Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, F. Mramba. Amteua Dkt. Mwinuka kukaimu

Maamuzi ya mwendo kasi.Nina uhakika utumbuaji huu hauna uhusiano kabisa na maamuzi ya mapendekezo ya kupanda kwa bei ya "nishati " yaliyofanyika hivi karibuni bali ni ule muendelezo wa kutaka kuweka "watu wake" sehemu muhimu.Kwani kwa mtu yeyote makini wa nishati hii anayejua "trend" nzima ya shirika hilo jinsi lilivyochoka na mzigo wa madeni lililonalo lililosabishiwa na serikali yenyewe hakukuwa na jinsi nyingine zaidi ya hayo mapendekezo na pia sio kwamba kutoa mapendekezo ni kosa bali anayetoa ruhusa ndo anastahili kuadhibiwa na sio mtoa mapendekezo.
 
Leo ni siku ngumu sana kwa kaka yangu Mramba, lakini namuomba awa na moyo mgumu kama chuma ndivyo alivyo rais wetu.

Ndugu zangu wana Jf katika sakata la tanesco lazima tuwe na maswali mawili kama kweli tunafikiria.

1. Labda kesi sio kuomba na kukubaliwa.

Watanzania wengi tunajaji kwanini bodo ya tanesco rais katenguwa, kwasababu tanesco waliomba maombi kabla.

2. Labda kesi ni kushindwa kudhibiti gharama za uzalishaji.

..................................................................................................................................................................................................................

IMG_20170101_162106.jpg


Hii wenzetu wanaita "in house play" nyumba ya kwako unapitia dirishani.Tz
1f64f.png
 
Sikubaliani na wewe kampuni kama hii kuongozwa na BCom. Anatakiwa Eng aliye na MBA au Project Management.

BCom itabidi atumie muda mwingi kujifunza na ku-understand their language kabla ya kuanza kuperform. Unless awe amekuwa kwenye hii industry kwa muda mrefu.
Hapa hata hahitajiki engineer ni MBA au mtaalamu yeyote wa management.
 
mkuu unit700anagawa wapi sijaelewa
Alikuwa anawagawia unit 700 bure kwa akina nani? Wakiume au wakike? Wasomi au makabwela? Funguka fafanua!![/QUOTE]

Soma link hiyo

Au nakusaidia hapa chini

_______

MKATA KIUJF-Expert Member
#1
Nov 23, 2016

Bila kupoteza muda wafanyakazi wa TANESCO wote wanapewa units za umeme 700 kila mwezi kwa shilingi elfu 10 tu.

Huku mtanzania maskini anapandishiwa bei za umeme kila kukicha?


Hii sio fair!

Halafu wanasema tanesco inapata hasara huku wanajipa umeme wa thamani ya laki mbili kwa shilingi elfu 10 tu, hapo tanesco ina wafanyakazi karibu 5000 huu si ukichaa huu. wakisema hawajui chanzo cha hasara zao...

Hili nalo la kumsubiri Donald Trump kweli aseme waafrica hatujui kujiongoza na hatuna akili

Mtu unamlipa mshahara mamilioni... bado unampa na umeme wa laki mbili au tatu bure.. wakati shirika linajiendesha kwa hasara.. linategemea ruzuku za serikali.

Ha ha ha Donald Trump ni mkweli sana kwamba kuna watu wa iq ndogo sana hasa weusi.

Mchawi wa tanesco ni tanesco wenyewe hata waongeze bei ya umeme.. kwa hili la kujipa umeme bure wote hawawezi kuendelea.
 
[01/01/2017 18:56] Robertson: Leo 1.1.2017 Prof. Muhongo amehojiwa na Radio One na kueleza sababu za kusitisha mpango wa EWURA wa kupandisha bei ya Umeme kwa 8.5% kama ifuatavyo: -

1. Kwenye mikutano ya 'public hearing' nchini kote wadau walipinga myongeza ya bei;

2. hadi jana 31.12.2017 EWURA, kinyume na matakwa ya sheria, haikuwa imepeleka ripoti ya uamuzi wake kwa waziri mwenye dhamana, kujadiliwa na kupitishwa/kuthibitishwa kabla ya kutangazwa kwa pendekezo la bei mpya;

3. Ufumbuzi wa matatizo ya kifedha (madeni) wa TANESCO hauwezi utatuliwa kwa kupandisha bei ya Umeme. TANESCO inatakiwa kuwa na mkakati wa ku-improve efficiency kwenye management yake badala ya kuongeza bei ya Umeme; na

4. Wakuu wa TANESCO hawawpaswi kulipana bonus kila mwisho wa mwaka kiasi cha kufikia Tzs. 60m/- kwa mtu mmoja wakati shirika linashindwa kujiendesha isipokuwa kwa kupandisha bei ya Umeme. Hii inamaanisha kuwa wananchi wakamuliwe ili ipatikane pesa ya mabosi wa TANESCO kulipana bonus! Prof. Muhongo amesema ameagiza hata hiyo bonus isilipwe au irudishwe kwa waliokwisha kulipwa.

Soma sababu ya NNE ndo imekula Mramba
 
Ha ha ha ha Picha ndio limeanza. On the Phone from Tetemeko..."Naniii hebu edit ile barua ya Dr. NIMR weka hili jina huyu jamaa wa TANESCO........"
Haaaahaaaa jf mama mbavu zanguuu ! Ivi hiyo simu ni yakupiga tuu ! Nani ata mpigia
 
Tarehe na mwezi aliyotumbuliwa ni rahisi sana kuikumbuka. Kamwe hataisahau. Tarehe 1 1
 
kwa hiyo suluhisho nikupand isha bei
Wala suluhisho si kupandisha bei. Tunaelezwa kila siku hapa tanesco wameingia mikataba ya kifisadi na uendeshaji mzima wa shirika upo kwa maslahi ya vigogo leo mnakuja kumfukuza kazi mramba.
Kwanini msiwakamate wakina IPTL na wale wazee wa escrow account wanaendelea kuchota mabilioni kila dakika?
 
Hongera ulimwengu, sasa hakuna nidhamu ya kazi Bali kuna nidhamu ya woga
 
Ra
Ha ha ha ha Picha ndio limeanza. On the Phone from Tetemeko..."Naniii hebu edit ile barua ya Dr. NIMR weka hili jina huyu jamaa wa TANESCO........"
Rais anatembea na mwandishi wake wa habari popote aendapo,hakuna haja ya simu ni papo kwa papo
 
Sasa hawa wahadhiri mbona wanaisha pale UDSM😵😵😵
Hawataisha wako wengi tu. Siku hizi PhD watu wengi tu wanazipata. Wengine wana PhD tatu au zaidi kwa mtu mmoja. Enzi za kuwapa watu madaraka makubwa ilihali kisomo chao ni duni kimepitwa na wakati. Haiingii akilini mtu ana kashahada kamoja tu ka umeme anapewa shirika kubwa la umeme kama la TANESCO wakati kuna mamia ya watu walio na ma PhD ya umeme? Hakuna cha godfather siku hizi. Godfather ni kisomo chako na hasa PhD yako. Tanzania ina bahati, kwa mara ya kwanza tumepata rais mwenye PhD (original siyo Hon.) tena ya sayansi, siyo sanaa.
 
Wala suluhisho si kupandisha bei. Tunaelezwa kila siku hapa tanesco wameingia mikataba ya kifisadi na uendeshaji mzima wa shirika upo kwa maslahi ya vigogo leo mnakuja kumfukuza kazi mramba.
Kwanini msiwakamate wakina IPTL na wale wazee wa escrow account wanaendelea kuchota mabilioni kila dakika?
Acha kuhamisha magoli wewe.aliekutwa na ngozi ndie alieuwa chui
 
Back
Top Bottom