Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Naona kaamua kuweka Mhaya ila kwa dkt. Mwinuka ndo kachemsha moja kwa moja!! Namfahamu Mwinuka tena sana.
Haahaa sasa hayo mapungufu uyajuyo ndio yataifaa lile shirika maana itakuwa rahisi kutii bila kuuliza.
 
Mungu mwema. Nami nimesikia alikuwa anatafuta gepu kitambo!
 
ingekuwa wanajiendesha kwa faida na hawapandishi bei ovyo. tusingelalamika..

kwanza wajiendeshe kwa faida kwa kufanya kazi kwa spidi.... ndio wapate bonus.

mtu haperform na bado unampa unit 700 huko ni kulea ujinga..

nitajie shirika popote linalogawa bonus huku linajiendesha kwa hasara
Wanatakiwa pia waweke daraja la watumiaji ambao hawazidi unit 500 huwezi kumfananisha mtumiaji wa nyumbani na mwenye kiwanda huu ni upofu. Nashauri hata boss wa ewura apumzike. Yaani ukitoka ile tariff ya chini kabisa inafuata watumiaji wa kati hadi 7500units. Kwanini kusiwe na rate za majumbani hadi 500units???
 
Yeye badala ya kuanza kujenga viwanda kila siku anatengua na kuteua tumeshamaliza mwaka mmoja tayari. Washauri wa raisi wana kazi gani?
Hujitambui were
Ajenge yeye fundi!!?

Mmeishiwa hoja
Huyu ndiye Rais wakweli
 
Lecturers wataisha vyuoni kwa speed hii. Tuna under utilize elimu zao kuwapa management posts badala ya kuacha wafundishe maelfu ya wa TZ
 
Watumishi wa umma si mmwachie ofisi zake afanye mwenyewe? Hii ni kuviziana haiwezekani uniambie Waziri mwenye dhamana alikuwa hayajui haya.
Unatafuta umaarufu kwa umma kwa kuwadhalilisha watu hii haikubaliki.
 
Oyoooooooooooo! hatimae Fel Mramba ameuanza mwaka 2017 vibaya!
 
Leo 1.1.2017 Prof. Muhongo amehojiwa na Radio One na kueleza sababu za kusitisha mpango wa EWURA wa kupandisha bei ya Umeme kwa 8.5% kama ifuatavyo: -
1. Kwenye mikutano ya 'public hearing' nchini kote wadau walipinga myongeza ya bei;
2. hadi jana 31.12.2017 EWURA, kinyume na matakwa ya sheria, haikuwa imepeleka ripoti ya uamuzi wake kwa waziri mwenye dhamana, kujadiliwa na kupitishwa/kuthibitishwa kabla ya kutangazwa kwa pendekezo la bei mpya;
3. Ufumbuzi wa matatizo ya kifedha (madeni) wa TANESCO hauwezi utatuliwa kwa kupandisha bei ya Umeme. TANESCO inatakiwa kuwa na mkakati wa ku-improve efficiency kwenye management yake badala ya kuongeza bei ya Umeme; na
4. Wakuu wa TANESCO hawawpaswi kulipana bonus kila mwisho wa mwaka kiasi cha kufikia Tzs. 60m/- kwa mtu mmoja wakati shirika linashindwa kujiendesha isipokuwa kwa kupandisha bei ya Umeme. Hii inamaanisha kuwa wananchi wakamuliwe ili ipatikane pesa ya mabosi wa TANESCO kulipana bonus! Prof. Muhongo amesema ameagiza hata hiyo bonus isilipwe au irudishwe kwa waliokwisha kulipwa.
 
Jamaa si angesubiri angalau hata kesho au tarehe tatu ndio atumbue? Shikamoo Rais wangu Magufuli
 
safi sana rais wangu tumbua hao hawana huruma na watanzania halisi,tutaheshimiana tu.
 
Back
Top Bottom