Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Matokeo yake mteja ndie anawabembeleza Tanesco ili wamuungie umeme hadi anahonga ili aupate umeme.
Hii kitu ni ujinga ulio pitiliza,nakuhakikishia ikitokea shilika akapewa mzungu kitu cha kwanza kufanya atajitahidi kuwafwata wateja mpaka vichochoroni na kuwaonganishia umeme almost bure ili watu wanunue umeme na yeye apate fedha.
 
Eng. Felchesmi Mramba kutumbuliwa ni stahili yake haswa kwa kuwa yeye ndiye aliwashawishi EWURA kuwa hakuna namna nyingine ambayo shirika linaweza Fanya ili kujiendesha kiufanisi zaidi ya kuongeza bei za umeme

yeye alipaswa kutafakari kwa kina namna atakavyoendesha shirika kwa ufananisi pasi na kuongeza bei za umeme kwa mfano angeweza punguza gharama za uendeshaji kama hayo maeneo ambayo waziri muhongo ameyaonesha.

By the way muhongo ni mnafiki na ni mjanja sana kwa kuwa ameweza kuzisoma vyema Alama za nyakati mchakato wa kuongeza bei alikuwa anaujua na hakuchukua hatua amesubiri mpaka bei zimepanda ndipo kaona mtukufu anaweza akasepa na kijiji so ni vyema akalinda kibarua chake kwa kutumia plan B yaani kupinga ongezeko la bei.alipaswa kuupinga mchakato wenyewe kama aliona ongezeko lililoombea na Tanesco alikuwa na tijabyoyote.Pongezi mh mhongo kwenye wewe ni professional
 
Sikubaliani na wewe kampuni kama hii kuongozwa na BCom. Anatakiwa Eng aliye na MBA au Project Management.

BCom itabidi atumie muda mwingi kujifunza na ku-understand their language kabla ya kuanza kuperform. Unless awe amekuwa kwenye hii industry kwa muda mrefu.


Mkuu hebu soma tena ulichoandika kisha uje uniambie hukubalini na mimi kitu gani.
 
Alimuita wakajadili sababu za kupandisha gharama za umeme tunaongozwa kwa visasi na visa vya kutaka sifa ya kuonekana tunajitoa kwajili ya wananchi ila muda ndio msema kweli Jana ilikuwa 2016 Leo 2017 kesho kutwa 2018 tutaona ukweli wa huu utumbuaji kama maisha ya wananchi yatakuwa mazuri au yatakuwa afathalia ya jana
 
bora kamtumbua bado kitengo cha ewura.
unapandisha umeme kwa wanyonge?????
 
Naona alipotoka kwenye ibada mwasho ulipanda..maana alikuwa anaongea kwa uchu kweli.
 
Let say he is right kachukizwa na maamuz ya kupandishwa kwa bei ya umeme ni obvious kwamba Mramba hawez kufanya hivyo bila baraka ya bodi..sasa anaiachaje bodi na kumuondoa mramba.

Pili shirika kama Tanesco linahitaji taaluma ya uendeshaji na siyo kuchukua intruder ambae hata hafaham na hana taaluma hiyo na wala hana experience ya uendeshaji

Mfano Dr Idrisa Rashid ilimchukua muda sana hadi kuja kumaster challanges na kusonga mbele

Wapo watu hapo Tanesco wenye uwezo mkubwa tuh kama Engineer Nazir Kachwamba...Engineer Deklan Mhaiki...na kadhalika ambao may be wangeweza kumrith mramba

Sasa kukimbilia kufanya maamuz ya mlipuko kama hayo ni kutuaminisha kwamba kuna watu wake alishawaandaa na anawatafutia kazi...ma kututhibitishia kwamba katika awamu hii wachaga na waislam ni watu wa kuogopwa kama ukoma
Kumekua na Wimbi la Kuteua Wahadhiri ambao hawajawahi hata kukaa Ofisini zaidi ya Kuzoea Ku deal na Coursework za wanafunzi hivi kwa mfano Utumbuzi wa Lawrence Mafuru pale Wizara ya Fedha alikosekana mtu kweli hadi wakaenda kumchukua Lecture wa Economics UDSM?

Mwele Malecela ametumbuliwa hivi karibuni katika kitui cha Utafiti wa Tiba na Magonjwa cha Ajabu hajapelekwa pale Daktari Wa binanadamu amepelekwa mtu aliyebobea kwenye Fisheries!

Leo hii ametumbuliwa ndugu Engineer Mramba hivi hata pale TANESCO walimkosa mtu wa kushika nafasi hiyo sizijui sana mpangilio/hirachy za vyeo pale Tanesco lakini Hata Regional Managers wanaweza kushika nafasi hiyo tofauti na aliyetoka kushika chako moja kwa moja.
 
Mnama naona povu linakutoka ovyo ndugu yetu katumbuliwa daah!

Tulikuwa namshambulia JK bure alitukumbuka kina meku sasa huu mziki wa sasa hivi ni hatari mnama.

Tufanyeje mnama?
Mkuu hizi siasa za kuwatenga kina meku ni nzuri sana. Zinatakiwa ziachwe zimee sana muda ukifika tutapata majibu. Kule Rwanda hazikuanza siku moja zilipaliliwa zikamwagiliwa maji muda ulipofika wakavuna. Wacha tuvumilie tu mnama.
 
Wakati mwingine hawa wakurugenzi wanajioteshea wenyewe majipu. nchi inaongozwa na wanasiasa, wanasiasa wameahidi wananchi bei ya umeme itapungua. wewe unakuja na madharau yako unaongeza bei against the promise ya yule yule aliyekuteua.

Mramba hakujifunza kwa yale yaliyowakuta viongozi wa jiji la mwanza dhidi ya wamachinga.

Mkuu wa nchi anataka nchi ya viwanda halafu mashetani wengine wanataka kumwakwamisha.
 
Kubadilisha watu si suluhisho.kwa mwendo huu atamaliza nchi nzima na Umeme utaendelea kuwa kero nchi hii.
 
Back
Top Bottom