Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,434
- Thread starter
- #181
Kubali tu ulikosea, uliuvaa mkenge. Lengo lako ni exaggeration lakini hapo umelewa mwenyewe.
View attachment 454128
Gunia la mahindi December 2, 2015 kutokana na Takwimu hizo.
Average minimum 60,500/- na average maximum price 67,750/-.
Bei ya juu Morogoro na Mwanza (85,000)
Bei ya chini ni Songea (47,000/-).
Kwa kuwa utasema hizi ni data za kupikwa, nakuwekea clip ya wakaazi wa Mbeya wakihojiwa kuhusu bei za vyakula
Angalia 8:17 mpaka 8:44 uone trend ya bei ya mahindi, na ufananishe takwimu za idara ya masoko na wakaazi wa Mbeya kuhusu bei ya mahindi (hiyo ilikuwa may 2016).
Pia,
Wednesday, January 23, 2013
Serikali yatangaza bei mpya ya unga Dar
Serikali yatangaza bei mpya ya unga Dar
Hiyo ni link kama unataka kuhakikisha kuwa mwaka 2013 January (actually from Dec. 2012) bei ya unga wa mahindi ilikuwa 1500/- kwa kilo. Ikapunguzwa baada ya tangazo hilo mpaka kufikia 900/-.
Hakuna cha bias! Hizi takwimu zikionyesha hali mbaya huwa mnazikumbatia sana.
Na kwa kuonyesha jinsi ulivyo muongo na mbabaishaji rejea post yako #10 kwenye uzi huuhuu ambapo umejadili inflation kwa kutumia figures hizi hizi za NBS ukidai kwamba inflation inayotakiwa tuifuate ni ya vyakula (11% from jan 2015 to jan 2016).
Sasa hapo huoni kama unajimix mwenyewe???
Kuhusu hivyo vitakwimu uchwara vya Zitto kabwe eti kuna nafaka za siku nane .. hebu jiulize mwenyewe kama mwaka jana October kulikuwa na 254,000 tonnes na mpaka October 2016 kulikuwa na 90,000 tonnes. Is 90,000 one eighth (13%) ya 254,000? Ninavyojua mimi ni one third (35%).
Pili jiulize, amejuaje kuwa tani 90,000 za mahindi zinatosha siku nane? Na tani 254,000 zinatosha miezi miwili(61 days)?
Kuhusu wewe kubishana na mimi mambo ya kisiasa ...... pshht! Please mayn!
Takwimu zako ni zile zile ambazo i have questioned na kujaribu sana kukuamsha kutoka kwenye usingizi pono wa msukule kwamba thats not the 'absolute truth'. Swali lako kuhusu national reserve ya chakula linaonyesha jinsi gani you are ignorant on these issues but also jinsi gani unatumika kama msukule kusafisha visivyo safishika.
Majibu kwa swali lako lipo mdomoni mwa Waziri mwenye dhamana ya Kilimo (Chizeba) ambaye juzi ametamka rasmi kwamba akiba ya chakula iliyopo inaweza lisha taifa kwa siku saba tu incase of emergency? Sasa with your ignorance, endelea kupiga mahesabu ya 61 days, 91 days as if we are here to discuss maturity of treasury bills. Bei reflects supply and demand, i hope your ignorance self will realise that by now. You are definitely confused. Usiwe unaparamia mambo tu kuhalalisha ujira wako. Nenda kule jukwaa la siasa kwa akina MsemajiUkweli, Ritz, Lizaboni, na viongozi wako wengine humu mkapige siasa. GT sio jukwaa la siasa.
Anachosema Waziri Chiseza is very much in line with my earlier concern kwamba takwimu kuhusu akiba ya taifa ya chakula na hata food inflation zimejaa ulakini kuliko ukweli. Natarajia urudi na spinning juu ya alichokisema Waziri. Mtumbueni maana anasema ukweli ambao always ni mchungu kwa genge lililopo Lumumba.
Kwa mtu ambae anafuatilia mjadala huu objectively, taarifa ya Waziri kwa kiasi kikubwa inafanya sehemu kubwa ya takwimu zako na mijadala yako yote ielekee nyumbani kwake - kwenye choo cha shimo. The fact remains kwamba theres food insecurity inayonyemelea taifa, na muda sio mrefu uhalisia utajitokeza katika mfumuko mkubwa wa bei za vyakula (of which i have always maintained kwamba takwimu released haziakisi uhalisia). Muda sio mrefu wananchi wengi wataanza kufa njaa, lakini kwa vile CCM has always survived kwa exploitation ya mkulima kwa mfumo ule ule wa kikoloni, you will care less.
-Tayari Longido (ITV news @8PM, 3/1/2017) tumesikia wananchi hawana chakula na badala yake wameamua kubadilishana mbuzi la beberu kwa debe moja la mahindi. Lakini pamoja na kupata hayo mahindi, bado wanakosa fedha za kwenda kusaga wapate sembe kwa ajili ya kusonga ugali kwa sababu hakuna fedha katika mzunguko.
-Nadhani pia umesikia kuna mikoa wananchi wameanza kushindia wadudu kama mlo.
-Pia huko Morogoro ambapo ni moja ya food baskets za taifa, leo ukibeba mfuko wa mahindi kurudi nao mjini baada ya Xmas na Mwaka mpya, njia nzima unakodolewa macho.
-Pia nadhani unakumbuka Rais alilazimika kutembelea magereza mwezi November Mwaka jana na moja ya concerns zake ni kwamba food reserve ya taifa inakuputika and his estimation, wafungwa ndio wanaomaliza akiba hiyo, wanadoea vya bure, wafanye kazi ya kuzalisha chakula chao wenyewe. Inasemekana wafungwa wengi wanaachiwa huru kama njia ya kutanua national food reserve. What a deficit in policy making!
-Mwisho nadhani unakumbuka wakuu wa wilaya (makada wenu Lumumba) walionywa kwamba asisikike hata mmoja akilalamika wananchi wake wana njaa. Kwa vile wapo kutetea matumbo yao, most likely wengi watakuwa na taarifa juu ya njaa na pengine hata vifo vitokanavyo ba uhaba wa chakula lakini hawawezi kusema ukweli kuogopa kutumbuliwa, na badala yake kuwaletea vitakwimu ambavyo mnatembea navyo humu and elsewhere vifua mbele kwamba thats the absolute truth.
Inasikitisha sana.