Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Najua hilo ila niliona ujio wa gesi utaongeza uzalishaji wa umeme hivyo umeme wa maji ungeshuka kidogo badala yake wanapandisha
gift, acha kusikiliza kauli za wanasiasa!haya mambo ni ya kitaalamu sana. Kuchimba gesi baharini ni ghali usiombe. Anayewekeza huko kurudisha hela zake lazima gesi iuzwe gari and hence umeme. Mnadanganywa tu. I have been in Norway, Sweden where Statoil (Norway) is situated! Nimeongea na wao kama marafiki tu, sio kazi rahisi
 
Hivi kosa ndio hilo la kuiomba EWURA ipandishe bei ili kuweza kujiendesha?au kuna mengine?
nadhani kuna la ziada hapo maana kuna wahauri wanampotosha kiongozi wetu mbona wa ewura kaachwa????y mramba ???
 
Hiyo ndio kauli mbiu yetu kwa sasa, tunawalinda "wanyonge walioumbwa kwa mfano wa Mungu"; wanaowanyanyasa wameumbwa kwa mfano wa shetani, ni kuwatumbua tu, hakuna namna nyingine!
 
Kweli kabisa. Na hili ndo linatokea ATCL. Japo MD wake siyo phd lakini kwa vile ni wa kuokotwa mambo hayaendi
 
Serekali inawasiliana kwa nyaraka...madokezo...paper trail sio kujitangazia tangazia
Unaweza kutoa flow ya how things need to be done kabla ya kutangaza bei mpya ya umeme?! Usiongee kwa maneno bali with reference manake EWURA wamesema wazi kwamba:

Hao sasa, wanadai walifuata taratibu kwa mujibu wa sheria na kanuni hizo hapo juu! Which means; kama taratibu hazikufuatwa; ina maana EWURA nao hawakufuata sheria na kwa kiburi tu wakapokea maombi ambayo hayakufuata utaratibu na hatimae kuidhinisha kupanda umeme wakati taratibu hazikufuatwa!!!

Kwanini basi serikali hawakuanza na hawa waliodhinisha upandaji wa bei ya umeme wakati serikali haijaarifiwa? Au hiyo EWURA ina mamlaka nyingine juu yake?!
 
nadhani kuna la ziada hapo maana kuna wahauri wanampotosha kiongozi wetu mbona wa ewura kaachwa????y mramba ???
Hapa naona kuna kitu, hata ingekuwa mimi ningependa shirika ninaloliendesha lipate faida kubwa! Lazima nilete mapendekezo ya kupandisha bei! Ila pia kuna mdhibiti anahakiki! Sasa Huyu Mramba kosa lake ni nini? Mimi sioni mdhibiti kakubali sasa ndio mwenye proposal ahukumiwe?
 
Kama mtu anamkamua mwananchi maskini mvuja jasho ili kujilipa bonus ya mamilioni kwa mwaka, sina huruma na mtu huyo bila kujali ametokea kusini au kaskazini. Koo za mafisadi zikalime kahawa zile jasho la halali kama tufanyavyo siye.
 
Mwaga uali wa Escrow.Bado gavana Ndulu zama mpya na mambo mapya timua wote hata watendaji wa kata.
 
Mkuu kwa akili ya kawaida hata mtoto wa darasa la saba anaelewa kuchukua hiyo kitu baharini sio kitu kidogo teknolojia ya juu inahitajika.

Ila sioni sababu ya tanesko kupandisha umeme labda waseme wanashindwa kucontrol umeme wao wajanja wanaiba hivyo wanaingia hasara.

Ukishindwa kucontrol kinachotoka basii hata kinachoingia hutaweza. kuna sehemu nimeishi mambo yanafanywa bwana sio mchezo. sababu ya tanesko kupata bhasara ni kuibiwa umeme hivyo ni uzembe wao wala sioni sababu ya kupandisha bei bali walinde nishati yao isiibiwe na wezi
 
ndio maana nikasema kuna la ziada yaan mtu aliyetoa ruhusa kaachwa aliyetoa wazo katumbuliwa maajabu zaidi yatatokea!!
 

Nimekupata mkuu, kama wewe ungekuwa Mangu namfahamu vizuri na ule undugu wake na Tundu Lissu.

Usikute vetting yake imepitia mezani kwangu.

Nimepiga sana biashara za ujasirimali Singida.

JF ni sebule ya majadiliano tuondoe personal issues.

πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Tuna ushahidi thabiti kuwa umeme unaibiwa kwa kiwango unachokisema cha kuleta hasara kubwa hivyo? Au ni wanasiasa? Mimi umeme unaniathiri ukipanda, sitaki bei ipande, ila siungi mkono the way we make decision on such important issues, victimizing people.
 
Daaaah yani hakuna watu wanafiki dunia hii kama UKAWA,nyie watu pepo hamtaiona kwa unafiki na uzandiki ulivoawakaa,mmepiga kelele hapa jf tangu jpm aingie madarakani kuwa tanesco ni jipu,tulitangaziwa kupanda kwa gharama za umeme mkasema jpm hana la kufanya tanesco imemshinda,jana kamtumbua mkaskazini mwenzenu mmeanza kumdhihaki jpm na mmekuwa upande wa tanesco,kweli hii mitandao izimwe nyie nyumbu tuwasikie kwa sauti zenu halisi
 
Udini maybe but be sure ukabila is real.
 

Mkuu, EURA walitakiwa warudishe maombi hayo ya Tanesco mpaka ufafanuzi na makubalino na waziri Muhongo yatakapotokea.

Mramba alipaswa kumshauri waziri (ambae tayari walikuwa hawaivi kutokana na kauli yake kule bungeni kuhusu ufanisi mbovu wa Tanesco)

Hivyo utaratibu ni EWURA kurudisha maombi kwa Tanesco na kuwashauri wamwone waziri ambae ana mamlaka kisheria na kikatiba kuangalia hizo bei ya umeme na kutoa maamuzi ya mwisho.

Mtizamo wako wewe juu la hili ukoje?
 
argument ya msingi kuhusu kutenguliwa kwa Mramba ni kwamba hawakufuate procedure..
Hii sababu inaonekana siyo ya kweli maana kama sababu ni hiyo, board na mkurugenzi wa EWURA walistahili kuwa wa kwanza kuhojiwa.

Huenda sababu ya kufukuzwa kwake ni kulipana bonus lakini hata hiyo sidhani anayelipwa ni pekee yake. Kwa nini board iliyoidhinisha isiwe mhusika mkuu wa kwanza?
 
belive m ukinunua umeme wa buku unapata uniti 2.9 vat n kama 180 na points, kacm kangu hakawez ku2pia picha. ko 800 tugawe kwa unit 2.9 tutapata bei ya unit 1
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…