Kupitia mitandao ya kijamii, kama wananchi, tunataarifiwa msafara wa rais wetu ulisimama ktk foleni, rais wetu akatoa maamuzi ya kutaka kutembea kwa mguu, sasa kama wananchi tunajiuliza
1. Suala la usalama na wanausala wa Kenya wanalichukuliaje kwa kiongozi mkubwa kama rais ambaye hupatikana kwa gharama kubwa kiuchumi?
2. Kwa kuzingatia sura ya matukio ya ugaidi yanayoikumba nchi yenu, je ni mpango mkakati gani ulikuwa unaendelea kwa msafara wa kiongozi wetu?
3. Licha ya tabia ya rais wetu kuwa na ziara za kushtukiza lkn kwa hili ilikuwa tofauti kwani taarifa mlizitoa wenye siku mbili kabla, je ni sehemu ya dharau kwa rais wetu?
Tafadhari, tungependa mtuoneshe upendo kama tunaowapa mkija kwetu.