Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Kumekua na Wimbi la Kuteua Wahadhiri ambao hawajawahi hata kukaa Ofisini zaidi ya Kuzoea Ku deal na Coursework za wanafunzi hivi kwa mfano Utumbuzi wa Lawrence Mafuru pale Wizara ya Fedha alikosekana mtu kweli hadi wakaenda kumchukua Lecture wa Economics UDSM?

Mwele Malecela ametumbuliwa hivi karibuni katika kitui cha Utafiti wa Tiba na Magonjwa cha Ajabu hajapelekwa pale Daktari Wa binanadamu amepelekwa mtu aliyebobea kwenye Fisheries!

Leo hii ametumbuliwa ndugu Engineer Mramba hivi hata pale TANESCO walimkosa mtu wa kushika nafasi hiyo sizijui sana mpangilio/hirachy za vyeo pale Tanesco lakini Hata Regional Managers wanaweza kushika nafasi hiyo tofauti na aliyetoka kushika chako moja kwa moja.
 
Pendekezo ni kosa? Kupendekeza! Si unamkatalia!

Amesema hakumshirikisha yeye wala makamu wake wala kiranja Mkuu wala waziri wa Wizara husikia.

Ila ujumbe ni kwamba hawakumshirikisha yeye si unajua tena Mkuu nchi hii kwa sasa yeye ndo kila kitu.
 
ingekuwa wanajiendesha kwa faida na hawapandishi bei ovyo. tusingelalamika..

kwanza wajiendeshe kwa faida kwa kufanya kazi kwa spidi.... ndio wapate bonus.

mtu haperform na bado unampa unit 700 huko ni kulea ujinga..

nitajie shirika popote linalogawa bonus huku linajiendesha kwa hasara

huo ni wivu wa kike, hizo unit 700 ukute hata yeye huo utaratibu aliukuta.
 
Hii tabia ya kuteua wahadhiri wa vyuo vikuu inaathiri vyuo vyetu. Bahati mbaya, si kila mhadhiri anafaa kuwa msimamizi wa shirika la umma. Sitasema zaidi. Tusubiri tuone.
 
Subiri wewe unateuliwa kuchukua nafasi ya Ngalamgosi na kwa vile we we sio Mhadhiri, mambo yata balance!
 
Kuna swali nimejiuliza, nikakosa jibu. Labda nisaidiwe, hivi hili suala kwa nini halikuzuiliwa ktk hatua za awali? Hivi kwa nini TANESCO hawatafuti wateja, ila wanataka watafutwe? Kwa wenye majibu, tafadhali
 
Bado huyu wa EWURA

Huyu anatakiwa atumbuliwe kabisa waache kula pesa za mafisadi na kuja kusingizia professional...........

Sasa hivi kuna gesi inazalishwap umeme,Tanesco wamefunga Luku karibu kwa watumia 75% sasa hasara inatoka wapi?.........

Wakati mtu akitaka kuunganishiwa umeme ananunua nguzo,vifaa vyote kama mita ananunua sasa hizo garama zinatoka wapi?......

Mchawi ni Tanesco wenyewe waliokubali kuingiza siasa kwenye professional yao kusaini mikataba mibovu kama kuwalipa watu Milioni 400 kwa siku...........

Huyu mkurugenzi huwezi sema hana maslahi wakati umeme ukipanda na tozo yao kama EWURA inapanda pia....

Hawa ndio walisababisha mafuta ya taa yapande bila sababu eti uchakachuaji...

Uchakachuaji unathibitiwa kwa kupandishwa mafuta ya taa?.......

Halafu kichekesho pesa wanayokusanya yote kwenye mafuta,umeme maji ni pesa ya kugawana tu kula kwenye vikao,posho na kuandaa press kwa ajili ya kutoa matamko......

Huyu anatumwa na wezi na wanyonyaji wenye kampuni za kufua umeme tuwe wa kweli hapa Rais kuchukua hatua wala siwezi shangaa............

Haya ndio majipu........

hahahaaaaa hatar
 
Yani hii nchi bana, wakati yuko na zile sarakasi za kuandaa mapendekezo jamaa ana mchora tu, wala hakumzui..

toba! kaingia 18 mtumeeee!!!
Ha ha haaa, eti anamchora tu. Ndo hivyo mkuu saiv kama ww ni mtumishi wa serikali/umma jiandae sawasawa.
 
kWELI BANA, MANAKE ATAKAYEMTEUA LAZIMA ATATOKA UDSM NA ATAKUWA MHADHIRI, MARK MY WORDS
Lazima ateue anaowajua. Kwa miaka aliyokuwa UDSM 1983......wengi aliowaacha sasa hivi ni maprofesa
 
Hii ndio tanzania ya Magufuli maskini Felchesm Mramba ulichovuna nenda katumbue na ww
 
Nadhani hii ni kweli kwa upande mwingine lakini Dr Tito nadhani alipofikia alikua msimamizi yaani mkuu wa idara mechanical and industrial engineering bado alikuwa anahitajika sana kitivoni na UDSM kwa ujumla.
Anaweza kuiua UDSM bila ya mwenyew kujijua. Maana wahadhiri wote wanapelekwa kwenye siasa chuo kinabaki na makapi tu. Suala la human resource planning kwa UDSM linapwaya sasa.
 
Hapa sasa kitovu cha wizi wa Tanesco kimekatwa.
Wale washirika wana haha kweli kweli.

Najaribu kuisoma akili ya Mhongo,naona kitu,,,ikiwa mikataba ya tanesco na Richmond haivunjiki,basi ni bora Tanesco ife na serikali kuanzisha shirika jipya Tanzania.
 
Hii inamaanisha kwamba kuna watanzania wengi wenye uwezo wa kulitumikia Taifa! Hivyo ukipata nafasi itumie kwa manufaa ya wengi!
 
Back
Top Bottom