Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

MKURUGENZI MKUU TANESCO ATUMBULIWA.

Rais Magufuli amemfukuza kazi Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Mhandisi Felchesmi Mramba kwa kutengua uteuzi wake kuanzia leo na amemteua Dkt Tito Esau Mwinuka kuwa Kaimu Mkurugenzi mpya wa TANESCO.

 
Pamoja na kutumbuliwa Kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, kuna haja pia ya kuangalia kwa undani zaidi ktk shirika kuna "VIRUSI" ambavyo si salama sana Kwa utendaji wa shirika letu.

Mhe waziri prof: muhongo tuna kuomba sana isafishe Tanesco ikae sawasawa, Kuna haja ya kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini kama kuna "virusi" viondoe mapema kabla havija zidi kuathiri.
 
Dsh! Huyu jamma anaeeze mtumbua hata askofu anakasi kama ya neymar wa baselona
 
Sijui kosa la Mramba ila katika wakurugenzi wa taa nesco huyu alipiga kazi.
Ninachoona ni (............)
 
Kuna comments naziona humu zinashangaza kweli. Kuna wachangiaji naona hawajui au wamejisahaulisha taasisi kama EWURA na mashirika ya umma yanafanyaje kazi. Wanasahau kuhusu kazi na majukumu ya bodi zinazosimamia mashirika/taasisi. Wanasahau ushirikikishwaji wa Serikali upoje kwenye maamuzi na utekelezaji wa maamuzi ya taasisi kama EWURA. Kwa ufupi tu, yatupasa tutambue kuwa tunachezewa akili na mamlaka ya uteuzi kwa malengo ambayo inayajua yenyewe - wengine watasema ya kisiasa, wengine watasema hili na wengine lile.
 
Sijui kosa la Mramba ila katika wakurugenzi wa taa nesco huyu alipiga kazi.
Ninachoona ni (............)
KOSA LIPO HAPA MKUU

Wakuu wa TANESCO hawawpaswi kulipana bonus kila mwisho wa mwaka kiasi cha kufikia Tzs. 60m/- kwa mtu mmoja wakati shirika linashindwa kujiendesha isipokuwa kwa kupandisha bei ya Umeme. Hii inamaanisha kuwa wananchi wakamuliwe ili ipatikane pesa ya mabosi wa TANESCO kulipana bonus! Prof. Muhongo amesema ameagiza hata hiyo bonus isilipwe au irudishwe kwa waliokwisha kulipwa.
 
Tanzania ina bahati, kwa mara ya kwanza tumepata rais mwenye PhD (original siyo Hon.) tena ya sayansi, siyo sanaa.
Na hatutakiwi kuihoji, lasivyo "tunapotea" kama yule jamaa.
 
Kaka wanalipana bonas?.ndo nasema kuwa idara na taasisi za serikali zote inabidi ziwe sawa kuanzia kima cha mshahara
 

Bonus zinapitishwa bodi kwa nini panga halijapita na huko
 
After all mramba kama mkurugenz mkuu wa shirika alichokifanya yeye ni kupendekeza ombi lake baada ya kuona gharama ya uendeshaji inaleta shida...kwa kupitia bodi yake ya Tanesco akaamua kupendekeza...then bodi kwa kutoa baraka zake ombi likaenda ewura na ewura nao wakaaprove...

Sasa hapo ilitakiwa Magufuli aanze na regulatory authority ambayo ni ewura kisha aje awaulize tanesco kwann wakitaka wapandishe bei ya umeme.

Na hata ukiangalia barua ambayo muhongo kaandika na kumcopy Rais na makamu na wazir mkuu aliandika kwa mkurugenz mkuu wa ewura na siyo Tanesco.

Juma is Poor Manager.
 
Acha porojo sister,kwa hiyo unapendekezwa Mramba aachwe kwa sababu tu kuna Escrow!
 

Mkuu, kheri ya Mwaka Mpya.

Mramba hajaonewa ila naona huna facts kuhusu khasa kilichomtoa hapo Tanesco.

Inawezekana likawa ni suala la EWURA au pia tangu mwezi may alipoagizwa asitishe mazungumzo na Symbion kuhusu PPA (power production agreement) na serikali.

Lakini pia inawezekana na gharama kubwa ambazo Tanesco inalipa kwa IPP independent power producers.

Utakumbuka hotuba ya bajeti ya profesa Muhongo bungeni mwezi Juni alisema kwamba serikali ipo kwenye mchakato wa kuondokana na IPPs kwa kuwa sasa tuna hata gesi kutoka Mtwara.

Mramba ameagizwa na serikali kuangalia mikataba ambayo Tanesco ilisaini na hawa IPPs na khasa ule wa Symbion ambao wanalipwa kiasi cha dola bilioni 5 kwa mwezi kwa kuwauzia umeme Tanesco kwenye mikoa ya Dar, Arusha na Dodoma.

Jambo baya kabisa kuhusu huu mkataba wa PPA ni kwamba iwe umeme upo au hakuna lazima Tanesco wawalipe Symbion kasi hicho cha fedha kila mwezi.

Na tatizo Mramba alisaini mkataba huo harakaharaka kabla ya raisi JPM kuingia, hivyo unategemea nini hapo?

Unapopewa maagizo na serikali khasa yenye kuhusu maslahi ya taifa (siyo maslahi binafsi) unatakiwa kuwa mwangalifu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…