect "Wazee wa mkoa " after 50years. If its a progressive, Ni kwa namna gani somebody can became one of them?
 
Leo Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mh. Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia kuongea na wazee wa Mkoa wa Dar es salaam. Tayari Rais ameshawasili Dar na bila shaka maandalizi yanaendelea. Ni kawaida kwa viongozi kufanya mazungumzo na makundi ya watu ama taasisi, utaratibu huu umekuwa desturi ya muda mrefu, japokuwa ni maarufu sana kwa viongozi kufanya vikao ama mazungumzo na wazee wa Dar es salaam.

Sio jambo geni kusikia kiongozi fulani, Rais ama Mkuu wa mkoa siku fulani atafanya mazungumzo na wazee wa mkoa wa Dar es salaam. Kabla ya leo siku zote niliamini utaratibu huu ni wa kawaida kwa kiongozi kufanya hivyo pale anapotaka kupata busara za wazee wa eneo lake analohudumu ama eneo ambalo makao yake yalipo, yaani mfano kwa Marais walikuwa wakiongea na wazee wa Dar kwakuwa IKULU ipo ndani ya Mkoa wa Dar. Sasa awamu hii jambo lipo tofauti kidogo japo si sana, sasa kwa tofauti hiyo ndogo imenifanya nitake kudadisi zaidi kuhusu hawa wazee wa Dar.

Naam! Hoja iko hivi, Rais aliyepita (JPM)alifanikiwa kuhamishia makazi ya serikali Dodoma. Na sasa Rais Samia anahudumu Nchi akiwa Dodoma ispokuwa pale tu anapokuja Dar. Sasa dhana ya kuongea na wazee niliamini huenda ingekuwa na mantiki kubwa zaidi kama ingekuwa Dodoma ambako ndiko yaliko makao rasmi ya Rais kuliko sehemu nyingine yoyote kwa sasa.

Au labda kuna nini cha mno kuhusu hawa wa kuitwa wazee wa Dar es salaam kiasi cha kumlazimu Rais kusafiri kuja Dar kuongea nao? Mbona kila mara wazee wa Dar.... Wazee wa Dar???
 
Ni rahisi kuwakusanya pamoja katika wingi wao. Ujumbe unawahusu wazee wa TZ, wao ni ishara tu.
 
Wazee wa Dar ni tunu kwani maarifa mengi na wameona mengi na pia wana weledi.
 
wa mkoani wapo busy na kilimo
wa mjini wanasubiri kodi hivyo wana muda mwingi
 
Wakati Mh.Rais anasema Atakutana na Wazee wa Mkoa wa Dar es salaam kwa Niaba ya Wazee wa Nchi nzima Binafsi niliamini Suala la ITIKADI za KISIASA halitakuwepo.Nimeshangaa na Kuona Mkutano wa Jana ni kama Uliandaliwa KICCM zaidi kuliko KISERIKALI.

Niliamini tunaposema Wazee Wangetafutwa Wazee kutoka Vyama vyote na kama Ingefaa kutoka Mikoa yote ili kuwawakilisha Wazee wenzao.

Kama Jana kulikuwa na Wazee 1000 na Tanzania ina Mikoa 30 basi Kila Mkoa ungetuma Wazee 35 na bila kuchagua Wazee wa Chama kimoja. Pia kama ule Mkutano ulikuwa wa Mh.Rais na Sio Mwenyekiti wa CCM basi Utitiri wa Viongozi wa CCM haukupaswa kuwepo.Mh Rais hebu tutoe kwenye siasa sana ili tuwe Wamoja Vinginevyo Ungeitwa Mkutano wa Mwenyekiti wa CCM na Wazee wa Ccm Mkoa wa DSM.
 
Wazee Wa Dar Es Salaam Ni Akina Nani? Je, Sifa Za Mzee wa Dar es Salaam Ni Zipi?

Ndugu zangu,

Leo Rais wa Jamhuri, Samia Suluhu Hassan ataongea na Wazee wa Dar es Salaam.

Kwenye juzuu ya kwanza kati ya tatu, kitabu ' The Making Of A Philosopher Ruler, ukurasa 124-125., mwandishi Mtanzania, Prof. Saida Yahya- Othman anawazungumzia Wazee wa Dar es Salaam.

Kati ya anaowataja, amemtaja Marehemu Mangara Tabu Mangara. Mwandishi anaelezea jinsi Julius Nyerere alivyowatumia Wazee wa Dar es Salaam kupata taarifa za hali halisi za watu wa kawaida mitaani.

Tabu Mangara alikuwa mmoja wa ‘ Watoto wa Mjini.’ Alipata pia kuwa bosi wa mama yangu mzazi wakati Mangara akiwa Mkuu wa Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali- Government Press.

Tabu Mangara Tabu Mangara alikuwa pia Mwenyekiti wa Yanga. Aliishi Kariakoo na alikuwa na nyumba pia pale Mtaa Mwanz Ilala ,jirani na Mtaa wetu tulioishi utotoni mwangi, Iringa Street.

Mwandishi Saida Yahya- Othman anakielezea kisa cha ndani ya Baraza la Mawaziri miaka ya 80.

Kulikuwa na uhaba wa bidhaa madukani na kukawa na bei za kulangua. Aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Joseph Mungai akapendekeza Serikali iyafunge maduka binafsi na kuwepo na maduka ya Serikali.

Mawaziri waliunga mkono hoja ya Mungai, lakini, Nyerere akawaambia wasubiri kwanza kabla hajapitisha maamuzi.

Nje kwenye korido za Ikulu, Julius Nyerere akamwambia Balozi Sued aende akamtafute Mangara Tabu Mangara, na amwambie Nyerere anamuhitaji Msasani kwa mazungumzo.

Pale Msasani Nyerere akamwelezea Mangara jambo zima na kumwomba ushauri.

Mangara akamweleza Nyerere hali halisi ya wananchi mitaani, kwamba watu wanaishi kwa madeni. Bajeti zao ni za siku kwa siku. Leo mtu akiwa hana kitu mfukoni, anakwenda dukani kwa Mshihiri kukopa. Mwingine anaweka rehani hereni za mkewe ili apate bidhaa za dukani.

Sasa, Mangara akamwuliza Nyerere;

“Maduka ya Serikali nayo yatafanya hivyo hivyo?”

Nyerere akamwelewa Mangara. Maamuzi yale ya kufunga maduka hayakufanyika.

Nini adili ya jambo hili?

Mwalimu alifahamu udhaifu wa baadhi ya Mawaziri wake wasomi , kwamba baadhi yao kwa vile wanaishi Oysterbay, walipoteza mawasiliano na watu wa kawaida na hali zao za maisha. Mangara ambaye hakuwa hata na digrii ya Chuo Kikuu, aliwazidi hekima baadhi ya Mawaziri wa Nyerere.

Mwalimu pia alijua, kuwa watu wa aina ya Mangara Tabu Mangara, hawakuwa wasaka tonge. Ni watu ambao kwenye kushauri kwao, hawakutarajia Nyerere awape vyeo. Walitoa ushauri kwa mapenzi ya nchi yao na kwa kumtakia mema Nyerere. Ndio hawa walioitwa ‘ Wazee wa Dar es Salaam.’

Wazee wa Dar es Salaam ni kina nani haswa?
Tangu enzi za Mwalimu’, kukiwa na jambo kubwa kitaifa, basi, Mwalimu aliliongea kupitia kwa “ Wazee Wa Dar Es Salaam”. Na mahali haswa wanapokutana ‘Wazee wa Jiji’ kumsikiliza ‘ Mkuu Wa Kaya’ ilikuwa ni pale Upanga kwenye Ukumbi wa Diamond.

Jambo hilo lililoasisiwa na Mwalimu likaja kuwa ni utamaduni wa kisiasa. Mathalan, ni pale Upanga Diamond Jubilee ndipo Mwalimu alipotangaza vita dhidi ya Idi Amin kupitia Wazee Wa Dar Es Salaam.

Nini chimbuko la Wazee wa Dar es Salaam?
Chimbuko lake ni Wazee wale 120 waliounda Baraza la Wazee wa TANU kwenye harakati za kupigania Uhuru. Waliongozwa na Mzee Suleiman Takadir.

Baada ya Uhuru Nyererw akaja kugombana na Wazee wa Baraza hili. Akalifutilia mbali Baraza mwaka 1963. Nyerere akaendelea kuongea na Wazee wa Dar es Salaam bila Baraza.

Kwanini Nyerere aligombana na akina Takadir?
Hii ni mada nyingine. Nimepata kujadiliana na rafiki yangu mwanazuoni Mohamed Said. Nitakuja siku moja kusimulia.

Nani anastahili kuwa Mzee Wa Dar es Salaam?
Ndio, kuna Mzee mmoja wa Dar es Salaam alipata kuniambia, kuwa sifa ya kwanza ya kuwa ‘Mzee wa Dar Es Salaam’ ni lazima uwe na zaidi ya umri wa miaka 50. Uwe mkazi wa Dar Es Salaam kwa miaka isiyopungua 20 mfululizo!

Hilo halijaandikwa popote, lakini ‘Wazee’ wenyewe wa jiji wanauzingatia utaratibu huo. Aliniambia.

Na kuna “Kijana wa Dar es Salaam” alipata kuninong’oneza, kuwa wako mbioni kuwashawishi wazee wa jiji waongeze sifa za kuwa mzee wa Darisalama.

Kwamba ili uwe Mzee wa Dar Es Salaam ni sharti, ama uwe umezaliwa na kukulia Dar, au umezaliwa nje ya Dar lakini ujana wako wote umeishi Dar. Hivyo basi, unapoteza sifa ya kuwa Mzee wa Dar es Salaam kama umekuja Dar ukubwani!

Na Wazee wa Dar Es Salaam wana Mwenyekiti wao. Kwa kawaida siku ya ‘shughuli’ ya wazee, Mwenyekiti wao huvalia kanzu, kibagharashea na kizibau.

Ndiye huyu ambaye huwa wa kwanza kumpokea ‘Mkuu wa Kaya’ anapoingia ukumbini kuwahutubia wazee.

Ni kwa namna gani basi Mwenyekiti wa Wazee wa Dar Es Salaam anachaguliwa?
Hilo ni swali la kizushi na usithubutu kuliuliza mbele ya ‘Wazee wa Dar es Salaam’- watakutoa mbio kwa bakora!

Lakini , lililo dhahiri ni kuwa, Wazee Wa Dar Es Salaam hawajawahi kuwa na Mwenyekiti mwanamke. Na leo itakuwa ni mara yao ya kwanza kuhutubiwa na Mkuu wa Kaya Mwanamke.

Kwenye uenyekiti, hata Bi. Titi Mohammed hakupata kufikiriwa. Heshima ya kumpa barabara kuitwa kwa jina lake ilitosha, na amshukuru Julius, alipata kuniambia Mzee ' orijino’ wa Dar Es Salaam.

Ndio, Mkuu yeyote wa Kaya katika nchi hii atashauriwa aongee mbele ya Wazee wa Dar Es Salaam kama ana kubwa analotaka liwafikie wananchi.

Katika miaka ya karibuni Rais wa nchi, hayati Magufuli, alipata kulihutubia taifa kupitia Wazee wa Mkoa wa Dodoma.

Inasemekana jambo hilo liliwashtua baadhi ya Wazee wa wa Dar Es Salaam. Na kuna siku nilitembea kwa miguu mitaa ya Kariakoo Kusini; Livingstone, Mahiwa, Swahili na mingineyo.

Hatimaye nikafika kwenye kijiwe cha chai na kahawa pale Mtaa wa Lumumba. Nilukuta mjadala juu ya Wazee wa Dar Es Salaam. Na hapo nikayasikia manung’uniko.

Ndio, baadhi ya Wazee wa Dar Es Salaam wanaamini pia, kuwa Ilala ndio Dar Es Salaam. Na kwamba ni Wazee wa Ilala ndio waliompokea Julius Nyerere alipoingia mjini.

Wanahoji;

Iweje Wazee wa ‘mashambani’ Kinondoni na Temeke nao waitwe Wazee Wa Dar Es Salaam?

Swali linabaki;

Wazee Wa Dar Es Salaam ni akina nani?

Ni Tafakuri Jadidi.

Maggid Mjengwa,

Dar es Salaam.
Huyu Mzee Tabu Mangala hakika Mungu alimjalia hekima na maono ya hali ya juu.

Ushauri aliompa Nyerere hakika ndio maisha yetu halisimtaani hadi hivi leo, wengi tuna madaftari ya mkopo kwenye maduka ya Mangi na Wapemba, hakika wanatustiri watu hawa, ukitaka kujuwa siri zetu waulize hawa Mangi na mpemba kama vile siku hizi ukitaka kujuwa siri za dada zetu wewe waulize bodaboda wa mtaani kwake.
 
Back
Top Bottom