Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Nadhani kuna jambo halipo sawa. Maana naona hapo ewura ndio walitakiwa kupeleka research zao kwa waziri na kuonesha kwann wamekubali 8% na sio 18% . Au nchi hii hawaruhusiwi kutoa mapendekezo?? Maana ewura ndio katangaza ongezeko toka kwenye mapendekezo ya Tanesco
 
Nilitegemea Prof Muhongo atumbuliwe kwanza kisha wafuate wa chini yake.


Naona jamaa katolewa kafara
Hamna cha kafara wala nini...tulimpinga sana huyu mkurugenzi na EWURA juu ya kupandisha bei hawakusikia
 
..duh!

..tra alifukuza bodi akamuacha mkurugenzi mkuu.

..tanesco amefukuzwa mkurugenzi mkuu bodi ya wakurugenzi imeachwa.

..sasa tukisema nchi inaendeshwa kwa mihemko tutakuwa tumekosea?

..halafu anakwenda kuyazungumzia mambo haya
KANISANI!!

Yani akifuka Tanesco mkurugenzi
Lazima na TRA afukuze Mkurugenzi!!!
JokaKuu punguzeni Chuki
Haziwasaidii zaidi yakuumiza Nafsi yenu.
Kama Rais ndio huyo

Habadiliki kamwe
Mlie mtaka hakuwa
 
Ina maana kosa ni kuiomba EWURA kupandisha umeme?! Walisubiri EWURA wakubali ombi ndipo wamfukuze?! Sawa! Lakini Bukoba tunataka kusikia juu ya rambi rambi tu zilizoliwa na si habari ya Mramba. Ajenda za uchaguzi wa madiwani zinakosekana naamini mtawafukuza wengi mpaka ifikapo january 22.
 
Ndio maana tunasema kabla ya kufukuzwa bosi wa tanesco, bosi wa ewura anafanya nini hadi sasa?
Pia kumbuka hawa wametoa maombi tu, na ombi linaweza kukataliwa kwann haikufanyika hilo?
 
Dah Magufuli kumteua Mwinuka sijui kawaza nini? Kati ya sehemu ambazo hutakiwi kufanya majaribio ni Tanesco.. Kama ni kutafuta mtu pale UDSM basi Prof. Kimambo alikuwa anaweza sanaaa ila siyo Mwinuka!! Ila sasa ndo hivyo tena Kimambo anapitia Chalinze Mzee na huwa anakula pale Mombo.. humo hataki hata kuwasikia lakini Kimambo ni bonge la mbunifu!!
 
Huyu alikuwa mmoja wa watu waadilifu kwenye hii nchi. Na uchafu wa wakina muhongo nashangaa hawa watendaji wanawezaje kufanya kazi
Uko kinyume mkuu,hebu tujaribu kuunganisha hizi dots.
1. Sos alijiuzulu katika awamu ya nne,lakin ya tano akarudishwa wizara hiyo hiyo,,,kwanini???
2.JPM alilia sana mikataba ya tanesco,lakin ikawa ngumu kuivunja,,,wakati huo huo Mramba yupo wizarani,kwanini????
3.Ewura ilitangaza kupandisha gharama kwa 8.5%,,,SOS akakanusha haraka sana,,,kwanini???
4.Mramba katumbuliwa haraka sana,,,kwanini????

Mawazo yangu;
-Sos,alirudishwa wizarani kwa kaz maalum.
-Mramba alikuwa anavutiwa muda tuu.
-Tanesco inatakiwa kufa ili mikataba yake mibovu na wakina richmond ife.
 
Majibu mazuri sana, yafungulie thread mpya then waambie mods wasiifute au kuiunganisha na thread nyinginezo.
Na Title iandike kwa herufi kubwa ili wadau wa JamiiForums waione kirahisi.
 
Kwa lugha hii basi amelipiza kisasi kwa mramba maana hiyo ishu ya bonus tanesco walinyanganya na baadae wafanyakazi kwa kushirikiana na TUICO walipigania hiyo bomus kwasababu ipo kisheria. Kwa maelezo hayo bus mimi naona ni matazam finyu sana kwasabau analipwa, na bunus ni shilingi ngapi kwenye upanuzi wa miundo mbinu ya TANESCO
 
Kosa ndio hilo LA umeme watupishe na serikal yetu,huu sio wakati wa kuumiza wananchi.GOOD ENOUGH MY PRESIDA
 
Ili tuendelee tunahitaji watu,ardhi,siasa safi,uongozi bora na kutumbua
 
Hujitambui were
Ajenge yeye fundi!!?

Mmeishiwa hoja
Huyu ndiye Rais wakweli
Huwa siwezi kumwelimisha mtu mwenye upeo mdogo wa kufikiri kama wewe siku nyingine usiwe unajipendekeza unarept coment zangu.
 
Mkuu wawekezaji wa kitapeli kama IPTL hata wazime mitambo yao hakuna shida maana wanatuibia fedha zetu nyingi kwa mikataba wao wa kitapel
 
Ila mbona jamaaa namuonaga anapiga kaz kisomi sana mramba ...ila duh hizi drama ...
Na wa ewura nae mbona kaachwa
Kisomi vipi mkuu fafanua basi kiduchu.

Unapandisha bei ya umeme kwa wananchi bila kumwambi rais wala makamu wake unategemea nini.

Huyu jamaa alishageuza Tanesco mali yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…