MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Haya ameyasema rais Magufuli kwenye hotuba yake ambapo amesoma takwimu za uwekezaji wa Wakenya Tanzania. Amesisitiza umuhimu wa kudumisha undugu na kuendeleza ushirikiano kwa hali zote.
Akatoa mifano ya makabila ambayo yapo Kenya na Tanzania, wakiwemo Wajaluo na Wamaasai jinsi wanavyoishi bila kuchoreana mipaka hii ya mzungu.
Kuna mengi waliyokubaliana na rais Uhuru hususan kuhusiana na shughuli za baina ya nchi zote mbili, na wakaamrisha mawaziri husika kuratibisha kabla mwaka huu haujaisha. Watakutana Tanzania na kuanza mikakati ya kuboresha makubaliano yao.
Rais Magufuli amekaribishwa kirasmi na kupigiwa mizinga 21 ya heshima. Hii hapa video ya hotuba yake.