Elections 2015 Magufuli akutana na nguvu ya Umma Mbeya, azomewa, aambiwa wanamtaka Lowassa

Elections 2015 Magufuli akutana na nguvu ya Umma Mbeya, azomewa, aambiwa wanamtaka Lowassa

hamuezi kufanya uhuni na upuuzi then mkajusifia kuwa ni nguvu ya umma.nguvu ya umma haiwezi kuwa ya kitoto namna hiyo ,ila tukubali tukatae magufuli ndiye rais wetu na huo ni ukweli ambao watu wengi ahataki kuusikia
 
hao wazomeaji wasifikiri makufuli ni jk,kwamba atapotezea tu

Hii unamaanisha yale yanayosemwa kuhusu visasi vyake ni dhahiri ama???

Ukikutana na JK muulize Musoma na Mara kwa ujumla tulimkosea nini???
 
Kama kweli kazomewa ebu tuwekeeni picha tujiridhishe, vinginevyo tutachulia kuwa huo ni unafiki
 
mbeya leo asubuhi alipokuwa anaenda mbarali wananchi walizuia msafara wake na kumwambia wanataka mabadiliko na mtu wa kuyaleta mabadiliko ni lowassa

sina hakika kama mtoa post amefikiri sawasawa kabla ya kutuma hii post, kwasababu kwa mtu mfuatiliaji wa habari lazma atagundua kuwa magufuli hakua na mkutano wowote mkoani mbeya wala hakusimama kuzungumza na watu wambeya kabisa. Magufuli alikua makambako na hakuzomewa kabisa na watu leo, hizi propaganda za washikwa viuno sio za kuzingatia kabisa.
Jaribuni kuleta vitu vyenye mashiko kwa wote au kwa kundi flani.
 
Last edited by a moderator:
Mahala pengine Zomea zomea katika siasa ni silaha pekee ya mtu aliyeshindwa na ambaye siku zote kakata tamaa jambo ambalo ni tofauti sana kwa mji wetu wa mwanjelwa kwani wao wanashida ya kukosa uvumilivu wa hata kufikia hatua ya kutotoa nafasi sawa na haki ya upande mmoja, mfano kuchana nguo, mabango, na mambo mengine yanayoashiria uelewa mdogo kwenye siasa na hata ktk michezo kwani tumekuwa pia tukishuhudia ushabiki wa prison Vs mbeya city na hili limekuwa likichangiwa zaidi na hata aina ya viongozi tunaowapata kwa ngazi takribani zote kutokuwa taa kwa jamii kama vile tunavyoshuhudia uropokaji, na ushuhuda fitinishi majukwaani kana kwamba baada ya uchaguzi hakuna maisha tena

Vp kuhusu upigaji wa push up
 
pia ifahamike kuwa katika nchi kubwa kama hii yenye vyama vya siasa zaidi ya 20, ni vigumu watu wote kukupenda au kukukubali....ndio maana tunakutana na mambo kama kupingwa, kukataliwa sehemu flani flani. Hivyo mwenye kushadadia mtu kuzomewa jaribu kupanua fikra na sio mdomo.
 
Dodoma, Livingstone Lusinde
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imejadili kwa kina suala la kupanda kwa gharama za maisha nchini. NEC inakiri kwamba ni kweli lipo tatizo la kupanda kwa gharama za maisha nchini.

Tatizo hili pia limezikumba karibu nchi nyingi za Afrika Mashariki na kwakweli karibu sasa lipo dunia nzima.

Baadhi ya sababu za kupanda kwa gharama za maisha hapa nchini ni pamoja na;

1. Hali mbaya ya mavuno inayotokana na uhaba wa mvua au mvua kunyesha kipindi cha nje ya msimu katika maeneo mengi nchini.
2. Kuongezeka kwa bei ya mafuta duniani, hivyo kuongezeka kwa gharama za uzalishaji wa bidhaa na usafirishaji wa mazao.
3. Kuyumba kwa thamani ya dola ya Marekani.
4. Kuwepo kwa soko huria ambapo sasa mazao ya chakula yanapata soko nje ya nchi, na wakati mwingine kuuzwa nje kwa njia ya magendo na hivyo kusababisha uwepo wa ukubwa wa mahitaji na hivyo kuongezeka kwa bei ya chakula nchini.
5. kuongezeka kwa walaji wakati uzalishaji ukiwa mdogo.
6. kutofanikiwa (ikiwemo kuhujumiwa na wafanyabiashara wasio waaminifu) kwa baadhi ya mikakati ya kudhibiti mfumko wa bei.

Uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Taifa.

1. Pamoja na Serikali kuendelea kuchukua hatua za muda mrefu na wa kati za kukabiliana na tatizo hili, CCM inaiagiza Serikali kuchukua hatua za haraka za muda mfupi ikiwemo kuangalia upya baadhi ya kodi katika vyakula pamoja na kodi ya ongezeko la thamani VAT katika sukari.

2. Utaratibu wa ruzuku ya mbegu na mbolea upanuliwe ili kunufaisha wakulima wengi.

3. Serikali iongeze kasi ya utekelezaji wa mpango wake wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi chakula nchini, hasa kwa kupitia Hifadhi ya Nafaka ya Taifa, ikiwa ni pamoja na kujenga maghala zaidi ya mazao ya chakula katika maeneo ya uzalishaji wa mazao, na kutenga fedha nyingi zaidi kwa ununuzi wa mazao hayo. Pamoja na hili, mipango ifanywe kuongeza uwezo wa wakulima kuhifadhi chakula chao wenyewe na kupunguza upotevu baada ya mavuno (post-harvest losses).

3. Serikali iendelee kupanua utaratibu wake wa kutumia Hifadhi ya Nafaka ya Taifa (SGR) kama nyenzo ya kudhibiti kupanda kwa bei za vyakula. Wakati wa uhaba wa vyakula katika maeneo ya mijini, kasi ya kupeleka chakula maeneo hayo iongezwe na utaratibu mzuri zaidi wa usambazaji wa chakula utumike ili walaji, na sio wasafirishaji na wasindikaji, wanufaike.

4. Serikali iongeze kasi ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya kilimo nchini, hasa ASDP na SAGCOT, ambayo itasaidia kumaliza tatizo la chakula nchini na kuongeza ajira na kipato kwa Watanzania walio wengi.

5. Serikali idhibiti malipo ya huduma ya ndani kwa kutumia fedha za kigeni, hasa dola za kimarekani. Aidha, Serikali iongeze udhibiti wa Maduka na mahoteli yanayofanya biashara ya fedha za kigeni ili kuondoa hujuma kwa uchumi wa nchi inayofanywa kutokana na uhuru uliokithiri katika biashara hii.

6. Waajiri wahimizwe kupandisha mishahara na malipo mengineyo kwa wafanyakazi wao ili waweze kumudu gharama za maisha.

7. Serikali iweke jitihada zaidi za kudh ibiti ulanguzi wa bidhaa muhimu na upandishaji holela wa bei za vyakula, kodi za nyumba na usafiri.


Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
Ideology and Publicity Secretary
Posted by CCM Blog

Kumbe wanajua nn cha kufanya ili kupunguza gharama ya maisha na bado hawakufanya Kwa kipindi chote hicho. Kazi imewashinda pumzikeni
 
tunazijuwa sinema zenu, Tutamchagua Magufuli kwa kura nyingi coz tunajuwa lowasa anavyojiandaa kwenda kutufanyia biashara ikulu, mpeni salam tumeshtuka.

Labda wewe na mumeo.

Vote for UKAWA; vote for Lowassa.
 
Hiyo siyo nguvu ya umma ila ni uhuni.

Uhuni mtu yeyote akiamua anaweza kuufaya, lakini matokeo yake ni kuvujika kwa amani.

Kama wao wameshaamua kuwa wanamtaka Lowassa nini kinawapeleka kwenye mkutano wa Magufuli?

Inaonekana kabisa kuwa kuna kundi lililojiandaa kufanya fujo na walishaandaa camera wapige hii picha ya video.

Ukawa badala ya kuchekelea vitu kama hivi inabidi mvikemee kwa sabau watanzania hawapendi vurugu, hawatamchagua mtu anayeandaa vikundi vya vurugu.

Vurugu unaileta wewe kwenye video hamna vurugu bali kuna kinyume cha kushangilia.
 
Kwa nini NEC wanaruhusu mtu kupiga kampeni sehemu ambayo hana Ratiba haya mambo yatasababisha Vurugu
 

sina hakika kama mtoa post amefikiri sawasawa kabla ya kutuma hii post, kwasababu kwa mtu mfuatiliaji wa habari lazma atagundua kuwa magufuli hakua na mkutano wowote mkoani mbeya wala hakusimama kuzungumza na watu wambeya kabisa. Magufuli alikua makambako na hakuzomewa kabisa na watu leo, hizi propaganda za washikwa viuno sio za kuzingatia kabisa.
Jaribuni kuleta vitu vyenye mashiko kwa wote au kwa kundi flani.

Duuuuh kweli wewe hamnazo
 
hiyo ni kazi ya kitoto maana watu hawa wameandaliwa kuzomea hivyo kwetu wala sio tatzo tunajua muda utafika na ndipo mtakapokuja kujua kuwa magufuli ndio rais wetu
 
Mbeya hatutaki kuisikia CCM kabisa




wezi wa mali ya umma, watumishi wazembe, wababishaji na wale wote waliowekwa madarakani kwa bahati bahati wakati wa utawala wa mr ziro; pia kile kikosi kazi cha watu waliokosa muelekea makupe wakubwa na wanene waliowekwa madarakani na mmasai pori tunafahamu kuwa roho ziko juu na mnapumulia mkiwa ICU kwa sasa...wakati wa ukombozi ni huu mtajitambua tu.....tinga tinga litawashughulikia wote. hapa kazi tu....
 
Back
Top Bottom