Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Binafsi nashindwa kuielewa hii serikali ktk watu smart na makink waliowahi kuwa wakurugenzi pale tanesco Mramba ni the best hii inshu ya bei ya umeme lazima raisi alikuwa anajua waziri na wizara yake wanajua na hata bodi ndo waliipitisha hii sasa sijaelewa raisi anaposema eti hakuhusishwa hizi siasa hazitatufikisha popote pale kwa miaka 5 itakuwa haya haya tengue teua tengua teua
 
huyu mramba ni sawa tu kutumbuliwa umeme umeshushwa mwaka jana mwezi wa nne baada ya miezi 8 eti upande hakujielewa
 
Kama kuna sekta zinazo hitajika kufumuliwa na kuundwa upya basi Tanesco na idara za maji nchi nzima,huwezi fanya kazi kwa mazoea kiasi hicho huu ni unyumbu wa hari ya juu mno. Tanesco inapashwa kuanzia sasa iwatafute wateja popote walipo na kuwaunganishia umeme kwa bei ya chini kabisa ili itengeneze fedha kwa watu kununua umeme,pia idara za maji ziwafwate wateja na kuwaunganishia maji almost for free ili watu wanunue maji. Sio huu mpango wa kuuza nguzo kwa raiya ni unyumbu ulio pitiliza,mteja afwatwe huko aliko sio kumsubili ofosini.
 
Uskute mzee wa watu jana katuma sms za wishes ya mwaka mpya yenye kutaka 2017 uwe mzuri kwake,kwa bahati mbaya hata tarehe 1januari haijaisha kaanza na gundu,bonge la nuksi hii...
 
Mramba ni the best how?
 
Matokeo yake mteja ndie anawabembeleza Tanesco ili wamuungie umeme hadi anahonga ili aupate umeme.
 
Twafwa!
Magufuli baba watumbua siku ya kwanza ya mwaka, tena jumapili!
 
Sikubaliani na wewe kampuni kama hii kuongozwa na BCom. Anatakiwa Eng aliye na MBA au Project Management.

BCom itabidi atumie muda mwingi kujifunza na ku-understand their language kabla ya kuanza kuperform. Unless awe amekuwa kwenye hii industry kwa muda mrefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…