Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,984
- 19,288
Wakuu, kwema
Kama mnavojua kuna inflation kubwa kila nchi duniani nimeweka screenshot chache kuonyesha hilo.
Sasa watu wasioelewa wanasema inflation imesababishwa na Samia na Magufuli angekuwepo bidhaa zingekuwa chini sana
Kanuni ya msingi kabisa kwenye uchumi ni kuwa bei za vitu zinakuwa determined na demand vs supply au uhitaji vs upatikanaji.
So uhitaji wa bidhaa fulani ukiwa mkubwa ila upatikanaji wake ukawa mdogo lazima hiyo bidhaa itapanda tu bei hata rais angekuwa nani
Mfano mavuno ya mahindi mwaka huu yamekuwa kidogo kutokana na ukame lakini uhitaji wa mahindi ni mkubwa, so matokeo yake lazima ni bei ya mahindi kupanda, simple as that
Sasa hebu tuangalie historia ya Magufuli katika ku deal na matatizo ya kiuchumi yalivyokuwa na tutajua kama angeleta unafuu katika hali ya sasa au ndio angeogeza balaa
Sakata la sukari: Kama mnavyokumbuka mwaka 2016 Magufuli kwa papara alipiga marufuku sukari kutoka nje ya nchi, matokeo yake ni sukari kuwa adimu hence bei yake kupanda, ila cha ajabu kwa uelewa mdogo wa Magufuli, alianza kusema wafanyabishara ndio wanafanya hujuma kupandisha sukari na akaagiza sukari kusakwa na jeshi, matokeo yake sukari ikapanda zaidi.
Sakata la korosho: Kuna muda korosho zilinunuliwa kwa bei nzuri sana huko Mtwara, watu wakafaidi, hii ni kwa sababu bei katika soko la dunia ilikuwa nzuri, so hata wafanyabishara watanunua kwa bei nzuri kutoka kwa wakulima, ila misimu uliofuata bei ikashuka, kwenye soko la dunia, so hata wafanyabishara nao wakatoa bei ndogo huku, Magufuli kwa akili zake pia akasema ni wafanyabishara wanamhujumu, akaagiza jeshi kununua korosho wazibangue hata kwa mabomu, matokeo yake ni korosho zile zilishindikana kubanguliwa na zikawa zinaozea kwenye maghala na watu wengi waliporwa korosho zao bila kulipwa.
Sasa kwa mifano hiyo michache tu inaonyesha jinsi gani Magufuli alivyokuwa akifanya vitu kwa impulse, (kwa hasira bila kufikiri)
huyo mtu angekuwa rais kipindi hiki ambacho dunia ina struggle na inflation unajua angefanya situation kuwa mbaya zaidi, pengine angeagiza jeshi lifanye biashara ya mafuta ili yashuke bei.