Magufuli 2015-2020: Matarajio ya uchumi na changamoto zake

Magufuli 2015-2020: Matarajio ya uchumi na changamoto zake

Ronal Reagan waswahili husema subira yavuta heri, hapa naona kama inavuta 'shari'
Tumetuliza boli, right...

Katika nchi yetu iko tofauti kubwa kati ya makaratasi na uhalisia, lakini mwenzetu alishupalia makaratasi na wino wao tu!

Tulimweleza wazi kuwa wino na karatasi sio factor ya yeye kuweka mayai yote kwenye kapu moja, hakusikia wala kuelewa. Na kwa vile muda ni hakimu mzuri na wa haki, Machi aliyoisema imekuja na matokeo yako bayana kama jua.

Labda sasa tumwalike kwenye the way foward.
 
Kwa muda mrefu sasa baadhi yetu tumekua tukihoji malengo ya serikali ya awamu ya Tano kisera katika kusimamia uchumi wa nchi. Specifically tumekuwa tukihoji, je:

· Utekelezaji wa sera za uchumi chini ya Serikali ya wamu ya tano umekuwa ukienda sambamba na “appetite” (kiu/hamu) inayotawala uchumi wa taifa?

· Nini intakiwa kuwa kipaumbele kisera (uchumi) kwa upande wa Benki Kuu na kwa upande wa Serikali Kuu/Wizara ya Fedha/Hazina?

Kama ambavyo tumeshajadili kwa muda mrefu, uchumi wa nchi unaendeshwa/simamiwa kupitia njia kuu mbili:

1. Monetary Policy:

Monetary Policies zinakuja kwa sura mbili ambazo ni (Expansionary Monetary Policies & Contractionary Monetary Policies). Majukumu ya kusimamia uchumi kupitia Monetary Policies yapo chini ya BENKI KUU ya nchi, na ili kufanikisha hilo, Benki kuu huwa inatumia nyenzo zake mbali mbali kama vile interest rate (riba) nk. Lengo kuu hapa ni Benki Kuu ‘to influence’ mzunguko wa fedha ndani ya uchumi (Demand and Supply of money) kupitia ‘monetary policy tools’ kama vile riba (interest rates), open market operations (mauzo na manunuzi ya treasury securities), nk. Kwa mfano iwapo Benki Kuu itajiridhisha kwamba uchumi wa nchi umesinyaa kutokana na kushuka kwa shughuli za kiuchumi/uzalishaji na mzunguko wa fedha, na kiu iliyopo ni ongezeko la fedha katika mzunguko wa uchumi, basi BOT itachukua maamuzi kama vile kupunguza interest rate kwa lengo la kuongeza fedha katika mzunguko wa nchi; Kwa upande mwingine, pia iwapo BOT/benki kuu itajiridhisha kwamba uchumi wa nchi umepata joto kali/una ‘overheat’ kupelekea hatari ya mfumuko mkubwa wa bei, basi uamuzi utakuwa ni pamoja na kuongeza interest rate kwa lengo la kupunguza fedha katika mzunguko wa uchumi wa nchi.

2. Fiscal Policy:

Fiscal Policy ni njia kuu ya pili ya usimamizi wa uchumi wa nchi na jukumu hili lipo chini ya SERIKALI KUU/Wizara ya Fedha/Hazina. Kufanikisha jukumu hili, serikali kuu pia hutumia nyenzo zake mbalimbali (tofauti na zile chini ya Benki Kuu). Mara nyingi usimamizi/uendeshaji wa Serikali Kuu/Hazina/Wizara ya Fedha wa uchumi wa nchi huwa unapitia kwenye “Bajeti za serikali” ambapo Serikali kuu hutumia kwa mfano nyenzo zake kuu mbili ambazo ni ‘Kodi’ na ‘Matumizi’. Katika hili, lengo kuu huwa ni - shifting the budget position ya serikali ili kuendana na mahitaji/kiu/appetite ya uchumi kwa wakati huo. Kwa mfano, iwapo Serikali Kuu/hazina watajiridhisha kwamba uchumi wa nchi umesinyaa kutokana na kudorora/kupungua/kuanguka/kushuka kwa shughuli za kiuchumi/uzalishaji, na kushuka kwa mzunguko wa fedha, Serikali kuu inaweza kuja na maamuzi ya kisera ya kupunguza idadi ya kodi au viwango vya kodi (‘e.g Tax cuts’) sambamba na kuongeza matumizi ya fedha za umma; Na kwa upande mwingine, iwapo serikali kuu itajiridhisha kwamba uchumi wa nchi umepata joto kali/over heat, hali ambayo inaweza pelekea kuibuka kwa mfumuko mkubwa wa bei kwenye uchumi wa nchi, uamuzi wa Serikali Kuu huwa ni kupunguza fedha katika mzunguko wa uchumi kwa kupandisha viwango au idadi ya kodi na huku pia ikipunguza matumizi ya umma.

Tukijerea katika maswali yetu ya msingi hapo juu:

Maamuzi ya hivi karibuni ya BOT inawezekana yametusaidia kupata majibu kwa maswali husika. Hivi karibu, Benki Kuu ya Tanzania kupitia Gavana wake Beno Ndullu ilitangza uamuzi wa kuingilia mwenendo wa uchumi wa taifa kwa kupitia “Monetary Policy Tool” yake i.e ‘interest rate’ (Riba) ambayo sasa itashushwa kutoka kiwango cha sasa cha 16% hadi 12%. Kwa mujibu wa Gavana Ndullu, ‘appetite’ ya uchumi wa nchi ipo kwenye “Expansionary Policies”, angalau kwa jicho la Monetary policy (hence Expansionary Monetary Policy). Kwa maelezo yake mwenyewe, Gavana Ndullu amesema kwamba hatua hii ya BOT itasaidia kuongeza mzunguko wa fedha katika uchumi na pia upatikanaji wa fedha (mikopo/credit) kwa sekta binafsi. Ndullu alienda mbali na kusema pia kwamba kiwango hiki cha riba (12%) kitatumika pia ‘to discount treasury securities’. Maana yake hapa ni kwamba BOT inapunguza ‘yields’ on treasury securities kutoka kiwango cha 16% hadi 12%. Athari za hatua jhii ni kwama umma utapunguza ‘appetite’ ya hizi treasury securities kwa sababu kuzinunua haitalipa tena kama awali. Kitendo cha kununua treasury securities maana yake ni kwamba fedha zinatoka kwenye mikono ya wananchi kwenda BOT; Na kitendo cha umma kupunguza kasi ya kununua securities husika maana yake ni kwamba fedha nyingi zinabakia kwenye mikono ya wananchi/mzunguko wa uchumi.

Swali linalofuatia:

Je, Serikali Kuu/hazina/Wizara ya Fedha kwa upande wake itachukua maamuzi gani to complement maamuzi ya Benki Kuu/BOT?

Kwa kawaida, malengo ya ‘Monetary Policy’ (chini ya Benki Kuu) na ‘Fiscal Policy’ (chini ya Wizara ya Serikali Kuu/Wizara ya Fedha) yanatakiwa kulenga kitu kinachofanana. Kwa mfano, tuchukulie kuna changamoto/tishio kubwa ya ‘Mfumuko wa Bei’ katika uchumi wa Taifa. Athari zake huwa ni kubwa kwa mfano on ‘business confidence’, ‘cost of borrowing’(private sector), na ‘fall in real income’ za wananchi (iwapo mfumuko wa bei una kasi kubwa kuliko ongezeko la kipato/mishahara ya wananchi). Katika mazingira haya, Benki Kuu na Serikali kuu/hazina, wote wanatakiwa kuja na sera za “Contractionary Policies” – kwa maana kwamba - Benki Kuu kwa upande wake inatarajiwa kuja na “Contractionary Monetary Policies”, huku Serikali Kuu kwa upande wake nayo ikitarajiwa kuja na “Expansionary Fiscal Policies”.

Dhumuni la msingi la Monetary and Fiscal Policies ni kupunguza kitu kinaitwa ‘Cyclical Fluctuations’ ndani ya uchumi wa taifa. Katika hili, kitu kinachoangaliwa ni je Afya ya uchumi wa nchi ikoje – mfano kwa kuangalia viwango vya ‘inflation’ & ‘unemployment’ vilivyopo katika uchumi. Viwango vya inflation and Unemployment vina athari ya moja kwa moja kwenye mapato na mishahara ya watu; consumer demand or aggregate demand (total demand of all goods and services produced within the economy); bei za production inputs (raw materials kwa viwanda, agricultural inputs kama pembejeo n.k).

Wasi wasi wetu kuelekea Bunge lijalo la Bajeti (2017/2018):

· Je - tutegemee mgongano baina ya Monetary Policy & Fiscal Policy?

Kama tulivyokwisha ona, Benki Kuu wameshatoa uamuzi wao kwamab uchumi wa nchi unahitaji ‘expansionary Monetary Policy’. Kwa upande wa Serikali Kuu, bado wapo kimya, pengine wakiendelea kuona umuhimu wa ‘Contrationary Fiscal Policy’, au pengine wakisubiri bunge lijalo la bajeti. Vinginevyo mgongano huu ukiendelea kwa muda mrefu, utaumiza zaidi uchumi wa nchi kwa sababu:

Benki Kuu na Serikali Kuu/Wizara ya Fedha wanatakiwa kuwa well-coordinated kisera ili kuhakikisha kwamba kama uchumi unaelekea kuporomoka (kwa mfano ‘recession’) au kama unaelekea kukwama (kwa mfano ‘stagnation’), basi pande zote mbili zinakuja na mwelekeo mmoja kisera kukabiliana na changamoto husika.

Je - nini hutokea iwapo Benki Kuu na Serikali Kuu zinatofautiana ‘Kisera’ katika suala hili?

Kama tulivyokwisha ona, maamuzi ya BOT kupunguza interest rate (riba) maana yake ni kwamba BOT imejiridhishwa kwamba changamoto za sasa kiuchumi zinatakiwa kutatuliwa na ‘Expansionary Policies’. Kushuka kwa ‘interest rate’ kutapelekea - more bank lending, more business investment, and more consumer spending. Lakini ni muhimu sote tukafahamu kwamba hatua hizi za BOT zitakuwa ni za bure/kupoteza muda kama upande wa Serikali Kuu hautachukua hatua stahiki. Monetary Expansionary Policies zitabakia inadequate kutatua tatizo lililopo, hali ambayo itazidi kudhoofisha uchumi wa nchi. Ni hatari kwa uchumi wa Taifa na uchumi wa Wananchi iwapo - Monetary and Fiscal Policies are not in harmony/are out of sync!

Benki Kuu kuja na ‘expansionary monetary policy’ kwa kupunguza kiwango cha riba kutoka 16% hadi 12% bila ya msaada ya Fiscal Policies haiwezi kutatua changamoto ambazo Benki Kuu inajaribu kuzitatua. Hii ni kwa sababu athari za Monetary Policies katika uchumi zipo very uneven. Tofauti na wengi wanavyoweza kuamini/kuchukulia, private sector investment huwa haiamshwi na punguzo la riba (interest rate) peke yake. Badala yake, punguzo hilo linatakiwa kwenda sambamba na growth in aggregate demand (total demand of all goods and services produced within the economy) & economic growth.

Wakati ambapo kwa kawaida kasi kubwa ya kukua kwa uchumi huvutia uwekezaji kutoka sekta binafsi, high uncertainty na slowing growth hujenga mazingira ya economic ‘disaster’. Na katika nyakazi hizi ambapo sekta binafsi inakabiliwa zaidi na uncertainty, wawekezaji wa ndani wamekuwa wakisuasua kujiingiza in expensive and risky investments. Inasemekana kwamba tangia serikali ya awamu ya Tano iingie madarakani, investment activities pale kituo cha uwekezaji (TIC) zimepungua sana tofauti na huko nyuma; pia kupitia vyanzo mbalimbali, kumekuwepo na ripoti kwamba wafanya biashara wengi wanaondoka sokoni.

Kwa kumalizia, kuna haja ya Serikali Kuu - kupitia Wizara ya Fedha kuja na maamuzi (Expansionary Fiscal Policies) ambayo yatasaidia Benki Kuu ifanikishe malengo yake ya kuokoa janga ambalo linaweza kuja kutokea. Kwa upande wake, Benki kuu imeshafanya kazi inayopaswa kufanywa, sasa ni wakati wa Serikali Kuu kuisaidia BOT kufanikisha malengo husika ili kunusuru uchumi wa nchi.

Wawakilishi wetu bungeni wanatakiwa kuelewa umuhimu/uzito wa masuala haya na kuwakilisha vyema ‘concerns’ zilizopo kwa sababu wao ndio wakutuongelea sote katika ngazi husika. Ni muhimu waelewe kwamba punguzo la interest rate lililofanywa na BOT halitakuwa na maana bila ya Waziri Mpango kujna na ‘expansionary fiscal policies’. Bila ya uangalifu, uchumi wa nchi utazidi kuingia katika mgogoro mkubwa.

Wabunge wetu waelewe umuhimu wa Fiscal Expansionary Policy nyakati hizi ni kwamba:

Serikali ikiongeza matumizi yake katika uchumi wa nchi, it transfers funds kutoka kwenye ‘public cofers’ na kuzipeleka sekta binafsi, suala ambalo linapelekea ‘a multiplier effect’ katika uchumi wa taifa, sambamba na hatua za BOT (Expansionary Monetary Policy ya hivi karibuni). Umuhimu huu unakuja zaidi kwa kuzingatia ukweli kwamba the government accounts for over 50% of financial transactions in the economy. Kwahiyo hatua ya serikali kuja na expansionary fiscal policies itapunguza hali ya ‘uncertainty’ iiyopo na itajenga positive environment for private sector investment to flourish (kama inavyokusudiwa na BOT kupitia sera yake ya hivi karibuni).

Je Serikali ya magufuli kupitia Waziri Mpango itakuja na maamuzi hayo katika bunge lijalo la bajeti?

Tusubiri. Muda ndio mwamuzi sahihi katika hili.
 
Katika tasinia ya uongozi wataalamu wa mambo wanatoa nasaha kwa viongozi wote duniani kuwa kusoma vitabu kunawaongozea maarifa makubwa juu ya kuwaongoza binadamu kwakua manual ya binadamu ni vitabu vilivyoandikwa na binadamu.

Sasa katika kuliona hili katika Taifa letu leo kuna mambo kadhaa ambayo kwa kiasi kikubwa baadhi ya viungozi wetu kama wangejikita kusoma vitabu wangeweza kwa kiasi kikubwa kuja na majibu mujarabu wa changamoto nyingi zinazotukumba na kuzipatia uvumbuzi wa haraka na bila ya kuuacha makovu kwa wanainchi.

Sasa basi mimi na wewe tutoe ushauri kwa viongozi wetu kama leo ungeulizwa u Rais wetu asome kitabu gani katika kufikia hatua za juu za kuipaisha nchi yetu katika Nyanja zote ? ni kitabu gani ungeshauri?
 
51zvGi40dvL._SX331_BO1,204,203,200_.jpg


how-to-lead-effectively-3-638.jpg


leadership-game-plan-learn-how-to-lead-effectively-and-make-them-believe-in-you-with-these-leadership-skills-leadership_6636716.jpeg
 
1.Mastery
2.How to win friend and influence people
3. Things fall apart.
Asome kwanza hivyo ili abadili tabia, then tutampatia vingine vya kumjenga.
 
Mfalme Juha au Kusadikika...
Hivyo vya kimombo havitaeleweka na hata vikieleweka havitakaa kichwani..
Lakini inabidi tukiri kuwa kare kajamaa hakakuwa na maandalizi ya kuwa pale alipo sasa..
 
Katika nchi yetu iko tofauti kubwa kati ya makaratasi na uhalisia, lakini mwenzetu alishupalia makaratasi na wino wao tu!

Tulimweleza wazi kuwa wino na karatasi sio factor ya yeye kuweka mayai yote kwenye kapu moja, hakusikia wala kuelewa. Na kwa vile muda ni hakimu mzuri na wa haki, Machi aliyoisema imekuja na matokeo yako bayana kama jua.

Labda sasa tumwalike kwenye the way foward.
Hehhhhhhhhhhehe ... mahindi sasa kilo 600/=, naona mavuno yamechelewa kidogo, ila ndiyo hivyo. I was just a couple of months late na tusubiri bei ya unga ianze kupungua. Utaelewa tu!
 
Hehhhhhhhhhhehe ... mahindi sasa kilo 600/=, naona mavuno yamechelewa kidogo, ila ndiyo hivyo. I was just a couple of months late na tusubiri bei ya unga ianze kupungua. Utaelewa tu!
Kobello bwana...si mahindi tu, katika hali ya sasa vitu vingi vitapungua bei na sababu inajulikana!
 
Kobello bwana...si mahindi tu, katika hali ya sasa vitu vingi vitapungua bei na sababu inajulikana!
Na hiyo sababu ndiyo niliyokuwa nawaambia. The only thing ni kuwa off for a couple of months.
 
Back
Top Bottom