SoC01 Magonjwa ya Afya ya akili yanatibika, vunja ukimya

Stories of Change - 2021 Competition

Baba Swalehe

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2017
Posts
20,178
Reaction score
39,641
" Daktari huwezi kuelewa ntakachokuambia bora nife nacho " yalikua ni maneno ya mgonjwa wangu niliyekua namhudumia kwa muda mrefu , niligundua ana matatizo zaidi yanayopelekea afya yake kudhorota siku baada ya siku

Afya ya akili kwa kimombo (mental health) ni swala ambalo limekua likichukuliwa kwa mzaha katika jamii zetu za kiafrika , ukisikia kuhusu afya ya akili ndugu msomaji akili yako lazima itakupeleka moja kwa moja kuwaza " UKICHAA " .

Afya ya akili sio ukichaa , afya ya akili ni uwezo wa akili mtu kufanya vitu kwa usahihi , kufikiri kwa usahihi , kutenda kwa usahihi , Ni uwezo wa ubongo kuchanganua mambo na kuyafanya kwa usahihi, mtu unaweza usiwe kichaa lakini hutendi kwa usahihi au hufikiri kwa usahihi . Unawaza kufa tu kila saa unawaza dunia yote imekutenga hayo yanaweza kuwa ni mawazo yako lakini sio sahihi

Ubongo wa binadamu umetengenezwa kwa namna ya tofauti sana tatizo lolote linaloweza kutokea kwenye ubongo linaweza kupelekea matatizo mengine mengi kwenye viungo vingine vya mwili unachukua asilimia mbili tu ya uzito wa mwili mzima lakini asilimia ishirini ya nishati nzima ya mwili inapelekwa kwenye ubongo, wanasayansi bado tunajaribu kuchunguza uhusiano wa matatizo ya akili na reaction mbali mbali zinazotokea kwenye ubongo lakini kwa uchache (nitatumia lugha rahisi ili kila mtu hata asiyesoma sayansi afahamu) naweza kusema matatizo mengi ya afya ya akili yanatokana na kukosekana kwa uwiano katika kemikali mbalimbali za saketi kwenye ubongo (neurones) mfano wa kemikali hizo ni serotonini na neuroepinephrine (nimekosa neno lake la kiswahili ).

Hizi nyuroni huwasiliana zenyewe kwa zenyewe na katika kuwasiliana hutumia kemikali nilizozitaja hapo juu na zingine nyingi inapotokea hakuna uwiano wa kemikali ndipo hapo mtu tunasema ubongo wake umepata shida na hafanyi mambo kwa usahihi mfano kunapokua na utengenezwaji mwingi wa kemikali ya dopimine katika saketi za ubongo hapo ndipo tunasema mtu ana ukichaa uliopitiliza( psychosis) , ndo hawa tunawaona wanaokota makopo kwenye mabarabara.

Kwa mtu mwenye msongo mkubwa wa mawazo inamaanisha kemikali za serotonini zinatengenezwa kwa kiwango kichache sana katika nyuroni zake za ubongo , serotonini sisi wataalamu wa afya hupenda kuiita " kemikali ya furaha" sababu ikipungua furaha ya mtu hupungua na hata hamu ya kula hupungua.

Kwa hiyo ubongo ni kama kiungo chochote kila kwenye mwili kwamba na chenyewe kinaweza kuumwa na kinaweza pata ajali hata maneno tu yanaweza kufanya ubongo upate ajali mfano unatukanwa au unadhalilishwa na mtu unayempenda kila siku na shida kubwa inakuja kwamba ubongo ndo unaongoza ogani zingine za mwili hivyo unapopata shida ogani zingine zitadhurika pia na hilo ndilo lilikua linatokea kwa mgonjwa wangu nliyemtaja mwanzo wa hili andiko

kwa hiyo kama tulivyoona hapo juu kwa uchache afya ya akili ni jambo linalohusu kukosekana kwa uhusiano wa kemikali mbali mbali za ubongo ,Hivyo jamii inapaswa itambue kwamba ukiwa na tatizo la akili sio kwamba wewe ni kichaa ni kwamba umeumwa kama unavyoweza kuumwa meno au mguu ndio ukichaa ni ugonjwa wa akili lakini sio kila ugonjwa wa akili ni ukichaa , sisi kama jamii inapaswa tuwe na uelewa wa kuweza kuwsaidia watu mbali mbali wanaopitia matatizo ya afya ya akili wakiwemo vichaa bila kuwabagua.

Mtu anapokufuatwa na kukuelekeza shida yake jaribu kumsikiliza kama vile tulivyoona kwamba maneno yanaeza kuuletea ubongo ajali tafiti zinaonyesha maneno ya kufariji na kutia moyo yanaweza kupelekea mtu akapata ahueni katika mambo yanamkabili . Mtu akikwambia ana msongo wa mawazo tusimuone kama mtu weak mtu anayejiendekeza hii ipo kwetu sana wanaume na ndio wahanga wakubwa wa magonjwa ya akili.

Usikimbilie katika kufanya hitimisho la nini anaumwa msikilize kwa umakini , tafuta sehemu iliyotulia ongea nae sio lazima ukubaliane na anachoongea lakini kwa kuonyesha unajali hisia zake utakua umemsaidia pakubwa sana , muulize maswali machache yanayoweza kumfanya aongee zaidi lakini sio maswali yanayoweza kumfanya ajihukumu zaidi

Tunakutegemea wewe unayesoma hapa kuwa nyenzo ya kutuletea mtu mwenye magonjwa ya akili ili sisi tushughulike nae kitaalamu zaidi , jaribu kumshauri kwamba inapaswa awaone pia wataalamu wa afya hapo ni baada ya kumshauri maneno kadhaa ya kutia moyo na kubwa katika yote angalia na umsome huyo mtu kama ana mawazo ya kujidhuru na u deal na hilo jambo haraka kadri unavyoweza

katika makala zingine zinazofuata tutaongelea nini mtu anapaswa kufanya anapohisi ana tatizo la afya ya akili , hatua za kuchukua na pia tutaongelea nini serikali inapaswa ifanye kutatua matatizo haya leo tumeongelea jamii inapaswa ifanye nini na ielewe nini kuhusu afya ya akili usisahau ku vote kwenye alama ya ^ hapo chini

NIMALIZIE KWA KUSEMA " MAGONJWA YA AKILI YANATIBIKA VUNJA UKIMYA"
Asanteni sana
 
Upvote 98
Jamii nyingi za kiafrika huwatenga na kuwaficha watu wenye ugonjwa wa akili kama vile kuwafungia kwenye chumba ambacho wakati mwingine huwa kina giza hivyo kuwazidishia athari zaidi kiakili. Jamii nyingi huwapa majina yasiyofaa watu wenye dalili za ugonjwa wa akili, majina kama vile: kichaa, chizi, dishi limeyumba, mwehu, mwendawazimu, mtambo, chupa imepooza n.k. Zipo familia ambazo kwa kuhofia kunyanyapaliwa na jamii, huwaficha watu wenye ugonjwa wa akili au kutokuwa wazi kusema ndugu yao ana ugonjwa wa akili.

Msaidie mtu mwenye matatzo ya akili
 
baadhi ya magonjwa ya akili yanaweza kurithiwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia ya vinasaba. Hata hivyo si kila atakayezaliwa na mzazi ama koo zenye historia ya magonjwa ya afya ya akili kwamba lazima atarithi ugonjwa huo. Wapo watakaorithi ugonjwa huo lakini pia wapo ambao hawatarithi ugonjwa. Baadhi ya magonjwa yaliyo na uwezekano wa kurithiwa ni pamoja na skizofrenia(schizophrenia) . Huu ni ugonjwa ambao mtu hupoteza uwezo wa kutofautisha uzoefu halisi na ule usio halisi kama vile kuona na kusikia vitu ambavyo watu wengine hawavioni wala kuvisikia.

Amka... Magonjwa ya akili yanatibika
 
" Daktari huwezi kuelewa ntakachokuambia bora nife nacho " yalikua ni maneno ya mgonjwa wangu niliyekua namhudumia kwa muda mrefu , niligundua ana matatizo zaidi yanayopelekea afya yake kudhorota siku baada ya siku

Afya ya akili kwa kimombo (mental health) ni swala ambalo limekua likichukuliwa kwa mzaha katika jamii zetu za kiafrika , ukisikia kuhusu afya ya akili ndugu msomaji akili yako lazima itakupeleka moja kwa moja kuwaza " UKICHAA " .

Afya ya akili sio ukichaa , afya ya akili ni uwezo wa akili mtu kufanya vitu kwa usahihi , kufikiri kwa usahihi , kutenda kwa usahihi , Ni uwezo wa ubongo kuchanganua mambo na kuyafanya kwa usahihi, mtu unaweza usiwe kichaa lakini hutendi kwa usahihi au hufikiri kwa usahihi . Unawaza kufa tu kila saa unawaza dunia yote imekutenga hayo yanaweza kuwa ni mawazo yako lakini sio sahihi

Ubongo wa binadamu umetengenezwa kwa namna ya tofauti sana tatizo lolote linaloweza kutokea kwenye ubongo linaweza kupelekea matatizo mengine mengi kwenye viungo vingine vya mwili unachukua asilimia mbili tu ya uzito wa mwili mzima lakini asilimia ishirini ya nishati nzima ya mwili inapelekwa kwenye ubongo, wanasayansi bado tunajaribu kuchunguza uhusiano wa matatizo ya akili na reaction mbali mbali zinazotokea kwenye ubongo lakini kwa uchache (nitatumia lugha rahisi ili kila mtu hata asiyesoma sayansi afahamu) naweza kusema matatizo mengi ya afya ya akili yanatokana na kukosekana kwa uwiano katika kemikali mbalimbali za saketi kwenye ubongo (neurones) mfano wa kemikali hizo ni serotonini na neuroepinephrine (nimekosa neno lake la kiswahili ).

Hizi nyuroni huwasiliana zenyewe kwa zenyewe na katika kuwasiliana hutumia kemikali nilizozitaja hapo juu na zingine nyingi inapotokea hakuna uwiano wa kemikali ndipo hapo mtu tunasema ubongo wake umepata shida na hafanyi mambo kwa usahihi mfano kunapokua na utengenezwaji mwingi wa kemikali ya dopimine katika saketi za ubongo hapo ndipo tunasema mtu ana ukichaa uliopitiliza( psychosis) , ndo hawa tunawaona wanaokota makopo kwenye mabarabara.

Kwa mtu mwenye msongo mkubwa wa mawazo inamaanisha kemikali za serotonini zinatengenezwa kwa kiwango kichache sana katika nyuroni zake za ubongo , serotonini sisi wataalamu wa afya hupenda kuiita " kemikali ya furaha" sababu ikipungua furaha ya mtu hupungua na hata hamu ya kula hupungua.

Kwa hiyo ubongo ni kama kiungo chochote kila kwenye mwili kwamba na chenyewe kinaweza kuumwa na kinaweza pata ajali hata maneno tu yanaweza kufanya ubongo upate ajali mfano unatukanwa au unadhalilishwa na mtu unayempenda kila siku na shida kubwa inakuja kwamba ubongo ndo unaongoza ogani zingine za mwili hivyo unapopata shida ogani zingine zitadhurika pia na hilo ndilo lilikua linatokea kwa mgonjwa wangu nliyemtaja mwanzo wa hili andiko

kwa hiyo kama tulivyoona hapo juu kwa uchache afya ya akili ni jambo linalohusu kukosekana kwa uhusiano wa kemikali mbali mbali za ubongo ,Hivyo jamii inapaswa itambue kwamba ukiwa na tatizo la akili sio kwamba wewe ni kichaa ni kwamba umeumwa kama unavyoweza kuumwa meno au mguu ndio ukichaa ni ugonjwa wa akili lakini sio kila ugonjwa wa akili ni ukichaa , sisi kama jamii inapaswa tuwe na uelewa wa kuweza kuwsaidia watu mbali mbali wanaopitia matatizo ya afya ya akili wakiwemo vichaa bila kuwabagua.

Mtu anapokufuatwa na kukuelekeza shida yake jaribu kumsikiliza kama vile tulivyoona kwamba maneno yanaeza kuuletea ubongo ajali tafiti zinaonyesha maneno ya kufariji na kutia moyo yanaweza kupelekea mtu akapata ahueni katika mambo yanamkabili . Mtu akikwambia ana msongo wa mawazo tusimuone kama mtu weak mtu anayejiendekeza hii ipo kwetu sana wanaume na ndio wahanga wakubwa wa magonjwa ya akili.

Usikimbilie katika kufanya hitimisho la nini anaumwa msikilize kwa umakini , tafuta sehemu iliyotulia ongea nae sio lazima ukubaliane na anachoongea lakini kwa kuonyesha unajali hisia zake utakua umemsaidia pakubwa sana , muulize maswali machache yanayoweza kumfanya aongee zaidi lakini sio maswali yanayoweza kumfanya ajihukumu zaidi

Tunakutegemea wewe unayesoma hapa kuwa nyenzo ya kutuletea mtu mwenye magonjwa ya akili ili sisi tushughulike nae kitaalamu zaidi , jaribu kumshauri kwamba inapaswa awaone pia wataalamu wa afya hapo ni baada ya kumshauri maneno kadhaa ya kutia moyo na kubwa katika yote angalia na umsome huyo mtu kama ana mawazo ya kujidhuru na u deal na hilo jambo haraka kadri unavyoweza

katika makala zingine zinazofuata tutaongelea nini mtu anapaswa kufanya anapohisi ana tatizo la afya ya akili , hatua za kuchukua na pia tutaongelea nini serikali inapaswa ifanye kutatua matatizo haya leo tumeongelea jamii inapaswa ifanye nini na ielewe nini kuhusu afya ya akili usisahau ku vote kwenye alama ya ^ hapo chini

NIMALIZIE KWA KUSEMA " MAGONJWA YA AKILI YANATIBIKA VUNJA UKIMYA"
Asanteni sana
aliyejitangaza ana faili mirembe apelekwe, aliwashi mpiga mtu rungu la kichwa, tafadhali sana wananzengo hapo DOM mpelekeni jamaa.
 
Elimu ya afya ya akili ni muhimu sana kwa jamii kwani ndiyo inayoishi na watu wenye matatizo ya afya na ugonjwa wa akili. Jamii ikipata elimu itaweza kutambua dalili za watu wenye ugonjwa wa akili na kuwapa msaada mapema.
 
Ni kweli mkuu,topic yako nimeipenda stigma juu ya wagonjwa wenye matatizo ya afya ya akili itaweza kuisha kama kutakua na awareness ndanii ya jamii...and you are creating awareness so you deserve some votes! 👍 👍 👍
 
Jamii inapaswa itambue hilo

Pia wanawake wajawazito ni muhimu kuzilinda afya zao za akili pia sana
 
Ni kweli mkuu,topic yako nimeipenda stigma juu ya wagonjwa wenye matatizo ya afya ya akili itaweza kuisha kama kutakua na awareness ndanii ya jamii...and you are creating awareness so you deserve some votes! 👍 👍 👍
Amina naamini itakuwepo katika mada zitakazoshinda....

Jumapili ntaandika mwendelezo

Karibu sana
 
Athari za kutoshughulikia matatizo ya afya ya akili kwa vijana ni kubwa kwa mujibu wa WHO na mara nyingi zinaendelea hadi ukubwani na kuwakosesha fursa ya kushamiri katika maisha yao.... Hivyo ni muhimu kulinda na kujilinda wenyewe
 
Back
Top Bottom