Magolikipa waliotamba zamani nchini

Magolikipa waliotamba zamani nchini

Freedom tommorrow

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2015
Posts
1,795
Reaction score
1,131
Naomba niwakumbushe kuanzia miaka ya 1970 mpaka miaka 1990. Tanzania iliwahi kuwa na makipa mahiri sana walipokuwa langoni. Yule ambaye hakuwai kuwaona hata mmoja kati ya hawa nitakaowataja hapa chini basi ni kweli walikosa uondo, ingawa wengi wao wameshatoweka duniani lakini bado tunawakumbuka. Je nani alikuwa kipa bora? Mimi naona ni marehemu athumani mambosasa

1. athumani mambosasa- alikuwa na kipaji kikubwa sana alipokaa langoni- alichezea simba
2. omari mahadhi bin jabir- alikuwa pia na kipaji kikubwa sana jezi yake ilikuwa namba 0- simba
3. hamisi kinye- alikuwa haomtoki mpira mkononi. Uliwahi kumtoka siku yanga ilipocheza na majimaji ya songea mwanzoni mwa miaka 1980, iliukwa ni mpira uliopigwa na selestin sikinde mbunga-alichezea yanga
4. juma pondamali- alikuwa na madaha na mbwembwe nyingi alipokua langoni- alichezea pan africa
5. joseph fungo- alikuwa mgumu sana kufungika- alichezea yanga
6. iddi pazi- alikuwa kipa mzuri sana miaka ile. Ndie aliyekuwa mpigaji mzuri wa penalt-alichezeasimba
7. madata lubigisa- alitamba sana kipindi chake baada ya kuwa na defence imara ya kina george masatu- alichezea pamba ya mwanza.
8. ali bushiri- akikaa golini alikuwa anapendeza, taifa stars walipata taabu sana kumfunga walikuwa wanakutana na zanzibar. Alichezea kmkm ya zanzibar
9. james msigala- alikuwa kipa mrefu sana, na alikuwa afungiki kwa mipira ya juu- alichezea plisner
10. Mohamed mwameja- a
likuwa hafungiki kirahisi katika penalt, ndiye aliyeipa ubingwa simba kwenye michuano ya afrika na kati kule zanzibar-alichezea simba
11. Ramadhani korosheni-
ni kipa mzuri alikuwa anadaka vizuri sana vichwa vya mbizi vya abeid mziba-alichezea small simba ya zanzibar.
12, Kichochi Lemba- Alivuma kwa umahiri wake alipokuwa langoni na wakati mwingine alikuwa anavaa kofia akiwa golini pia alijua sana kucheza mipira cross na mipira ya kona- Alichezewa RTC KAGERA

Ama kweli magolikipa tulikuwanao
 
Steven Nemensi wa simba
Ofen Martin ''Chusa'' Ushirika enzi hizo
Peter Manyika wa Yanga
 
Ndio maana hamuweki picha zenu na hamtimii majina yenu kwa sababu ya hayo maharage sasa kipa wew unaleta majina ya wasio makipa
 
Kuna Patric Mwangata, pia alikuwa pan, sasa hivi kocha, ila huyu ni baada ya miaka ya 90
 
Athumani Msomali- Reli Kiboko ya vigogo morogoro

Joseph Katuba- Yanga, Simba

Rifat Saidi- Yanga
 
Mohamed Nyalusi,Yanga.

Sadik Kalokola,Yanga

Joseph Katuba,R.I.P,Yanga

Rifat Said,R.I.P,Yanga

Doyi Moke,Yanga

Chachala Muya,Yanga.
 
mohamed nyalusi,yanga.

Sadik kalokola,yanga

joseph katuba,r.i.p,yanga

rifat said,r.i.p,yanga

doyi moke,yanga

chachala muya,yanga.

mtani unanichekesha sana ha ha ha ha: Lakini nakubari kitu kimoja sidhani kama yanga mpaka sasa WAMEMPATA kipa mzuri kama hamisi kinye. yule kipa nilimkubali. NAKUMBUKA TAIFA STARS ILIPOPAMBANA NA HARAMBEE STARS PALE KENYA KWENYE MWAKA 1980-82 HIVI ALIKUWA GUMZO. ILA ALITOLEWA KIPINDI CHA PILI BAADA YA KUKUTANA NA FORWARD HATARI WA HARAMBEE JJ MASIGA WOTE WALIUMIA NA KUTOLEWA NJE. Nakumbuka mtangazaji hamed jongo wa rtd kipindi kile alikuwa anamsifu kwa kuruka kama nyani. Hao uliwaweka hapo hakuna hata mmoja aliyemfikia.
 
Athumani Msomali- Reli Kiboko ya vigogo morogoro
Joseph Katuba- Yanga, Simba
Rifat Saidi- Yanga


  1. wakati Athumani Msomali anadakia Reli, sub yake alikuwa Duncan Mwamba, kwa waliowahi kumuona huyu golie, alikuwa similar or near to Juma Pondamali, na hasa pale Reli inapokuwa mbele kwa magoli kadhaa.
  2. Sahau Saidi Kambi (rip), huyu nitasikitika sana kama wapenzi wa Yanga hawamkumbuki, huyu alikuwa bonge la golie katika historia ya Jangwani, alitokea Morogoro, huyu alisababisha headline maarufu sana katika magazeti ya chama - UHURU na MZALENDO enzi hizo, headline iliitwa "SAHAU ENDAPO HATASAHAU" kisa hiki nakiweka kiporo kwa leo, ila tu kwa uchache ni kwamba, mechi ilipigwa Taifa - shamba la bibi, saa 10.30, kilichotokea hapo, Minziro anajua, ila watoto wa Morogoro Mjini saa 3 usiku siku hiyo hiyo ya game, tupo Mtaa wa Nunge, kwao na kina Sahau Kambi, anatupa post match info, rip sahau.
  3. Saburi Abeche: Huyu hakupata umaarufu maskini ya Mungu, kama kuna watu wanalidai soka la bongo, huyu nae yumo. Mshikaji alidakia SUA (Sokoine Univ), kipindi hicho timu iko daraja la pili, inapambana kuingia ligi daraja la kwanza, bonge la golie, connection yake na Gulamali pamoja na Sahau, ilimfikisha Yanga, huku timu ya SUA ikifa bila kupanda daraja, akiwa YANGA hakupata nafasi ya kudaka, wenye namba zao, tena walikuwa wanadaka kwa zamu ni SAHAU na NEMES.

Jamani Zamani Tamu.
 
Back
Top Bottom