Asante kwa kuanziasha mada hii, naamini tutaweza kushare experience na baadhi hata kupata suluhisho la matatizo haya
Binafsi nina mzazi mwenye shida hiyo, ni mama yangu mzazi, according to the history, baba alitueleza kwamba mama alipata hilo tatizo dakika chache baada ya kujifungua mdogo wetu wa mwisho, hapo ilikua nni mwaka 1989, since then baba hakuweza kufanya chochote zaidi ya kutule maana sisi tulizaliwa watatu na tulipishanainterval ya miaka miwili,
Wakati mama anapata tatizo sisis yulikua bado watoto kwa hiyo baba alibeba jukumu la kutulea bila msaada wa ndugu,
Bahati nzuri Mungu alitujaalia wote mimi pamoja na wadogo zangu kufanya vizuri kwenye masomo mpaka tumefika mahali tunajitegemea
Shida ya mama kubwa ni kuongea mwenyewe ni kama vile anakua anaongea au anabishana na mtu tusiemuona, wakati mwingine anaogopa hatuelewi anaogopa nini au analia tu bila sababu, hapendi kukaa karibu na watu na anamuoa kila mtu kama afui isipokua sisi familia yake
Mbaya zaifi huwa anaondoka nyumbani tunamtafuta mpaka tunachoka na akionfoka wakati mwinhine inachukua hata miezi mpaka arudi
Kiukweli kuna wakati huwa tunaishi kwa tension sana kwa kumchunga na kujitahidi kuwa karibu nae
Nilipopata kazi nikampeleka mama kea daktari bingwa wa magonjwa ya akili na akaanza dawa, mpaka sasa anaendelea vizuri na anafanya shughuli zake kama mtu mwenye akili timamu
Sent using
Jamii Forums mobile app