Magufuli alitumia kirungu na buti kuua upinzani akashindwa , Samia anatumia akili kuua upinzani. Samia atafanikiwa

Magufuli alitumia kirungu na buti kuua upinzani akashindwa , Samia anatumia akili kuua upinzani. Samia atafanikiwa

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Magufuli alikuwa na nafasi nzuri sana ya kuweza kuua upinzani lakini akatumia nguvu ndio maana yake akashindwa.
Samia kaingia kwenye mfumo katika kipindi ambacho upinzani/wapinzani wameshakuwa sugu . Kipindi ambacho wapinzani waliishiwa hofu
Katumia akili kidogo tu anakaribia kuummaliza upinzani.
Niko pale nimeetulia nasubiri enzi za ujamaa zirudi . Ila hofu yangu je, huo utakuwa ujamaa wa kweli au ujanja ujanja?
 
InShot_20240213_142054441.jpg
 
Unadhani upinzani ni kuvaa Gwanda au Gamba ?

Upinzani ni pale ambapo mambo hayaendi na watu wanaona wanakuwa short changed.., kwahio kinachotokea ni kuhahirisha tatizo sababu watu hawa walafi kwa faida ya leo wanafanya kesho yetu kama taifa kuwa ngumu maradufu... (Tatizo Vyama vyote vimekuwa platform za watu kupata Kura ili waende Kula) ila mwisho wa siku kitaa watu wakipigika hili Janga wanalochuma hawa walafi wachache watatugawia na sisi watazamaji ili tuweze kula nao..., Sad Times Indeed...

 
Upinzani hauwezi kufa kamwe, maana upo kwenye akili na mioyo ya wanadamu. Vitakufa hivyo vyama tu vya siasa na waanzilishi wake. Ila siyo upinzani.

Kumbuka tu binadamu wote hatuwezi kuwa na mtazamo unaofanana! Na hiyo tofauti inayojitokeza kwenye mitazamo yetu, ndiyo upinzani wenyewe huo. Hivyo usishangae kuona hata Rais na Mwenyekiti wa chama tawala akipingwa na baadhi ya wanachama wenzake au wasaidizi wake ndani ya chama/serikali anayo iongoza!! Kwa sababu hiyo ni hulka ya binadamu wote.
 
Back
Top Bottom