Magufuli hayupo kipi kinawafanya CHADEMA kuliachia hewani suala la Wabunge 19 wa Viti Maalum?

Mkuu,lakin bado wanajitambulisha kama ni wabunge wa chadema bado hapo bungeni,inatuacha njia panda wananchi
hiki ni kielelezo cha taasisi zetu kuwa dhaifu kiutendaji - hili ni tatizo kubwa sana - mifumo ya utawala wa Taifa letu una matobo mengi.


 
Ruzuku inawatoa udenda, ndio mana wameufyanta!🤣
 
Suala la wakina Halima Mdee lipo nje ya uwezo wa Chadema kama chama.
 
Ni kweli kama chadema wako serious sana na wanataka mabadiliko wanayo ya hubiri ni wakati wa kufanya maandamano nchi nzima kulazimisha wabunge hao watolewe.

Namimi nawauliza wanaogopa nini?
Hivi yale maandamano ya BAWACHA yaliishia wapi ? Au alivyotolewa Afande Muroto na kiki za maandamano zimekufa naturally.
 
hiki ni kielelezo cha taasisi zetu kuwa dhaifu kiutendaji - hili ni tatizo kubwa sana - mifumo ya utawala wa Taifa letu una matobo mengi.


Asante mkuu,saut iendelee kupazwa
 
Na kama wamepata nafas ya kuzunguka nchi maeneo karibu yote,kuhamasisha katiba mpya, wataweza vip kuitetea hiyo katiba mpya,na Ili hali hii ya sasa inavunjwa na wako weak katika kuitetea isivunjwe?
Shida waliweza kujificha kwenye kichaka cha Magufuli na sasa Magufuli is dead and gone watamwimbie wanaogopa nini kama wao ni wana mabadiliko?
 
Binafsi nashauri wasamehewe na MAISHA YAENDELEE

YALIYOPITA SINDWELE TUGANGE YAJAYO
 
Hatuwalaum,swali letu kwao ni kwamba wao kama chama wameshakata tamaa tayar juu ya suala Hilo?
Chadema imewafuta uanachama, katiba inasema nini kuhusu mbunge asiyekua na chama? Kina mama wa Chadema walitaka kuandamana hadi kwa spika hi ni baada ya spika kuendelea kuwalinda, uliusikia ule mkwara wa police kuhusu hayo maandamano? Unataka Chadema wafanye nini zaidi mkuu? Mbona hili kama ni jukumu la wananchi tena na sio Chadema.
 
Watanzania ni watu wa ajabu sana! Ukiwaonyesha tatizo lilipo wanataka wewe mwenyewe uliyeona tatizo ulitatue. Hii siyo kweli. Wengine tunatakiwa kusimamia kile alichotuonyesha mwenzetu ili tatizo liondoke. Sasa tukiendelea kusema, wewe uliyeona na kutuonyesha tatizo ndiye utatue hatutendi ipasavyo.

Fedha zinazofujwa na covid-19 ni za umma. Mtu mmoja angeenda hata mahakamani kushitaki kuvunjwa kwa katiba, kwamba kuna fedha za umma zinafujwa na wabunge hawa wasio na chama wakati katiba inamtaka mbunge awe na Chama.
 
Haahaa hyo itakuwa Sio taasisi Ni kikundi Cha wahuni, yaani sawa na mtu mwenye gari akafoji plate number za gari, Kisha raia mwema akatoa taarifa polis, Kisha polis asichukue hatua Kisha alaumiwe aliyetoa taarifa.
Kweli ndugu yangu. Chama kimetwambia wale sio wanachama wao. Sisi wenye fedha yetu tupaze sauti ili fedha hizo ziende kununua gloves hospitalini.
 
Sawa mkuu ILA ruzuku Chadema hawachukui na hii sio siri kabisa,always ukweli ubakie hivyo ili kuifanya hii JF iaminike
 
CHADEMA walishalimaliza hili suala kwenye first phase, wakawavua uanachama, sasa kuwaondoa bungeni kama mleta mada unavyotaka ni suala la Ndugai ambapo taratibu zote za kufanya hivyo kwa upande wa Chadema walizimaliza, kusema Chadema wamepoa sio kweli, wanaonekana kupoa kwasababu kazi yao walishaimaliza.

Hata hilo Baraza Kuu likija kukaa japo linaonekana kusuasua, kazi yake naamini itakuwa ni kupigilia msumari kile kilichofanywa na KK, sidhani kama patakuwa na jingine jipya zaidi ya hilo, kwani mpaka kufikia hapa tulipo, wale jamaa kule bungeni ni wahujumu uchumi tu, sio wanachama wa Chadema, binafsi ningependa Samia aoneshe kwa vitendo haki anayoipigania kwenye hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…