Magoli 10 ya kufungwa katika mechi mbili,Simba inabaki vipi kama ilivyo?

Kufungwa kwa Simba tena kwa idadi hiyo ya magoli ni kielelezo cha uduni wa ligi yetu.

Ni Kama ilivyo kielelezo cha ubora wa ligi dhidi ya ile ya eSwatini.

Long term ni kuboresha ligi yetu. Kuna mafyongo mengi sana. Kwa ubora upi tuwe na timu 20 TPL?

Hata timu za Yanga na Simba wakileta wachezaji wazuri toka nje ya nchi,watabweteka kwa ligi yetu mbovu. Wanajiona mastaa wakubwa. Kibembembe kinakuja wakikutana na walio bora. Tunavuna hizo tano tano.
 
Ni kweli sisi tunaweza kuwa ni underdog kwa al ahaly na as vital ilo tupo pamoja!!!! Mimi hoja yangu ni kwa hawa professional players tunaowalipa millionz of money, na mwisho wa siku they deliver nothing kwenye haya mashindano ndomana Mimi naungana na mtoa mada lazima kitu kifanyike. Thamani ya kikosi cha as vital ni 1.6billion na simba 1.8b meanz kumbe tunauwezo mzuri tu wakukinunua kikosi kizima cha as vital. Why as vital kikosi chao thamani yao kinaenda na thamani ya simba lakini wao wanaperform sisi tu nashindwa. Kuna matatizo mengi sana kwenye idara ya usajili wa simba ndomana wameweza kutuletea garasa kaulibaly na hapa hapa majuzi juzi wametuleta wachezaji kwa ajili ya majaribio badala ya kununua complete players.Inatupasa tuanze upya
 
Siioni Simba ikibadilika chini ya Kocha Aussen.
Mkataba wake ukiisha na aondoke tu.
Timu iko slow sana kama wakati wa Amog.
Aussen hana kingine tena zaidi ya hapa. Sikuzote Simba inacheza vile vile na hakina jipya tena.
Tofauti na Yanga, Kocha Zahera unaona kabisa anaibadilisha timu kila siku.
Na Simba ikukutana ya Yanga safari hii tena, haitakuwa mechi nyepesi kama ile ya kwanza na hakika kuna dalili ya Yanga kuondoka na ushindi.
Wakati Simba ikionekana iko vilevile Zahera anaoneka kufanya kitu flanj cha tofauti ktk Clabu ya Yanga.
Zero tu Aussen


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nini simba kufungwa khamsa bana, TP Mazembe kamshindilia mtu themaniya mpaka unajiuliza haya matimu mengine yalifikaje hiyo hatua?
 
Kiongozi, thamani ya vikosi vya Vita na Simba kuwa karibia sawa sawa, lakini Vita kuwa juu, inaonyesha ligi ya Congo ni bora kuliko ya kwetu.
Ufumbuzi ni mmoja tu. Tuumize vichwa kuboresha ligi yetu iwe na ushindani wa kutosha.
 
Habari zinasema kuwa jana kipindi cha pili AL AHLY waliambiwa Mo Dewji ambaye ni mmiliki wa simba ni mwarabu pia, ndio wakatuonea huruma. Inasemekana kipindi cha kwanza walijua mmiliki ni mtu mweusi.
 
Kiongozi, thamani ya vikosi vya Vita na Simba kuwa karibia sawa sawa, lakini Vita kuwa juu, inaonyesha ligi ya Congo ni bora kuliko ya kwetu.
Ufumbuzi ni mmoja tu. Tuumize vichwa kuboresha ligi yetu iwe na ushindani wa kutosha.
Hii nakubaliana na wewe Mkuu!!!! Ligi dhaifu nayo inachangia haya
 
Acha maneno weye nyinyi mechi ya jana wamecheza wachezaji 9 mnaowaita proffessional player na mmekufa 5 acheni mdomo rudini nyumbani mmalizie viporo kwa kichapo kikali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari zinasema kuwa jana kipindi cha pili AL AHLY waliambiwa Mo Dewji ambaye ni mmiliki wa simba ni mwarabu pia, ndio wakatuonea huruma. Inasemekana kipindi cha kwanza walijua mmiliki ni mtu mweusi.
Ww na iyo avatar yako imeendana na akili yako, ww ni kuku na akili yako pia inauwezo wa kuku,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabisa mkuu, tofauti na hapo nikama tunaigiza
 
Acha maneno weye nyinyi mechi ya jana wamecheza wachezaji 9 mnaowaita proffessional player na mmekufa 5 acheni mdomo rudini nyumbani mmalizie viporo kwa kichapo kikali

Sent using Jamii Forums mobile app
Samahani dada haya mambo ya soka niya wanaume wewe huwezi kuyaelewa hasa tukija kwenye upande wa tactics.

By the way, niko na mke tayari sihitaji mwingine so try your luck somewhere else.
 
Hii ya 5 super ni zawadi nzuri sana kwa WALACE KARIA, ameijua nguvu ya TUNDU LISU, sasa achague kuwa mwenyekiti wa CCM au aendelee kuwa mwenyekiti wa TFF aendelee kupokea zawadi, shubamit...Nahisi yule golikipa wa simba ana ubinadamu ulio pitiliza, katoa zawadi nzuri sana kwa MH. LISSU.
 
Simba ni chama la wana hakuna team hapo poleni kwa ,,,,KHAMSAA,,

Sent from my using Tapatalk
 
Wamesha badilisha makocha vya kutosha, wamesaji kila mchezaji aliye wavutia kiasi cha kujiita wanakikosi kipana. Tatizo in ligi yetu ya mipango. ligi ya simba na yanga, tff ya simba na yanga na nchi ya simba na yanga. Tutafanikiwa tu pale tutakapo amini juu ya ushindani wa kweli. Timu ipate matokeo kwa uwezo wake siyo maelekezo toka juu ama imani za kishirikina. Wanao haribu mpira ni wachache kwa tamaa za kipuuzi ikiwemo maslahi ya kisiasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alisema kocha wa nkana simba hamna mabeki Badala kufanyia kazi mkaleta Koriebali
 
Kikubwa kwa simba ni kudhibiti nidhamu ya wachezaji. Hata kama unawachezaji wa kiwango cha chini ila wakijenga nidhamu kila mchezaji akajituma matokeo yanapatikana.

Mimi niliifatilia timu ya Enyimba fc mwaka 2003 mpaka wanakwenda kuwa mabingwa. Wachezaji wake walikua niwazalendo kweli kweli walijituma sana pia uongozi wa enyimba ulijenga spirt ya nidhamu kwa timu hata ilipo poteza kwa idadi kubwa ya magoli kwa Ismailia ilijipanga na ikatwaa ubingwa mara 2 mfululizo.

Tatizo la simba nikuchekea wachezaji. Mimi nadhani kwenye mapinduzi cup na sport pesa ilitakiwa viongozi wawachukulie baadhi ya wachezaji hatua kali za nidhamu ili wajitambue kwamba wanawajibika ipasavyo wakiwa kiwanjani.

Kwa beki hi wasipochukua hatua magoli mengine 10 yakotu. Hapa ndipo ninapo wakumbuka. Victory costa nampoka na Bonifas pawasa, ramadhani waso ulikua hupiti kizembe. simba ya mwaka 2003 ilikua bora sana japo ilikua nachangamoto kubwa ya kifedha na uwekezaji tofauti na sasa.
 
Huwezi kabisa ukalinganisha mpira wa Tanzania na ule wa Egypt na ikumbukwe kuwa hawa Al Ahly ni bingwa mara nane wa hili kombe or in other words they're perennial champions.

Nakumbuka hawa waarabu mwaka 1982 waliwahi kuichakaza Yanga bao 5-0 huko Cairo kwenye mashinano kama haya na kutoka nao sare ya 1-1 jijini Das es Salaam. Pia mwaka 1985 kwenye kombe la washindi Afrika waliitoa tena Simba ktk round ya pili kwa jumla ya magoli 3-2, Simba walishinda mechi ya kwanza Mwanza 2-1 kabla ya kuchapwa 2-0 huko Cairo.

Inaonekana Simba ya safari hii "Is no match to the Egyptian side" tofauti hata na ile ya 1985 ya akina Zamoyoni Mogella, Mtemi Ramadhani, Kiwelu Mussa, Malota Soma, Zuberi Magoha, Athumani Maulid, Moses Mkandawire, Ramadhani Leni nk.

Simba hawana "Pace" na hilo wapinzani wao wameshalifahamu na ktk kila mechi huo udhaifu ndio utakuwa kaburi lao na hata Physical Fitness kwa maana nzima ya "Stamina", Simba bado sana sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…