Sibonike
JF-Expert Member
- Dec 23, 2010
- 17,296
- 18,027
Kufungwa kwa Simba tena kwa idadi hiyo ya magoli ni kielelezo cha uduni wa ligi yetu.Timu iliyofungwa na Simba katika mechi ya kwanza ilishamtimua Kocha wake. Sasa inapata matokeo. Imetoa sare na wababe wote wa Simba.
- Kocha hajafukuzwa
- Benchi la Ufundi halijaguswa
- Wachezaji hawajachunguzwa au kuwajibishwa
- Viongozi hawajafukuzwa wala kuhojiwa
Simba kuweni serious. Hii ni Klabu Bingwa Barani Afrika. Mnatuwakilisha Tanzania. Mkiaibishwa tunaaibishwa sote. Mkifanikiwa na kupata sifa tunapata sifa sote.
Simba haiwezi kubaki kama ilivyo sasa!
Ni Kama ilivyo kielelezo cha ubora wa ligi dhidi ya ile ya eSwatini.
Long term ni kuboresha ligi yetu. Kuna mafyongo mengi sana. Kwa ubora upi tuwe na timu 20 TPL?
Hata timu za Yanga na Simba wakileta wachezaji wazuri toka nje ya nchi,watabweteka kwa ligi yetu mbovu. Wanajiona mastaa wakubwa. Kibembembe kinakuja wakikutana na walio bora. Tunavuna hizo tano tano.