Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Hapana jamani Mramba amezidi kiburi hakujali hata wakubwa wake.Inakuwaje anajiamulia maamuzi makubwa bila kutaka ushauri hata kwa Waziri? Anajiona bado yuko awamu ya NNE.Kheri ya mwaka mpya Mramba umetusumbua sana weeeee.
 
Kwa kweli huyu Dr.Mwinuka aliyeteuliwa anastahili cheo hicho,kwa wanaomfahamu huyu jamaa ni mchapakazi hatari mwenye hofu ya Mungu
Sasa hawa wahadhiri mbona wanaisha pale UDSM😵😵😵
 
Kama sijakosea na km nimekosea niwiwe radhi bure Rais alisema "kama hujui kitu cha kufanya uliza" Hii kauli ndio inayowatumbua wengi. Na pia nafikiri wale waliopewa mamlaka ktk vitengo au wizara fulani hawajajua nini maono ya Rais maguful. Jambo usilolijua nisawa na usiku wa giza hata km utaonekana unaenda wale wanaojua hiyo njia watajua kuwa haujui kutokana na mwendo wako,utakuwa wa mashaka ingawa unaonekana unaenda. Maguful anajua ni wapi anataka kuipeleka hii nchi,ndie mbeba maono. Ishu wengine hawajajua tunakopelekwa kwakuwa tulizoea mfumo fulani wakila mtu kuwa na maono yake. Hii ndio shida. Mm aijamchaagua ila ni raisi wangu na inanibidi nikubaliane nae tena hata km sikutaka kumuombea ninamuombea sasa kwakuwa aliomba tumuombee. Tusubiri tuone tunakoelekea na ninyi viongozi si kila jambo mnatutwisha sisi wananchi mzigo. Leo hii kila mtu analia maisha magumu sheleli haionekani,matokeo yake mnatuongezea 8 asilimia ya umeme. Hamna hata aibu kweli au kwasababu mko kwenye vitengo? Wale wa vijijini wanaotegemea zao moja la msimu wafanyeje? Mvua yenyewe imegoma,mnaongeza bei ya umeme!! Ni shida. Nampongeza Rais na Mungu amlinde. Tulikuwa tumepotea njia saana ,sasa tutajua km tuendako ndionau siko,ila magufuli km dreva anajua anakoenda,tukifika atashika brek tu.
Hii INA maana moja tu ktk nchi hii anae jua ni yeye tu! Wengine wote hawajui wanapaswa kumuuliza kwa kila kitu. Yeye ndie msaafu wa nini kifanyike
 
Magu, umebakiwa na kazi moja tu katika tumbua jipu...
Sasa ifuate zamu ya mkurugenzi mkuu wa DAWASCO.. Inahitajika damu mpya pale ili shirika liweze kusonga mbele...
Tanesco bado sana hichi ni kiharara tu kakiminya
 
Wivu na hasira zilizochanganyikana na umaskini hizi

wapate faida kwanza ndio wajipe umeme bure...

ila kupandisha mabei ovyo ndio source ya kutumbuliwa...

nitajie kampuni au shirika lolote duniani linalogawa huduma bure kipindi ambapo linapata hasara...

only in tanzania
 
Anaiachaje bodi ya Tanesco sasa?anaacha kuzuia mabillion yanayolipwa kwa IPTL kila leo kwa jasho la kodi yetu anaenda kumuondoa mramba?

Kuendesha nchi kwa ubaguz wa udini na ukabila hakuna mwisho mwema

..duh!

..tra alifukuza bodi akamuacha mkurugenzi mkuu.

..tanesco amefukuzwa mkurugenzi mkuu bodi ya wakurugenzi imeachwa.

..sasa tukisema nchi inaendeshwa kwa mihemko tutakuwa tumekosea?

..halafu anakwenda kuyazungumzia mambo haya
KANISANI!!
 
ingekuwa wanajiendesha kwa faida na hawapandishi bei ovyo. tusingelalamika..

kwanza wajiendeshe kwa faida kwa kufanya kazi kwa spidi.... ndio wapate bonus.

mtu haperform na bado unampa unit 700 huko ni kulea ujinga..

nitajie shirika popote linalogawa bonus huku linajiendesha kwa hasara
tatizo sio hizo unit 700 kwani hata zikipigwa panga kama hakuna mfumo mzuri bado shirika hasara...
 
Naunga mkono Mramba kutumbuliwa...

kosa lake ni kukosa ubunifu, yaan kila wakijisikia tu ni kuongeza Bei ya umeme kwa wananchi? hamna ubunifu mwingine tofauti na kuongeza gharama kwa wananchi?

Kwa nini wasipunguze zile offer za Units kwa wafanyakazi wao? au wazifute kabisa hizo offer...! haiwezekani wafanyakazi takribani zaidi ya mia 500 tuwalipie gharama za umeme afu wao wanapikia majiko ya Umeme kila siku, sisi tunajibana na mkaa au gas wao tuwalipie!! haiwezekani...
Mkuu ongezea .....pia wana mishahara mikubwa plus marupurupu kibao na mianya ya rushwa ya nguvu
 
Kumekua na Wimbi la Kuteua Wahadhiri ambao hawajawahi hata kukaa Ofisini zaidi ya Kuzoea Ku deal na Coursework za wanafunzi

Shida mteuaji mwenyewe naye ni mshika chaki hivyo nadhani ana imani kubwa na washika chaki.
 
Kwa kweli huyu Dr.Mwinuka aliyeteuliwa anastahili cheo hicho,kwa wanaomfahamu huyu jamaa ni mchapakazi hatari mwenye hofu ya Mungu
"Mchapakazi hatari" una maanisha nini mkuu?
 
Mwinuka????? Dah haya bwana... Ila katoa fadhila kwa Wahaya ili kesho abwate weee na mambo mengine yaende!! Mwinuka ni mchanga mno na hajawahi kuwa mbunifu hata kidogo.! Hapana!! Mwinuka Tito hapana!!!!!
Sio kila postninahotaji ubunifu, huyo mrambi aliyekuwa mbunifu ni kili alichokifanya zaidi ya kuliingiza shirika katika madeni na kubuni watumiaji ndio walipe, kwa sasa tanesco waziri hisika anao utaalamu na uzoefu wala haitajiki mkurugenzi pale, mtu muhimu ni fundi wa service line endapo kutatokea dharura. Safi mheshimiwa raisi, mungu ibariki Tanzania.
 
Hii serikali mbona inafanya watu wote kama hatuna akili. kuhusu kupandisha kwa bei mbona EWURA waliweka kila kitu public?? Kwann serikali isiingilie kati toka wakati ule???. Yan Jan Mos imefika maamuzi ya mlipulipuko yanafanyika as if ndo serikali yote imejua jana kwamba bei ya umeme itapanda. Hapa ndipo serikali ya Mtukufu Rais inapopofanya siasa wakati ndugu zangu wa Upinzani wanapigwa mikwara kila leo. Hiz ni siasa uchwara.[HASHTAG]#SerikaliYaMilipuko[/HASHTAG].
Mikutano yote wananchi walipinga ila ewura na tanesco wamepandisha kimyakimya
 
Hapo ndo unaona makali ya JPM ukimpa pande hakuachi.
Na Magufuli keshawajulia anajuwa mnapenda kumuona akifukuza fukuza watu ili mwendelee kumuita "Jembe" mkijakushtuka 2020 hana alichofanya.
 
Back
Top Bottom