Ronal Reagan
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 5,298
- 3,059
Hehhhhhhhhhhehe ... mahindi sasa kilo 600/=, naona mavuno yamechelewa kidogo, ila ndiyo hivyo. I was just a couple of months late na tusubiri bei ya unga ianze kupungua. Utaelewa tu!
Actually ni kinyume na hivyo, miezi 4 ya mwaka bei huwa juu na miezi 8 bei huwa ya kawaida. Hii si kwa Tanzania tu, bali eneo lote la Afrika Mashariki. Na mwaka huu, mvua zimechelewa kwa hiyo kwa karibu miezi saba mfululizo bei y6a mahindi imekuwa juu.Labda wewe Kobello unataka tu kukoleza stori ili genge lisipoe!
Sasa ikiwa kati ya miezi 12 ya mwaka, miezi 2-3 bei inakuwa around shs 600 lakini miezi 9-10 iliyobaki bei inakuwa zaidi ya shs 800 na wewe unaona ni sawa, basi mimi sina la kusema zaidi ya kuwa nimetambua maslahi yako ni ya kiitikadi tu na wala sio wananchi na Taifa kwa ujumla.
Kinacholipwa hapo ni 15% ya mapato yote ya mwaka (estimated) ambayo ni kama 3T shs ambazo ni principal za ndani na capital ya nje.Tuliyoyaonya huko nyuma taratibu yanatimia. Hivi karibuni Serikali imetangaza kutenga TZS trilioni 9 kwa ajili ya deni la taifa. Hii ni Sawa na karibia 58% ya mapato ya kodi. Kwa maana hii, 42% itakayosalia ndio itatumika kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Maendeleo (assuming TRA targets are met), huku Serikali ikilazimika kukopa zaidi kutoka vyanzo mbalimbali vya gharama ya juu kwani concessional lenders wanazidi kutukimbia.
Kwa kipindi cha 1990-1993 Serikali ilikuwa ikitumia 28% ya mapato ya kodi kulipa deni la taifa, and we headed for disaster. Mgogoro wa kiuchumi kuelekea 2020 utakuwa ni mkubwa sana largely kwa sababu ya economic mismanagement lakini kama kawaida visingizio vitaendelea kutolewa kwa kasi kubwa na utetezi wa hali ya juu kudanganya watanzania wasiojielewa.
Tutajadili hili kwa undani zaidi Bajeti mpya itakapotangazwa Siku chache baadae.