Uchaguzi 2020 Magufuli kakosea sana kampeni zake mkoani Mara. Je, haujui mkoa ule au hapendi watu wake?

Baada ya kuapishwa alikuja Chuga ambako hakupata kura nyingi akiwa kavalia kombati za JWTZ kuonesha msiyempenda kaja....katumia miaka mitano kutunyoosha, sasa ni zamu yetu kutumia walau siku moja tu kumyoosha....tukutane October 28.
Huyu jamaa wa hovyo sana
 
Hata hao unaosagesti warudishwe wanakinaisha sababu muda wao ulishapita....wasanii wenyewe hawavutii.

Mtu pekee wa kuzinusuru kampeni za Magu ni Lissu.
Tatizo vijana wa sasa hawataki kujenga hoja. Watasifia tu, ukiuliza unatukaniwa mama yako.

Kuhusu Lissu tungoje hiyo siku.

Sent from my POT-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Kwenye hizi kampeni CCM wanalo...hivi ushawasikia wakipiga ule wimbo pendwa.....waacheni waandamane eeh...wataisoma namba?....theya already know karma is a bitch.
 
Na Lissu anatakiwa sasa aanze kumtandika law hizi kejeli zake kwa wapiga kura.

Huu ubaguzi haukubaliki hata kidogo.
 
PANGANI....

Kwa hiyo Dkt. Magufuli aache hadaa,
Mkuu mbona jimbo la bunda vijijini hujalitaja halina hata barabara ya lami mbunge wake si ni ccm boniface getere kwa nini huko hakupeleka maendeleo?
 
Hapa hakuna mshindi..., kuna One Big Looser nae ni Tanzania....

Tunavunja misingi ya UTU kwa kudhani tunatengeneza VITU
 
Tatizo la CCM miaka yote ni kudhani watu wooote ni malofa wapumbaf...!!
Wanadhani Watanzania hawatembei wala hawatambui sababu ya umaskini wao!!
 
Handeni na kilindi huko Tanga watu wake hawana taarifa kama binadamu anatakiwa kuishi kwa furaha ni shida kubwa ya kutisha kipindi Godwin Gondwe 'double G' akiwa DC kule kuna wakati kulikuwa na njaa alikuta watu wanakula maembe machanga na wengine wakishindia udongo hadi alilia.

Huko Dodoma majimbo mengi likiwamo la Kongwa njaa huwa haichelewi utawakuta wagogo wanakusanya funza (caterpillar) na kwenda kuwakaanga kiungo ni chumvi.

Sasa koote huko ccm imetamalaki na hakuna chama kimewahi gusa huko na ndo makao makuu ya umasikini hapa tz halafu utakuta mtu anashusha shudu kwamba majimbo ya upinzani hayapi kitu huu ni upuuzi wa kutupwa kwani mkoa wa Dodoma wasingekula funza kipindi cha njaa.
 
..kodi anakusanya nchi nzima.

..lakini maendeleo anapeleka walipochagua ccm tu.

..na haoni aibu kusema mambo hayo.
Magufuli anastahili kuchapwa fimbo nyingi tu. Sababu ni muuaji wa maendeleo ya wanainchi. Sote tunalipa kodi, maendeleo ni kwa kila Mtanzania.
Magufuli apigwe tu, hamna namna.
 
Hajajua kuwa Mara ni mkoa wa kina Mura. Hawarembi. Watamfurumusha huko. Alipoingia Mara aliona kibao kimeandikwa "KARIBU MKOA WA MARA"???

Napata taabu sana tunapo jiridhisha nafsi zetu kwa kudhania tunavyo fikiria na kupendezwa ndio utakuwa ukweli on the ground. Hali hii inapunguza uwezo wa kuweka jitihada za kueneza Injili ya Chadema katika hizo sehemu hizo.

Mkoa wa Mara naona kama vile tunaupoteza. Tuata elewa mambo mengi na kuona uwezekano wa matokeo kadiri muda unavyo kwenda.
 
Mkuu una uhakika no 10. UKONGA ni jimbo masikini sana?
umetumia vigezo gani kusema UKONGA ni maskini?
 
Unategemea Magufuli awaombee kura wapinzani?
You're wrong bro! Nisawa na Lissu kumuombea kura mgombea ubunge Ccm. Utakuwa ni ukichaa.

Magufuli nimgombea wa nafasi ya Uraisi kupita Ccm na anapofanya kampeni ni lazima awaombee kura wagombea wengine wa ubunge na udiwani wa Ccm.
 
Ngosha hakufaa hata kuwa kiongozi wa kata,
Ni mkabila,mtu wa visasi,ana Elimu kubwa,lakini akili hakuna,
 
Magufuli amepwaya mno haamini macho yake kwa jinsi alivyokutana na upinzani imara kabisa, amebakia kufoka, kutisha, kubwabwaja na kupayuka tu.
 
Hatukatai yeye kuwaombea wabunge wa CCM kura.

Tunakataa kuwaambia wananchi, msipomchagua wa CCM , siwaletei maendeleo.

Kumbuka yeye ni Rais hadi sasa
 
Mkuu una uhakika no 10. UKONGA ni jimbo masikini sana?
umetumia vigezo gani kusema UKONGA ni maskini?
Dsm yote nimetembea.

Ukonga ndio jimbo lililofubaa hatari.

Nenda Majohe, Mwanagati, Kipunguni, huko bombambili, n.k

Hakuna barabara, kuna njia za ng'ombe..

Umeme wengi hawana, walionao unatoka kisarawe.

Maji ya Dawasco hayajafika.

Wanachimba visima, wanaoga na kunywa ya chumvi.

Nimeishi huko najua..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…