Yesu aliwahi nae kuwachota masikini akili
Akawaambia ati ni rahisi kwa ngamia kupita kunako tundu la sindano kuliko tajiri kuuona ufalme wa Mungu
Acha masikini washangalie ---- yesu ilipofika jioni akaingia kwa zakayo akala chakula cha jioni
Daaah -- nimecheka sana katika hiyo scenario "
Kwa namna moja au nyingine nakubaliana na wewe kabisa without any doubts. hakuna jambo baya na lenye fedheha kubwa duniani kama umasikini
Imagine leo unafanikiwa ati masikini wanasema wewe ni Freemason, mara sijui unatumia ndumba, wakati wewe ukifanya kazi wao wanakuona, ukihenyeka wao walikutazama, kipindi ukisota hawakukuambia wewe ni Freemason, subiri utusue utasikia kila hadithi.
Masikini wanapenda kutiwa moyo hata kwa upuuzi.
Ili ujue masikini ni watu wa ajabu, embu ona hii; Matajiri wakipondwa na mtu yeyote huwezi kuwasikia matajiri wakilalamika au kunung'unika, pengine usisikie hata wakitoa maoni yao. Kwanza huo muda hawana. Kama watasikia wataishia kucheka na kumdharau aliyeongea mashudu yake, pengine wamuone alikuwa anatania. Lakini Njoo kwa masikini. Masikini watolee maneno ya kawaida tuu, labda waambie masikini ni wavivu, wazembe, na wapenda miujiza kwenye maisha. Utawasikia masikini wakija juu, ooh! unadharau, ooh! aliyekupa wewe katunyima sisi, mara oooh! Ipo siku yangu tuu wakati limeshinda limelalal au kijiweni halifanyi kazi.
Matajiri mbona wao wapo kimya, Yesu mwenyewe aliwapiga kijembe akiwaambia ni vigumu wao kuiona pepo lakini walijua wapi watamnasa, walijua kwenye sadaka na zaka atakamatwa, kwenye ujenzi wa hekalu, kwenye kula na malazi.
Masikini ndio walimsulubisha Yesu, matajiri wakamtafutia mafuta ya kuupaka mwili wake alipokufa, kisha tajiri mmoja akajitolea kaburi lake litumike kuuhifadhi mwili wa Masihi.. Matajiri ndio waliomletea Yesu zawadi siku alipozaliwa.
Angalia hata watakaomchukulia na kumdhamini mgombea yeyote hapa Tanzania na duniani kwa ujumla ni matajiri.
Kosa kubwa ambalo mtu anapaswa kujihadhari nalo ni kuwatetea masikini, masikini hana umoja, masikini ni mnafiki, masikini hana shukrani, wote waliowatetea masikini waliishia pabaya na hawakupata msaada. Muangalie Lisu anavyohangaika huko Ulaya, alafu muulize anaowapigania wanasemaje juu yake, au muulize masikini yeyote anamchukuliaje Lisu. Utashangaa.
Lakini ukiwatetea matajiri kwanza utapata ujiko, utapeleka tonge mdomoni, ikiwezekana utapata cheo. Huoni watu wanahangaika kumtetea Magufuli, wanajua ukimtetea mtu tajiri naye atakutetea lakini masikini utashangaa atakavyokuacha solemba.
Waulize kina Mdude Chadema, waulize kina Ben Saanane, wote hao walichagua kundi bovu.
Ujumbe huu sio wa wakwako