Magufuli alikuwa na kibali kikafutwa! Rais ni kibali, anajitambua? Je, tumsaidie atimize matakwa ya kibali chake ili kisifutwe, au tumuachie mwenyewe?

Samia Ana kila sababu ya kuridhika na kibali alichopewa. Aliyoyafanya ni makubwa na mazuri kuliko hata mtangulizi wake.
Sasa angeandaa mrithi wake atakae kuwa tayari kuendeleza dira ya taifa 2050 aliyoindaa samia na tume zake.
 
Kaka paskali wewe n Mtu WA Kwenda mbele ya muda sana🙌🏾🙌🏾🙌🏾 kisha kurudi wakati uliopo...

Mungu akujalie mema.

Nafikiri akiitua ndoo 2025 atakuwa amefanya Bora sana ila kwakuwa kuna namna ya kuyaona mambo na kutafsiri tunatofautiana mwambieni asinogewe akizidisha inabidi awe na hekima zaidi vinginevyo aweanajua nn anatakiwa kufanya na nn asifanye.
Lasivyo haitakuwa vile inatamaniwa Bali itakuwa vile mtoa vibali anahitaji👣
 
Yes, nilipomsikia akisema kuhusu 2025 nimeshauri Kuna Kitu Rais Samia Amekisema Kuhusu Kurejea Kizimkazi “Post 2025”. Nashauri na Nasisitiza Wenye Uwezo Kusaidia, Tumsaidie Kumshauri Ukweli!
P
 
Aisee, hili somo ni zuri na litaendelea kuishi.
Naungana nawe kuwa Mh. SSH ana kibali, tena toka kwa YEYE.
Angalizo ni kwamba anapaswa kukitendea haki kibali chake, na isiwe kimazoea. Kibali kinamtaka aiponye nchi hasa kwa kuunda Katiba mpya ambayo itazuia watawala wajao kutoturudisha nyuma. Katiba ya sasa inampa mwanya mkubwa mtawala yeyote 'kupenyeza' chembe za udikiteta. JPM aligundua mwanya huo na kuutumia vilivyo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…