Elections 2015 Magufuli ataja mafisadi CCM

Elections 2015 Magufuli ataja mafisadi CCM

Akizungumza kwa nyakati tofauti katika mikutano ya kampeni ya chama chake mjini Kisarawe, Pwani na baadaye Ukonga, jijini Dar es Salaam jana, Magufuli alikiri kuwa chama chake kiliwalea walarushwa na mafisadi kwa muda mrefu na ndiyo maana baadhi ya watu walianza kukichukia.
Anakwepa tu lakini anajua fika kwamba pamoja na mambo mengine hayo zile nyumba za serikali walizogawana (chini ya usimamizi wake) ni kati ya mambo makubwa yanayowafanya watu waichukie ccm.
 
neenda kumuulize sumaye atakujibu vizuri madai yako.

Amemtaja Jinga Kubwa?..Hiyo ni mbinu tu kama hizi zifuatazo!! Hakika mwaka huu ni wa “Mabadiliko” maana CCM wametumia na bado watatumia mbinu nyiingi bila Kufanikiwa kuyazuia Mabadiliko!!Mfano;
1. Wamenunua vyombo vya habari kama Magazeti,Vituo vya Redio na Runinga na Blogs lakini wapi!!
2. Wamenunua Viongozi Waandamizi wa vyama vya Upinzani kudhoofisha Mabadiliko lakini wapi!!
3. Wamenunua Wasanii wa Maigizo,Wanamichezo na Wanamuziki wa Kizazi Kipya kuwavuta vijana lakini wapi!!
4. Wametoa vitisho kwa watu wanaopenda mabadiliko vijana na wakina mama lakini wapi!!
5. Wamepenyeza watu kudhoofisha upinzani katika vyama na kwa Wanaharakati lakini hollaa!!
6. Wamejaribu kuzusha tuhuma mbalimbali kwa Viongozi wa “Mabadiliko” lakini wapiii!!
7. Wametumia vyombo vya dola kuzima “Mabadiliko” kwa kuwakamata na kuwasweka ndani na kuwafungulia kesi zisizokuwa na kichwa wala miguu wana Mabadiliko lakini wapiiiii!!
8. Wameunda Kamati ya watu 32 maalumu kwa ajili ya kuporomosha matusi na kuzusha tuhuma za ufisadi kwa Lowassa na wana “Mabadiliko” Lakini wapiiii!!
9. Waliapa kutokutumia Helkopta katika Uchaguzi wa Mwaka huu kwa kusingizio wanataka kupita kila kata kwa wapiga kura lakini wapiiii!!
10. Wameandaa tafiti feki za Twawezwa na Ipsos kuwalaghai wana “Mabadiliko” lakini wapi!!
11. Wametumia Mamilioni kuwalaghai watumishi wa Umma kama Polisi waliowatelekeza siku nyingi kwa kuwapa posho nono na ahadi lukuki lakini wapiiii!!
12. Wamejaribu kuwalaghai walimu ambao waliwasahau miaka nenda rudi na sasa wameahidi kuwalipa baadhi ya madai yao lakini wapiii!!
13. Wamejaribu kutoa kuwaondoa baadhi ya Watumishi wa idara Muhimu zinazohusika na uchaguzi ili kujenga hofu na kuandaa mipango miovu lakini wapi!!
14. Wamejaribu kuwatumia Vingozi wastaafu kuomba Huruma kwa Wananchi waliowaacha katika Umaskini mkubwa,maradhi na ujinga huku wakiwakejeli lakini wapiiii!!
15. Wamejaribu kuwazuia Wapinzani kutumia Viwanja vyao na Sehemu mbalimbali kwa ajili ya Kampeni lakini wapiiii!!
16. Wamejaribu kutumia ulaghai wa kuwavalisha wafuasi wao mavazi ya Upinzani ili wawakatate Viongozi wa Upinzani eti kuonesha kumeguka kwa Upinzani lakini wapi!!
17. Wamejaribu kupanga njama za kuwadhuru Viongozi wa Upinzani kwa namna mbalimbali lakini wapiii?
18. Wamejaribu kutumia Matamasha,Makongamano,Mikutano,Semina,Maandamano,Mikusanyiko,Matamko,na Warsha mbalimbali kubadili hisia za Wananchi dhidi ya Mabadiliko lakini wapiiiiiiiiiiiiiii!!!
19. Wamejaribu kupanga Mapinduzi hewa ya Kuwapindua Viongozi wa Upinzani kuonesha kumeguka kwa Umoja wa UKAWA lakini wapiii!!
20. Wamejaribu kupiga push ups,kuongea lugha za makabila mbalimbali,kucheza rhumba,kuandaa fiesta na Kufunga milango watu wasiondoke Viwanjani baada ya Fiesa lakini waaapi!!
21. Wamejaribu kusomba watu kwa malori,pikipiki,bajaji,Mabasi kutoka Mkutano mmoja hadi mwingie kujaza mikutano kuwahadaa wana “Mabadiliko”Lakini waaapi!!!
22. Kuzuia post za Ki “Mabadiliko” katika Mitandao ya Kijamiii kama JF,FB,Twitter, na Kuwa Block wanao post Mabadiliko ..Lakini wapiiii!!
23. Wamejaribu kuwashinikiza waajiri kuwafukuza Wafanyakazi wao wanaopenda Mabadiliko ili kuwatisha wengineo Lakini waapiii!!
24. Wamejaribu kurusha ndege za Kivita ili kuwatisha wananchi dhidi ya Mabadiliko pamoja na kuonesha Picha za Machafuko katika nchi mbalimbali na kufananisha Mabadiliko na Kuwait NA Iraq lakini waaapiiii!!!!
25. Wanajaribu kutengeneza “Goli la Mkono” kwa takwimu za wapiga kura na kuzuia Wapinzani kuhakiki taarifa sahihi za Vifaa na Daftari kwa wakati lakini wapiiiiii!!
26. Wamejaribu kuzindua Miradi iliyokwisha zinduliwa zamani pamoja na Miradi hewa ama ambayo hata haijaanza kuwarubuni wananchi lakini wapi!!!!
27. Na bado ndani ya siku zilizobakia watakuja na mbinu mbalimbali tena huenda zikawa ni mbaya zaidi na zenye dalili ya uvunjifu wa AMANI na UTULIVU wa Nchi ili mradi wazuie “Mabadiliko” ninaamini kwa Msaada wa MUNGU watashindwa na kulegea!!!!
Mimi nitampigia kura yangu ya thamani “EDWARD NGOYAI LOWASSA” pamoja na “Diwani na “Mbunge” wa UKAWA!!..Kwa maisha bora ya kwako nay a Kizazi chako Ondoa CCM,kwani imeishiwa pumzi!!!! “ALUTA Continua, Victoria Ascerta”.... “The Struggle Continues, Victory is Certain”; ...Mapambano yanaendelea, Ushindi unakuja!!
 
Alisema ataongoza nchi kwa kufuata ushauri wa ma raisi waliopita, sasa ikitokea anataka kumgusa fisadi 'X' bila shaka atashauri aache mara moja, kwani kumgusa fisadi X kunaweza kuleta matokeo hasi, na huo ndio utakua mwisho wake wa kupambana na mafisadi ndani ya CCM.

Kwa kifupi hiyo ndio athari ya 'system'

Tarehe 25 usifanye makosa, #Chagua_Lowassa
 
Ccm hawana jipya. Huyo makufuli kama ana nia ya kweli ya kupambana na mafisadi, atoroke aje
 
1. Ufisadi wa CCM ni mfumo; naweza kutamka hapa authoritatively kwamba John Magufuli hana ubavu wala mbinu za kuubadilisha hata chembe! kwa sababu CCM kuna watu wenye chama chao; na kwa bahati mbaya Magufuli sio mmoja wao!!

2. Magufuli hana ushawishi wowote wa maana ndani ya CCM; amelelewa kwenye periphery ya chama sio M-CCM kindakindaki kama walivyo kina Kikwete na Lowassa; Option aliyonayo Magufuli ni kutumia madaraka ya Urais na ubabe; ambao sio mbinu salama kwake kwa sababu watagang up na kumgeuka ajikute anaingia majanga kama yaliyomkuta Thabo Mbeki kule Afrika Kusini - RECALL!!

3: Mkakati wa kubadilisha katiba ya CCM uko katika advanced stages ili kutenganisha kofia ya Mwenyekiti wa chama na Rais wa Jamhuri; na mkakati huo ni mahsusi kumdhibiti Magufuli kutokana na kiinachoitwa HULKA YAKE YA UBABE; hilo likikamilika Magufuli hataweza kufurukuta na Urais wake, brakes kulia na kushoto juu na chini!! atakuwa frustrated na kuanza kutumia state power (mamlaka ya Urais na vyombo vya dola) to reign them in; kwa maana ya kuwadhibiti which is a perfect recipe for total anarchy ndani ya chama ambayo for obvious reasons therefore NJI nzima!!

Hata hivyo tusubiri tuone!!!!!!!
 
kuwataja hawezi, itakua kuwashughulikia...!!? naa hio mahakama ataianzsha yeye , ....!!?

porojo zimefka mwisho sasa...

pole kama bado unadanyka hadi sasa
 
Fisadi moja limekimbilia chadema.linaitwa Edward ngoyai Lowassa.akiingia tu huyu ndio wa kuanza nae.
 
Sasa kabla hajaenda ikulu na ndoto yake hiyo ya mchana anitajie hao mafisadi atakao washughulikia ni kina Nani ??? Akitaja tu kura yangu nampa kiroho safi ,asituletee hadithi za Jakaya na majina ya wauza unga toka anaingia Ikulu mpaka anaondoka hata jina la teja hajataja
 
1. Ufisadi wa CCM ni mfumo; naweza kutamka hapa authoritatively kwamba John Magufuli hana ubavu wala mbinu za kuubadilisha hata chembe! kwa sababu CCM kuna watu wenye chama chao; na kwa bahati mbaya Magufuli sio mmoja wao!!

2. Magufuli hana ushawishi wowote wa maana ndani ya CCM; amelelewa kwenye periphery ya chama sio M-CCM kindakindaki kama walivyo kina Kikwete na Lowassa; Option aliyonayo Magufuli ni kutumia madaraka ya Urais na ubabe; ambao sio mbinu salama kwake kwa sababu watagang up na kumgeuka ajikute anaingia majanga kama yaliyomkuta Thabo Mbeki kule Afrika Kusini - RECALL!!

3: Mkakati wa kubadilisha katiba ya CCM uko katika advanced stages ili kutenganisha kofia ya Mwenyekiti wa chama na Rais wa Jamhuri; na mkakati huo ni mahsusi kumdhibiti Magufuli kutokana na kiinachoitwa HULKA YAKE YA UBABE; hilo likikamilika Magufuli hataweza kufurukuta na Urais wake, brakes kulia na kushoto juu na chini!! atakuwa frustrated na kuanza kutumia state power (mamlaka ya Urais na vyombo vya dola) to reign them in; kwa maana ya kuwadhibiti which is a perfect recipe for total anarchy ndani ya chama ambayo for obvious reasons therefore NJI nzima!!

Hata hivyo tusubiri tuone!!!!!!!
Mkuu nimecheka sana , huyu bwana ni mkwara wa mdomoni tu si juxijuzi
 
  • Thanks
Reactions: MTK

Mkuu nimecheka sana , huyu bwana ni mkwara wa mdomoni tu si juzijuzi alitamka wazi kuwa anawaogapa mafisa katika mktano wa hadhara huko lindi.
 
Haaaa haaa hii nchi ina viongozi waoga balaa yaani kutaja tu majina ya wezi utadhani unapunguza au kuongeza neno kwenye biblia au quraan.
Asijichoshe akifika afanye ivi:
1.Ampandishe Diamond amwage miuno dakika 20
2.Apige push up 30 na kupumzika dakika 20
3.Asalimie kwa lugha mbalimbali kama kawaida dakika 20
4.Ahadi mbalimbali kama kufufua viwanda na bahari ya Hindi kupelekwa Iringa dakika 30
5.Kucheza na kuimba alinselema dakika 20
6.Apeane mikono na wasanii dakika 10 siku itakua imehesabiwa
Hili balaa la mafisadi haliwezi tena kasema wazi wapo uko chamani kwake yeye avunge tu maana majoka yenye makengeza yakiamka hizi siku chache zitakua nyingi.
 
Watu hawajagundua kuwa KASUKU ni mad!I wonder why..
 
fisadi mkuu ndie aliyemteua makufuli kwenye kikao cha fisiemu:lying::teeth::teeth::teeth:
 
Hawezi; hii TOUGH TALK anayofanya kwenye majukwaa ya kampeni ni ya Kutongozea tu kama alivyosema majuzi Balozi Getrude Mongela kwenye mdahalo wa Amani blue pearl Ubungo Plaza;

Mkuu nimecheka sana , huyu bwana ni mkwara wa mdomoni tu si juzijuzi alitamka wazi kuwa anawaogapa mafisa katika mktano wa hadhara huko lindi.
 
Hatudanganyiki tena hata mwenzake wakati anaomba kura zetu alisema ana majina ya wauza madawa ya kulevya hadi leo anatoka hajayaweka hadharani sasa atataka kutuambia nini watu tunataka mabadiliko sio propaganda:
 
Ni vizuri ametambua kuwa CCM IMELEA MAFISADI kwa muda mrefu.pia angeeleza atawasaidiaje wananchi walioathirika na ufisadi huo.Wapo watu wamepoteza maisha kwa kukosa tiba baada ya fedha ambazo zingenunulia dawa kuporwa na mafidadi wa ccm,wapo waliokosa elimu bora,ajira nk je tuifanye nini ccm?vibaka wazoefu bado wapo ccm na katibu mkuu anskiri hilo je kwa nini hamuwashughulikii?wale wa ESCROW bado mnawalea na kuwakumbatia ,je hiyo nia thabiti ya kupambana na mafisadi ni ipi?
 
Nawapeni pole sana wanaosema Edo ni fisadi

Kwan kama angekua fisad asingestahili kuchukua form wangwmwekea pingamiz na kama Kweli Edo ni fisadi Kweli magufuli hana uwezo wakushughulikia mafisad kwan angeanza na Edo ambaye wanamtaja tena amekua karibu sana naye yaan ni mgombea mwenzake kiti sawa hivyo

Tumechoka propaganda zenu ccm
 
Back
Top Bottom