Magoli 10 ya kufungwa katika mechi mbili,Simba inabaki vipi kama ilivyo?

Magoli 10 ya kufungwa katika mechi mbili,Simba inabaki vipi kama ilivyo?

🤔🤔🤔🤔🤔
 
Sidhani kama suluhisho ni kufukuza kocha au kupangua benchi la ufundi (unless sababu za vipigo hivyo ni hao watu na ni za makusudi)

Kila team huwa inafungwa, cha muhimu ni kujitathmini ni wapi hapakuwa sawa ili kujirekebisha next time out.

Ukisema kufukuza fukuza zingatia mikataba n.k inaweza kuiweka club katika hali ambayo sio nzuri (financially)
Ndio kila timu inafungwa lakini siyo goli 10 kwa mechi 2.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpira ni uwekezaji wenzetu wamewekeza vizuri kwa miaka mingi sisi Simba ndio tunaanza uwekezaji na mkataba aliosaini kocha wa Simba ni kuhakikisha timu inafika kwenye makundi msimu huu na amefikia malengo...kwaio tunajua tunachokitafuta sisi bado wachanga katika huu mpira wa kisasa ila Tumeanza mikakati na malengo ya Simba ni ndani ya miaka mitano (5) tuwe tumetwaa kombe la Africa kwaio huu ndio Kwanza mwaka wa pili....Ushauri tukitaka kushindana kikweli kweli ni kuchukua wachezaji kweli kweli kwenda Zambia kuchukua mfungaji Bora wa ligi yao,Kwenda Ghana kuchukua Beki bora,Kwenda Kenya kuchukua Beki bora,Kwenda Uganda kuchukua winga Bora, Yani nikwenda kuchukua Top player ilo ndio wanalolifanya Mazembe...uzuri kwamba Mo dewji ukiacha uwekezaji pia ni shabiki kindaki ndaki Kama sisi matokeo haya nae yamemuumiza Sana Kama sisi

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkitwaa ilo kombe nakun*ya iringa mbeya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli ligi yetu sio bora.Hata pale mwaka 2003 simba ile ya Siang'a(Rip) ilipowatoa mabingwa watetezi Zamalek ligi yetu bado haikuwa bora!

Proffesional aliyekuwepo Simba kipindi kile ni Ramadhani Wasso pekee (kama sikosei).Kwa hiyo kukosekana proffesionals sahihi haiwezi pia kuwa sababu ya kufungwa 5 bila mechi mbili mfululizo ugenini.

Soura,timu ya Algeria ambayo simba iliwafunga 3 bila hapa Dar,wamekataa kufungwa na AS Vita (ugenini) na Al Ahly (nyumbani).Na wala simba isitegemee mteremko huko Algeria kwakuwa Soura wamejifunza makosa yao.

Pamoja na udhaifu wa soka letu ambalo wengi mmeliongelea.Pamoja na upungufu tulionao kama taifa kwenye mipango yetu ya mpira kuanzia kwenye grassroots...lakini kwa vipigo hivi vya simba hatuwezi kujificha kwenye sababu hizihizi za kila siku.Game approach.....Unapocheza na timu iliyokuzidi uwezo inabidi kuiheshimu tu na kucheza kwa tahadhari huku ukiviziazizia kushambulia.Simba hawajafanya hivyo mechi zote mbili za Vita na Ahly....Wanaenda kwenye mchezo as if wapo level moja na hizo timu.Kosa kubwa sana na ndomana wanapigwa vipigo vya ajabu..Ingewezekana kabisa kufungwa kwa heshima au hata kutoa sare kwenye hizo mechi mbili kama tu kocha wa simba angekuwa na approach sahihi na kuwatumia wachezaji sahihi kwenye hiyo approach.Kukomaa na 4-4-2 huku una Kagere na Okwi mbele,na Chama akicheza nyuma yao ni dhahiri hutaki kujilinda...ni kama unaenda kucheza na Mwadui tu!Hata ukiwapa majukumu ya kukaba hawa watu hawawezi...

Alikuwa ana option bora zaidi ya kuweka viungo watano na mshambuliaji mmoja tu ambaye anatumika kwenye counter akisaidiwa na Chama ambaye atakuwa anaunganisha kiungo na ushambuliaji na kusaidia attacking mnapokuwa na mpira.Kagere angeanzia benchi nafasi angechukua kiungo mkabaji labda Mzamiru na kucheza 4-5-1 mbele Okwi pekee.Hapa priority inakuwa ni kuwazuia waarabu wasikufunge na wala sio kushindana nao kufunga!Mkiwazuia dakika 45 wasifunge hata wao wanakuja a bit frustrated kipindi cha pili na watakuja wamechemka na mnaweza kutumia hiyo advantage kufanya counters kadhaa kipindi cha pili.Kwa kufanya hivi hata mkipoteza mchezo haiwezi kuwa kwa mabao mengi hivyo na ambayo yanawaharibia psychology wachezaji wenu.Na mnajiweka vibaya zaidi kwenye kundi kuruhusu magoli mengi itakapotokea mmelingana points!

Kocha akubali kuwa amekosea kwenye game plan na ajirekebishe kuliko kuanza kutoa visingizio vya ajabu eti sijui simba haina wachezaji wakuweza kucompete kimataifa!Angekataa hiyo kazi in the first place mpaka simba ipate hao wachezaji wa kimataifa anaowaongelea..Kukubali kukiongoza kikosi cha simba kwenye michuano hii ni uthibitisho kuwa aliridhika na kikosi....akubali makosa yake tusonge mbele,asilete blablaaa......
 
Mkuu mpira umeanza lini kuujua? Samahani kwa swali hilo ila sina nia ya kukudharau ila nashangaa kuona kuwa Simba kufungwa goli 10 ndani ya dakika 180 ni jambo la ajabu hasa ukizingati aina za team tulizocheza nazo.

Hii haina tofauti na na Ulaya kule ukute team labda ya Romania huko CFR Cluj imequalify kucheza CL alafu iko group moja na top dogs wa Ulaya labda Barca na team nyingine tuchukue hata Schalke 04. Hapo unategemea Cluj watafurukuta vipi?

Tuweni realistic jamani, tuliposhinda ile mechi ya mwanzo watu mlikua na over expectations. Mlikua delusional.
Kwa maelezo yako unakubaliana na shafii kuwa simba ni underdog
 
Ni kweli sisi tunaweza kuwa ni underdog kwa al ahaly na as vital ilo tupo pamoja!!!! Mimi hoja yangu ni kwa hawa professional players tunaowalipa millionz of money, na mwisho wa siku they deliver nothing kwenye haya mashindano ndomana Mimi naungana na mtoa mada lazima kitu kifanyike. Thamani ya kikosi cha as vital ni 1.6billion na simba 1.8b meanz kumbe tunauwezo mzuri tu wakukinunua kikosi kizima cha as vital. Why as vital kikosi chao thamani yao kinaenda na thamani ya simba lakini wao wanaperform sisi tu nashindwa. Kuna matatizo mengi sana kwenye idara ya usajili wa simba ndomana wameweza kutuletea garasa kaulibaly na hapa hapa majuzi juzi wametuleta wachezaji kwa ajili ya majaribio badala ya kununua complete players.Inatupasa tuanze upya
Hawa professional tunaokoteza tu ndugu, hatujawa makini na mashindano haya,
 
Spurs alimfunga Wigan 9 ndani ya dakika 90.. Man U alimfunga Arsenal 8 ndani ya dakika 90.

Ni mpira gani nyie huwa mnaangalia?
Kibaya ni timu kushindwa kukaba wkt hawana uwezo wa kushinda, sio mbaya tujifunze
 
Wa Misri wananunua wachezaji kutoka EPL, simba wananunua wachezaji kutoka Lipuli fc halafu mnataka matokeo mazuri like serious?
 
Kiongozi, thamani ya vikosi vya Vita na Simba kuwa karibia sawa sawa, lakini Vita kuwa juu, inaonyesha ligi ya Congo ni bora kuliko ya kwetu.
Ufumbuzi ni mmoja tu. Tuumize vichwa kuboresha ligi yetu iwe na ushindani wa kutosha.
Mkuu wenzetu wacongo kwao ni njaa kali na maisha ni magumu ndyo maana wachezaji wao wakipata nafasi ya kuchezea hizi timu kubwa wanajituma kweli kweli kwa sababu wanajua nje ya hpo mtaani hakukaliki na akizembea tu namba inachukuliwa na mwenye njaa zaidi tofauti na bongo mchezaji hta akipigwa benchi anapewa posho elfu themanini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wenzetu walipoingia Makundi wakafanya usajii wa kufa mtu,Simba wanamchukuea Zana ambaye amekaa miezi sita bila kucheza,leo tena wanaleta wachezaji wa kuwafanyia majaribio,kweli?.

Juzi tena wamemsajili Mchezaji wa Timu ya Ndanda ,Vitalis Mayanga kutoka timu inayoshika nafasi ya 17 kwenye msimamo wa Ligi yetu ili akafanye maajabu gani Ligi ya Mabingwa Afrika wakati hata Mapinduzi Cup hajawahi kucheza kama si utani ni nini jamani?
 
Back
Top Bottom