Mtanzanias
JF-Expert Member
- Jul 30, 2021
- 1,747
- 3,725
Nimeona bwana Crescentius Magori ametweet kwamba wamesalitiwa kwenye mechi ya leo na inaonekana kuna baadhi ya wachezaji wataangushiwa jumba bovu muda si mrefu kuwa wameisaliti timu.
Kitu ambacho bwana Magori na viongozi wenzake awataki kukubali ukweli kwamba timu waliyonayo kwa sasa ni tofauti na ile ya msimu uliopita, na bado wameuza Chama na Miquisone wakashindwa kutafuta wachezaji wa maana wakaenda kusajili wachezaji wa gharama nafuu ili wawatengeneze badae wawauze tena.
Sasa kwa mfumo huo ambao wanaenda nao simba kwa sasa ni ngumu kuupata tena ubora wake, leo Magori anasema wamesalitiwa lakini hapo hapo yule Babra alisema Manara ndio alikuwa msaliti akamuondoa ina maana hiyo timu kwa sasa imejaa wasaliti.
Timu imeonekana haijiwezi kuanzia mechi za ndani, sisi tunaojua mpira tulikuwa tunasema ni suala la muda tu simba itakata moto na ndicho kinachotokea msianze kuwaangushia jumba bovu wachezaji wakati timu iko hoi aieleweki inacheza mfumo gani uwanjani ni ilimradi tu bora liende!
Mnaposimamisha wachezaji na nyie viongozi mjitafakari