Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Rais Magufuli leo ametengua rasmi uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini(TANESCO), Eng. Felchesmi Mramba.

Aidha Rais amemteua Dkt. Tito Esau Mwinuka kukaimu nafasi hiyo. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Mwinuka alikuwa mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM).


Bora angemrudisha Eng Mhando
 
Majibu mazuri sana, yafungulie thread mpya then waambie mods wasiifute au kuiunganisha na thread nyinginezo.
Na Title iandike kwa herufi kubwa ili wadau wa JamiiForums waione kirahisi.
nendeni songas, IPTL na Wattsila na TANESCO acheni hizi propaganda za kitoto..............................Ushajiuliza kwanini DR MANYAHI alijitoa kwenye bodi ya Tanesco
 
Huyu wa ewura hawezi kutumbuliwa kwa sababu zilizo nje ya mfumo ulioratibiwa
Ni kutafutana kwenda mbele, kule aliiondoa bodi akaiacha management, wakati management ndo iliishaur bodi. Huku anaiindoa management (DG) bodi ikibaki
 
Ninaota Watanzania tunaenda kutumbukia kwenye shimo baya sana, ambalo kuchomoka itatuchukua muda. Kwa sababu nchi sasa imekumbwa na shetani wa hisia. Kuanzia kwa Wananchi hadi viongozi. Siamini kama utafiti umefanyika kuhusu kwa nini TANESCO walitaka kupandisha bei! Hivi zile kesi za TANESCO nani analipia gharama zake? Mimi nadhani huo uamuzi haukuwa wa mkurugenzi peke yake. Sidhani kama mkurugenzi alijiamlia mwenyewe kupandisha bei ya umeme. Ningependa sana huyu mkurugenzi angeweka wazi sababu za kupandisha umeme.
 
Mimi naomba mnisadie... hivi alivyotumbuliwa anaondoka Tanesco au anaendelea kuwa mfanyakazi wa Tanesco ila tu anakuwa siyo Mkurugenzi mkuu tena?
Hawezi kufanya tena hapo manake anasubiria kupangiiwa kazi nyingine katika taasisi nyingine
Kwan Msigwa atakapo tenguliwa,press release ataandaa nan?
Teh,nko nawaza tu.
 
Dah Magufuli kumteua Mwinuka sijui kawaza nini? Kati ya sehemu ambazo hutakiwi kufanya majaribio ni Tanesco.. Kama ni kutafuta mtu pale UDSM basi Prof. Kimambo alikuwa anaweza sanaaa ila siyo Mwinuka!! Ila sasa ndo hivyo tena Kimambo anapitia Chalinze Mzee na huwa anakula pale Mombo.. humo hataki hata kuwasikia lakini Kimambo ni bonge la mbunifu!!
amefanya ubunifu gani ?
 
Au jina lake limo kwenye Ile orodha ya vile vitabu vitatu alivyokabidhiwa na mzee wa msoga.
 
Alikua anamtafutia target duuh noma sana
 
Leo Rais Magufuri ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Mwandisi Felchesmi Mramba kwa sababu ya kuomba ongezeko la gharama za umeme Ewura ya asilimia 18.5.

Kisheria Tanesco hawana Mamlaka ya kupandisha umeme isipokuwa kupeleka mapendekezo yao Ewura kwa maana hiyo Ewura wanaweza kukataa au kukubali.

Ewura kukubali mapendekezo ya Tanesco na kuamua kukubali ongezeko la asilimia 18.
 
Ningeshangaa sana holiday ndefu kama hii iishe bila kutumbuliwa mtu ndio wakati ambao JPM anapata muda wa kutafakari sana na kupata majawabu sahihi
 
Safi sana, wa ewura nae aondoke. wanatupandishia gharama za kuishi bila sababu! Ongera Magu.
 
Hii nchi sasa wakurugenzi wa mashirika ya umma itabidi waangalie upya Maisha yao!!!! Kuna kudhalilishana sana!!! Ukiona mambo Yanaenda kisiasa achia ngazi utani na heshima yako!!!!! Ujinga wa watanzania ni kule kuwa mnafiki na kutokuwa jasiri wa kusimamia unachoamini!!!! Njaa mbaya sana!!!!
 
Kama vile maigizo hivi...Huko Serikalini Vp? coordination ya serikali kabla ya jambo lolote haipo?
DG Wa EWURA hakupeleka ripoti ya mapendekezo kwa waziri mwenye dhamana ya masuala ya umeme. Ndipo coordination ilipoharibikia. I bet huyu wa Ewura nae siku zake zinahesabika
 
Back
Top Bottom