Magufuli aliondoa 'Service Charge' Tanesco ya 7,000 lakini Serikali ya sasa inazirudisha tozo kidogokidogo kupitia mfumo wa Luku

Magufuli aliondoa 'Service Charge' Tanesco ya 7,000 lakini Serikali ya sasa inazirudisha tozo kidogokidogo kupitia mfumo wa Luku

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Watu wengi wanaweza kuwa wamesahau, wakati Serikali ya awamu ya tano inaingia madarakani ilikuta shirika la umeme nchini(TANESCO) wanakata 7000 kila mwezi kama gharama ya kuhudumia laini. Ilikuwa pesa flani ya mtelezo kwa Serikali na shirika la umeme, 7000 ukizidisha na wateja wote wa kawaida nchini zilikuwa ni pesa nyingi sana. Watu walilalamika kiasi, pitia uzi huu wa 2012: Tujadili makato ya LUKU katika manunuzi ya Umeme (Service Charges). Changamoto ilikuwa kubwa zaidi kwa nyumba ambayo ilibaki tupu kwa muda mrefu.

Pamoja na malalamiko hayo Tanesco ilikuja na ufafanuzi huu; Maelezo kuhusu gharama za huduma "service charge" ambapo ilijitetea ni gharama za kuhudumia laini ikiwemo kukata miti, kubadili nguzo zilizooza na kadhalika.

Mungu si Athumani, April 2016 Serikali kupitia Ewura waliondoa makato ya 'Service Charge' baada ya Tanesco kupeleka maombi ya tozo hiyo kuondolewa ambayo awali waliitetea uwepo wake na hadi sasa tozo hii haikuwahi kurudi. Pia tozo ya aina hiyo iliondolewa na mamlaka ya maji ya Dawasa.

Serikali ya awamu ya sita ilipoingia madarakani March 2021, miezi mitano baadae walitambulisha tozo mpya kupitia mfumo wa umeme wa Luku na tozo hii ilikuwa ni 'Flat rate' kwa kila mita ambapo ilitakiwa kulipa 12,000 kwa mwaka ikiwa ni wastani wa 1,000 kila mwezi. Wadau walilalamika wakidai hii ni tozo kama tozo nyingine zinazotambulishwa awamu ya sita, soma: Kodi ya Jengo au Kodi ya Mita ya LUKU?

Baadae tozo hii ikaanza kubagua majengo ambapo ya ghorofa yalitakiwa kulipa zaidi ambapo kila floor ilitakiwa kulipia 60,000.

Tangu jana vilio vimeanza huku tozo hii ikiwa imeongezwa isivyojulikana, watu wameandikiwa 'debt collected' pesa nyingi na kila mtu akiwa na bei yake. Ni kama Serikali imeamua kutumia luku kukusanyia tozo yao mpya na wanairekebisha karibu kila mwaka, inapoelekea itafika/itazidi 7,000 ambayo ilikuwa inalipwa zamani na tukaipa jina la 'Service Charge' ilhali ya sasa tumeipa jina la 'kodi ya jengo'

Tozo lukuki na mikopo mingi iliyotia fora, Serikali ya awamu ya sita inapeleka wapi fedha zote hizi inazonyonya kwa wananchi wake?
 
Spika Tulia amegeuka mtetezi wa serikali na mafisadi wa awamu ya 6. Tutatetewa na nani?
 
Pesa za uchaguzi zinakusanywa kwa kila njia. Na kwanini Serikali hawatoi maelekezo kabla, wanajifanyia watakavyo kila wanapoamka.

Watanzania tuwe tunahoji, siyo tunawaacha hawa, tuwabane ili hata wakitaka kufanya ujinga, wajue moto utawaka.
 
Twafaaaaaaaaaaa! alafu Waziri wa fedha wa hii nchi ni mtu Selfish sana, sijui inakuwaje mtu kama huyu anakuwa waziri wizara nyeti.
 
Kuna watu humu watakupinga, Maana kwa mujibu wao kila alilo lifanya lilikuwa baya.Mama ndiye anaupiga mwingi ngoja tuone hadi kufika 2030 Watanganyika tutakuwa na hari gani, lakini kwa maoni yangu tutakuwa tumechoka sana.
 
watz ni watu wakuonewa na kudhurumiwa na kunyanyaswa maana bdo hatujajitambua ni vijana wachache wanaweza kusimama front na kudai haki...
 
Kila kilichojengwa na Jiwe kilipinduliwa miguu juu chini.
Nadhani alikosea kufanya 'one man show'... Alikuwa anaonekana Rais pekee na wote wote wakawa wanamuogopa Magufuli na yeye pekee ndio order zote kwake zinaanzia kwa utashi wake. Alikuwa mtu mzuri na machache mabaya lakini alisahau kuweka misingi ya utaasisi kama alivyofanya hayati Mkapa.
 
Back
Top Bottom