Serikali ‘yamwaga’ ajira 15,000
IMEANDIKWA NA MAGNUS MAHENGE, DODOMA | IMECHAPISHWA: 04 MEI 2017
SERIKALI itamwaga ajira 15,000 kwa watumishi wa kada mbalimbali serikalini kabla ya Juni 30, mwaka huu.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk Laurean Ndumbaro akizungumza na vyombo vya habari kwenye Ukumbi wa Habari wa Bunge, alisema ajira hizo ni za mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, mwaka huu na uchambuzi unaoonesha kila kada itapata watumishi wangapi utatolewa baadaye.
http://www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/22617-serikali-yamwaga-ajira-15-000