Magufuli aliahidi kuboresha mafao ya Wafanyakazi. Badala yake kavuruga maslahi yao, na ametumia fedha za mafao yao kujipaisha zaidi

Acheni kulalamika sana. Kama mnaona hafai jitokezeni kwa wingi kwenye sanduku la kura mumkatae na kumchagua mtu mwingine
 
Tutafute mtawala ambae siyo muongo na awe mkweli. Uchaguzi umefika.
 
Rais anafanya mazur lkn hapo naona alijisahau anapaswa kukumbushwa na wasaidizi wake badala ya kumuimbia mapambio
Baba mwenye watoto hata uwe na maghorofa 10 lakini watoto kila siku wanakula ugali mrenda hakuna haja ya kuwa na hayo maghorofa.
 
Hakuna Mfanyakazi mwenye akili timamu kichwani mwake anaweza kumfagilia Magufuli kwa chochote kile. Mimi binafsi nikimuona tu kwenye tv, faster nabadili channel. Maana namuona hana msaada wala faida yoyote ile kwangu.

Haiwezekani niishi kwa mshahara ule ule tangu enzi za JK halafu eti mtu aniambie tuna Rais! Labda aseme tuna RAHISI! ila siyo Rais.
 
Kiuchumi ukiona watumishi mishahara haiongezeki maana yake ni kuwa hata mtaani hali ya uchumi lazima iwe mbaya,hiyo ni kanuni ya uchumi-maana matumizi makubwa ya serikali ni kupitia mishahara na miradi.
Kwa bahati mbaya kwa Tanzania Miradi yote mikubwa wakandarasai wanatoka nje hivyo mapato yake nayo yanaenda nje.kwa hiyo njia pekee ambayo hela inaweza kupatikana mtaani ni kupitia mishahara.
By the way,haya mambo yalimuondoa mbunge wetu kipenzi aliyokuwa akitetea masilahi ya watumishi mule bungeni.Upumzike rafiki wa kweli Kasuku Bilago aliyekuwa mbunge wa Kankonko.
 

Posti bora ya wakati wote hiii
 
Kama ni mpira una zako 3 points
Tatizo lipo hasa kwa waalimu hao watumishi wengine maisha yao angalau, yaani hiyo majuzi hapo Dodoma pambio na sifa kwenda kwa bw. Yule wacha wakome
 
Mateso bila chuki, utawala wa ovyo kabisa
Hali yetu wafanyakazi tulio punguzwa kazi ni ngumu kila siku yupo PSSSF lakini madai hayatolewi na tuna magonjwa nyemelezi kama kisukari, shinikizo la damu nk.sisi tumefungua madai yangu mwaka jana mwezi 12 lakini hakuna anayejali mapaka sasa tunahali ngumu ,labda hizo pesa hatatuzipata mpaka tumefika kaburini.
Majibu tunayopewa hayaridhishi kabisa,mtu unaumwa unaambiwa mpaka ufikishe umri wa kustaafu ndiyo upewe pesa yako.
 
Wazee Wastaafu wanasotea mafao yao mwaka wa 2 huu
Mifuko ukianza kudai inakuwa na visingizio mara mwajiri haijaleta michango yako miezi 3 imemiss kwahiyo ngoja tufuatilie! Kwani walikuwa wapi kufuatilia kabla ya mfafanya kazi hajaacha kazi ? Wameajiriwa kwa kazi ya kufuatilia michango ya mwanachama lakini wanasubiri uanze kudai mafao ndiyo wanakuambia tufuatilie mafao kwanza,nayo ni njia ya kuchelewesha malipo ya mwanachama
Pili wafanyakazi. wengi wa mifuko hawataki kutoa namba zao za simu wanataka kila siku wewe uende ofisini na ukifika unaambiwa neno lile lile kuwa tunashughulikia jibu ambalo lingeweza kujibiwa kwa simu
 
Acheni kulalamika sana. Kama mnaona hafai jitokezeni kwa wingi kwenye sanduku la kura mumkatae na kumchagua mtu mwingine
Eti watu proffesional hawalipi mafao yao mpaka wastaaafu ,ambapo mikataba yao imeisha na kazi hawana wasubiri tu mpaka wafikishe miaka 60 kwa sababu ni proffesional!! Watakula hiyo proffesional yao mpaka wafikishe miaka 60?
Wawape basi kazi wafanye kazi mpaka wafikishe hiyo miaka wanayotaka wao
 
Chukua hatua
 
Ni hatari Sana ,

Sana....
Masikitiko haya Ni kila Kona, kila pembe ya nchi...

Hata hivyo udhaifu wa TUCTA kwa kukubali kununuliwa ndio unaleta hata yote
 
Pole sana mkuu, hela yako lakin unapangiwa jinsi ya kuitumia, so sad
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…