SoC01 Magonjwa ya Afya ya akili yanatibika, vunja ukimya

SoC01 Magonjwa ya Afya ya akili yanatibika, vunja ukimya

Stories of Change - 2021 Competition

Baba Swalehe

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2017
Posts
20,178
Reaction score
39,641
" Daktari huwezi kuelewa ntakachokuambia bora nife nacho " yalikua ni maneno ya mgonjwa wangu niliyekua namhudumia kwa muda mrefu , niligundua ana matatizo zaidi yanayopelekea afya yake kudhorota siku baada ya siku

Afya ya akili kwa kimombo (mental health) ni swala ambalo limekua likichukuliwa kwa mzaha katika jamii zetu za kiafrika , ukisikia kuhusu afya ya akili ndugu msomaji akili yako lazima itakupeleka moja kwa moja kuwaza " UKICHAA " .

Afya ya akili sio ukichaa , afya ya akili ni uwezo wa akili mtu kufanya vitu kwa usahihi , kufikiri kwa usahihi , kutenda kwa usahihi , Ni uwezo wa ubongo kuchanganua mambo na kuyafanya kwa usahihi, mtu unaweza usiwe kichaa lakini hutendi kwa usahihi au hufikiri kwa usahihi . Unawaza kufa tu kila saa unawaza dunia yote imekutenga hayo yanaweza kuwa ni mawazo yako lakini sio sahihi

Ubongo wa binadamu umetengenezwa kwa namna ya tofauti sana tatizo lolote linaloweza kutokea kwenye ubongo linaweza kupelekea matatizo mengine mengi kwenye viungo vingine vya mwili unachukua asilimia mbili tu ya uzito wa mwili mzima lakini asilimia ishirini ya nishati nzima ya mwili inapelekwa kwenye ubongo, wanasayansi bado tunajaribu kuchunguza uhusiano wa matatizo ya akili na reaction mbali mbali zinazotokea kwenye ubongo lakini kwa uchache (nitatumia lugha rahisi ili kila mtu hata asiyesoma sayansi afahamu) naweza kusema matatizo mengi ya afya ya akili yanatokana na kukosekana kwa uwiano katika kemikali mbalimbali za saketi kwenye ubongo (neurones) mfano wa kemikali hizo ni serotonini na neuroepinephrine (nimekosa neno lake la kiswahili ).

Hizi nyuroni huwasiliana zenyewe kwa zenyewe na katika kuwasiliana hutumia kemikali nilizozitaja hapo juu na zingine nyingi inapotokea hakuna uwiano wa kemikali ndipo hapo mtu tunasema ubongo wake umepata shida na hafanyi mambo kwa usahihi mfano kunapokua na utengenezwaji mwingi wa kemikali ya dopimine katika saketi za ubongo hapo ndipo tunasema mtu ana ukichaa uliopitiliza( psychosis) , ndo hawa tunawaona wanaokota makopo kwenye mabarabara.

Kwa mtu mwenye msongo mkubwa wa mawazo inamaanisha kemikali za serotonini zinatengenezwa kwa kiwango kichache sana katika nyuroni zake za ubongo , serotonini sisi wataalamu wa afya hupenda kuiita " kemikali ya furaha" sababu ikipungua furaha ya mtu hupungua na hata hamu ya kula hupungua.

Kwa hiyo ubongo ni kama kiungo chochote kila kwenye mwili kwamba na chenyewe kinaweza kuumwa na kinaweza pata ajali hata maneno tu yanaweza kufanya ubongo upate ajali mfano unatukanwa au unadhalilishwa na mtu unayempenda kila siku na shida kubwa inakuja kwamba ubongo ndo unaongoza ogani zingine za mwili hivyo unapopata shida ogani zingine zitadhurika pia na hilo ndilo lilikua linatokea kwa mgonjwa wangu nliyemtaja mwanzo wa hili andiko

kwa hiyo kama tulivyoona hapo juu kwa uchache afya ya akili ni jambo linalohusu kukosekana kwa uhusiano wa kemikali mbali mbali za ubongo ,Hivyo jamii inapaswa itambue kwamba ukiwa na tatizo la akili sio kwamba wewe ni kichaa ni kwamba umeumwa kama unavyoweza kuumwa meno au mguu ndio ukichaa ni ugonjwa wa akili lakini sio kila ugonjwa wa akili ni ukichaa , sisi kama jamii inapaswa tuwe na uelewa wa kuweza kuwsaidia watu mbali mbali wanaopitia matatizo ya afya ya akili wakiwemo vichaa bila kuwabagua.

Mtu anapokufuatwa na kukuelekeza shida yake jaribu kumsikiliza kama vile tulivyoona kwamba maneno yanaeza kuuletea ubongo ajali tafiti zinaonyesha maneno ya kufariji na kutia moyo yanaweza kupelekea mtu akapata ahueni katika mambo yanamkabili . Mtu akikwambia ana msongo wa mawazo tusimuone kama mtu weak mtu anayejiendekeza hii ipo kwetu sana wanaume na ndio wahanga wakubwa wa magonjwa ya akili.

Usikimbilie katika kufanya hitimisho la nini anaumwa msikilize kwa umakini , tafuta sehemu iliyotulia ongea nae sio lazima ukubaliane na anachoongea lakini kwa kuonyesha unajali hisia zake utakua umemsaidia pakubwa sana , muulize maswali machache yanayoweza kumfanya aongee zaidi lakini sio maswali yanayoweza kumfanya ajihukumu zaidi

Tunakutegemea wewe unayesoma hapa kuwa nyenzo ya kutuletea mtu mwenye magonjwa ya akili ili sisi tushughulike nae kitaalamu zaidi , jaribu kumshauri kwamba inapaswa awaone pia wataalamu wa afya hapo ni baada ya kumshauri maneno kadhaa ya kutia moyo na kubwa katika yote angalia na umsome huyo mtu kama ana mawazo ya kujidhuru na u deal na hilo jambo haraka kadri unavyoweza

katika makala zingine zinazofuata tutaongelea nini mtu anapaswa kufanya anapohisi ana tatizo la afya ya akili , hatua za kuchukua na pia tutaongelea nini serikali inapaswa ifanye kutatua matatizo haya leo tumeongelea jamii inapaswa ifanye nini na ielewe nini kuhusu afya ya akili usisahau ku vote kwenye alama ya ^ hapo chini

NIMALIZIE KWA KUSEMA " MAGONJWA YA AKILI YANATIBIKA VUNJA UKIMYA"
Asanteni sana
 
Upvote 98
Mfano, umetumia elufu kumi per day lakini ukasau umeitumia kununulia nini, au ukakumbuka vitu viwili tu vingine umesahau.

Mufano mwingine mkuu, umepewa maerezo mengi lakin ukayasahau baazi ya maerezo hayo, always ni ivyo.

321ea332-9bbb-4e2d-8274-9300c1f2e9ef.jpg

Sifanyi biashara ila nimeikuta mahal itakusaidia sana
 
Nimewahi kukutana na watu wako very smart kupita maelezo ila Kuna vitu anafanya Hadi unashangaa na kuona ka dish limeyumba, wengine pia huwa hawalali kabisa na kila siku humeza vindonge vya kutuliza akili, hivi hyo nayo ni kichaa au ni kitu gani?
Maana Hali kwao wanakuwa hawalali na hawachoki ni kukesha na ku overdue baadhi ya vitu
 
Kuna magonjwa tunajifunza kuishi nayo mfano schizophrenia... A very complex psychosis disorder

For schizophrenia naamini kuna siku wanasayansi tutatengeneza matibabu yake

Hata kwa surgery tu
nimepitia kusoma huko wanasema bangi inaweza kupunguza hilo tatizo...
 
nimefikiria tu huko majumbani,makazini wakina mama wanakuwaga na matendo unajiuliza kama ni akili yake au ya jirani
Wamama Wana shida sana, kuanzia mahusiano, kulea Yani full stress aisee.
 
Ila wengine tunalogwa na familia zetu wakishaona unaupewe Fulani au wazazi kukupenda kuliko wao

Imani potofu hizi
Alisikika mlevi mmoja
 
Nimewahi kukutana na watu wako very smart kupita maelezo ila Kuna vitu anafanya Hadi unashangaa na kuona ka dish limeyumba, wengine pia huwa hawalali kabisa na kila siku humeza vindonge vya kutuliza akili, hivi hyo nayo ni kichaa au ni kitu gani?
Maana Hali kwao wanakuwa hawalali na hawachoki ni kukesha na ku overdue baadhi ya vitu
Mkuu Watu wenye ukichaa huo unausemea unaitwa " schizophrenia"

Katika ubongo wao kemikali inayoitwa dopamine huwa inazalishwa kwa wingi

" dopamine ni rewarding chemical au kemikali ya mizuka 😁

Hawa watu huwa na delusions na hallucinations za hatari lakini hio kitu haiwazuii wao kufanya mambo ya kuushangaza ulimwengu mfano john nash akiwa na miaka 27 aliweza aliandika dissertation paper ya " non cooperative games iliyompa nobel prize later

Aristotle ashawahi sema" there is no genius without having a touch of madness

Sad enough many creative geniuses are more prone to major disturbances hii inatokana na hizi kemikali kuzalishwa kwa wingi kwenye brain zao

Wolfgang alikua na mood swings, lincolin na alexander the great hawa wote walkua wanadai wanaona mapepo 🤣

Albert Einstein mwanae alipata schizophrenia

Sio wote wenye schizophrenia ni magenius hapana ila kuna ma genius wanapata schizophrenia na wanafanya vitu hatari

Nkitoka kazini ntaandika zaidi... Bye
 
Ila wengine tunalogwa na familia zetu wakishaona unaupewe Fulani au wazazi kukupenda kuliko wao

Imani potofu hizi
Alisikika mlevi mmoja
Hahaha

Sawa bwana mkubwa

Ila haya mambo yapo yana run genetically

Mfano kama family yako ina impairment ya AKT1 Gene ina yo regulate dopamine level basi unakua vulnerable kupata schizophrenia
 
Back
Top Bottom